... wagogo au wachaga hayo mabucha?Goba ndiyo wahuni kwelikweli nyama inauzwa kilo sh 5000 lakini ukinunua kilo kuanzia tano ujue unanunua kilo Tatu tu,ni wezi balaa Goba center
Hata mbezi mwisho huu mchezo upo Sana na. Pia nimeambiwa hata wanapouza mchele na maharage nao wameanza huo nchezoTegeta kwa ndevu pale ni balaa, niliwahi kununua nyama kilo 3, nikaenda kwa mama muuza mchele nikamuomba anipimie ile nyama kwenye mzani wake ukasoma 2.25 kg nikarudi kwenye ile bucha nikawaeleza waipime tena upya maana na mashaka na kipimo huku nikiwa mkali kweli kweli, wale vijana walichukua jiwe lingine chini ya meza na kunipia upya, nikarudi tena kwa yule mama kupima ikasoma 3kg, yule mama akanieleaza kuwa huo ndiyo mchezo wao pale, kuanzia siku hiyo niliapa kutonunua nyama wala samaki pale.