Jinsi ya Kuacha ku-'Cheat' Mwenzi wako... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya Kuacha ku-'Cheat' Mwenzi wako...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Allien, Feb 17, 2011.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Jinsi Ya Kuacha Ku-Cheat

  Kwa sababu mbalimbali watu katika mahusiano wanaamua ku-Cheat wenzi wao. Wakati mwingine wanajisikia vibaya lakini hawaachi. Wanakuwa trapped, na hivyo kuifanya iwe tabia yao as long as hajashikwa. Wakati mwingine Cheating inachochewa pia na mahusiano mabaya na mwenzi wako, visasi na migogoro isiyotatuliwa katika mahusiano. Kuna sababu nyingi kwa nini Wenzi Wanacheat, hizo tutaongelea siku nyingine.

  Wataalamu wanasema wakati mwingine ni vigumu kuacha Cheating kwa kuwa ni Addiction hata kama Ku-Chaet si kuzuri. Inasemekana unapocheat unajisikia uko fulfilled kwa namna Fulani. Ili uache unahitaji mahitaji kama: emotional au physical, yatoshelezwe na Mwenzi wako. Ikishindikana kuacha inakuwa ni ngoma nzito.


  Hata hivyo hatima ya mwisho ya Cheating ni kujisikia Guilt; Aibu nk. Cheating haiongezi furaha katika mahusiano. Kwa kukusaidia inawezekana kabisa ukaacha Cheating. Zifuatazo ni dondoo zitakazokusaidia kuacha Ku-Chaeat:

  1.Kwanza kaa chini na jiulize kwa nini Una-Cheat, Hii itakusaidia kukurudishia akili yako ya kibinadamu na utashi juu ya chaguzi zako katika maisha. Kitendo cha kuelewa tu ni kwa nini unatabia ya namna Fulani ambayo huiachi ni msingi mkubwa sana wa kukusaidia kuacha.

  2.Chunguza values zako za maisha na jiulize kama Cheating ni moja kati ya hizo values zako. Hata kama umetokea katika familia ambazo Cheating ni kitu cha kawaida, lakini si lazima ukubaliane na chaguo la familia. Kataa.


  3.Jiulize tena kama Kum-Cheat Mwenzi wako kunakuongezea au kukupunguzia heshima na je kwa kufanya hivyo, unamheshimu au haumheshimu mwenzi wako. Faida yake ni nini?

  4.Fanya marejeo ya mahusiano yako na uangalie ni wapi pana mapungufu katika mapenzi na Intimacy. Hii itakusaidia kujua mahitaji yako ya kimapenzi. Ukishagundua ni rahisi sana kwako kuongea na mwenzako kwa uwazi mahitaji yako ya feelings na emotions. (NB: Tutajadili siku nyingine ni vipi uanweza kuongeza au kurejesha mapenzi kwa mwenzi wako).
  Ongea na mwenzi wako kwa uwazi ni nini hasa anategemea u kutarajia kutoka katika mahusiano yenu ili kuboresha mapenzi na mahitaji yenu. Mweleze kwa uwazi hisia zako ni nini pia unataka kutoka kwake. Make her your best lover and friend. Traet your lover. Spoil her.


  5.Achana kabisa na kata mawasiliano ya mara kwa mara na Kimada wako ya SMS na ya Simu. Acha kuwasiliana naye kwa email na kuchat online. Mblock au badili ID. Mpotezee. Ni kazi lakini kuwa jasiri. Inawezekana.

  6.Kumbuka unaye Mwenzi na Familia yako ambao wote wanakupenda; kukuthamini na kukuheshimu na kuwa una Ahadi nayo. Hao ndiyo source peke yake ya furaha na Amani ya kweli kabla hujafa.

  7.Achana na kufikiria mapungufu uliyonayo na vipi utayapata kwa njia haramu na jizuie hisia zako za kukutana na Kimada wako na weka azimio la kuachana naye. Mweleze ukweli Kimada wako kuwa huwezi kuendelea na uhusiano huu. Ataumia, lakini ni bora kwa Mwenzi na familia yako kama unaipenda.

  8.Kumbuka huwezi kuacha Cheating mpaka umechukua uamuzi huo “Mzito” wa kuacha. Usisubiri “The right moment” ili uache Ku-Cheat. Just stop. Just Do It Right Away, Now. Immediately.


  9.Fikiria madhara ya Ku-Chaet yatakuwa nini utakapokamatwa. Aibu na fedhea na guilt.

