Jinsi wauza mihadarati walivyoteka hoja za wabunge,hoja ya ukosefu wa chakula ilivyozikwa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,004
Sasa bunge letu likijumaisha wabunge toka vyama vyote limedhihirisha jinsi lilivyosheheni wahalifu. Steve Nyerere kwa kutumia laki nne tu aliweza kuwa badilisha wabunge kujadili suala la kukamatwa wauza madawa na kuwatetea na kuacha kujadili hoja ya chakula.

Hawa wauza madawa ni akina nani? ndio wadhamini wa wanasiasa? kwanini Steve alihakikisha Mbowe na Zitto wanakuwa katikati ya ajenda?

Nini kinawapeleka kiburi wanasiasa kujipongeza na kujisifia hadharani kufifisha biashara ya madawa ya kulevya?

Steve ametumia Ushawishi gani hadi kubadilisha vipimo vya mkemia mkuu kuonyesha bangi badala ya heroine? Je ni kweli alikuwa na laki nne za Tanzania au dola laki nne?

Ni kweli kwamba wabunge hutumika na "mabwana" zao? Ikumbukwe Zitto alianzisha hoja ya upungufu wa cha kula hadi kupinga takwimu za PM,kwanini hakuzungumza bungeni au wauza mihadarati walitoa hela nyingi zaidi ya wauza mahandi?
 
Iendeleze wewe hiyo unayoiita hoja ya ukosefu wa chakula. Kwani umeajiri watu wa kukusemea au kukuanzishia hoja? Wewe umefungwa mdomo? Wewe huyo huyo ndiye uliyekuwa kimbelembele kuwaita wenzio wachochezi halafu leo eti hoja ya ukosefu wa chakula imezikwa? Yaani kama huo ni upofu basi ni wa kiwango cha lami.
 
Mbona una panic?
 
Mimi nimeona hakuna haja ya kupiga kura aisee!!! Kwa namna ya wanasiasa tulionao?? Wasiyoweza kutetea wanyonge Bali madawa ya kulevya??/aaaah!! Wanakatisha tamaa
 
Na tatizo la chakula ndio 70% ya inflation tunayoishuhudia. Less than a week mtungi wa gesi 13kg umetoka 45K to 52K kwa dsm.
Mfalme Suleimani aliomba Hekma tu toka kwa Mungu, sijui viongozi wa Africa hua wanaomba nini?. Nauliza tu ila wengi huomba heshima instead na wasipoipata ndio miujiza inaanza.
 
Mkuu Siku Hizi Post Zako Zimekua Za Umbea Kama Taarabu Ndiyo Mana Wachangiaji Hawavuki Hata Page Mbili Jitafakari Punguza Mihemko Utaokota Makopo Ushauri wa Bure Hii Hali Siyo ya Kawaida Kapate Vipimo.
 
Hii ni JF madini ya ukweli Hupata wachangiaji baada ya miaka kadhaa,wengi wenu yaliyomo humu hamuyaoni
 
Back
Top Bottom