  10.Kutana na rafiki zako wa Kike na wa Kiume ukiwa na Mwenzi wako na usifiche kitu. Usiwe na miada yap eke yako unless ni very genuine. Uvae utu upya kwani wa kale umekwisha.

  11.Angalia jinsi ambavyo wewe, mwenzi wako na familia yako mlivyobarikiwa. Je huna shukrani? Ndo jinsi ya kushukuru kwa ku-Cheat?

  12.Acha kabisa kum-criticise mwenzi wako na kumlinganisha na Kimada wako. Heshimu sana hisia na TRUST ya Mwenzi wako na Tumia muda mwingi na Mwenzi wako na Familia. Pia jizuie kuwa negative juu ya maisha yenu na mahusiano yenu. Stay positive and focused.


  13.Kama unafikiri Kimada wako ni bora kuliko mwenzi wako wa sasa, napenda kukujulisha kuwa ni aslimia 5% ya mahusiano ambayo yanatoka na Cheating yatafanya kazi. Kwa hiyo hutaenda popote. Stop. Acha ubinafsi na mrudie mwenzako na muumba wako. Huna haja ya kuleta msongamano ndani ya mapenzi. Jiweke pembeni na mpenzi wako wa Ahadi.

  14.Kwa kumwacha Kimada wako huwezi kufa bali utakuwa na Amani moyoni. Hata kama utaona ni vigumu kumwacha. Just stop. Katika kipindi cha wiki 3 baada ya kufanya uamuzi “Mzito” utakuwa umeshafaulu kiakili na utaweza ku-overcome feelings za withdrawal.

  15.Chukua muda kufanya matengenezo na marekebisho katika ndoa yako. Jifunze jinsi ya kufanya mambo tofauti. Kama huwezi kukubaliana na hilo basi utawezaje kuacha. Fanya maamuzi sasa.

  16. Mrudie Muumba wako. Tubu. Omba msamaha kwa muumba wako. Anza maisha yako upya. Shiriki katika mambo ya mungu na kijamii. Find new interests kufidia muda na pengo "hewa" la Cheating"

  Allien
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Somo zito mkuu na nashukuru kwa ushauri wako. Nitazifanyia kazi hizi hoja.
   
 3. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  LOL Mkuu umenichekesha . . .

  Kwani wewe ni active member sasa hivi?
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii ni nondo ya haja inayohitaji utekelezaji, asante mkuu!!!
   
 5. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Baada ya kupata lawama kwenye post ya kufundisha watu ku-cheat sasa waliokulaumu watakuwa wamekuelewa. Yaani kama vile fundi lazima ajue kujenga na kubomoa pia.
   
 6. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Tuko pamoja Mkuu BL.

  Respect.
   
 7. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  JN . . . LOL hayo ndo mambo ya JF Mkuu.

  Tuko pamoja na kitaeleweka tu.

  Respect sana.
   
 8. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh! Big up baba, I am sure they are alot of victims in this forum. Lol.
   
 9. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Bora uwafundishe kuwa tunawapenda na kuwathamini kuliko hao vimada wao wanakokwenda kula raha wakati wa shida wanarudi kwa wake zao....thanks Mkuu......:coffee:
   
 10. LD

  LD JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante kwa somo zuri nitalitumia vizuri mpaka mbele ya safari huko!!!
   
 11. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,498
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  :amen::amen::majani7:
   
 12. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Tuko pamoja Mkuu.

  Respect.
   
 13. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  LOL . . . No matter what, Home is always the best and its where u belong.

  Tukimaliza series tunaanza Motivational Talks ya kujenga society ya maadili without Cheaters.

  PIC has a job to do . . . . LOL

  Respect.
   
 14. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Tuko pamoja LD. I hope wewe si mwathirika wa issue hii . . .
   
 15. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Respect Kamanda!
   
 16. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  you bet!!
  Nitaanza kujirekebisha kidogokidogo...I'm getting there
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Allien,

  I like this thread and your post number 1, we need to advocate for this tough decision... but a bigger challenge is sometime a partner, you mayd ecide to do all that only to come home to find maudhi yanazidi even more
   
 18. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  One Page.

  Respect.
   
 19. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mkuu; believe me inawezekana kabisa no matter ana maudhi kiasi gani. Tutaendelea kuelimishana how that one can be achieved hasa kama mtu haelewi somo.

  karibu Private Intelligence Club kuna mengi Mkuu.

  Respect.
   
 20. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umetupatia shule ya maana. Kwa kuanzia, Sasa hivi tu nimedelete contant ya 'kimeo'

  Big up Allien!
   
Loading...