Jinsi Wanaigeria wanayowatapeli Waafrika wengine mitandaoni

Jinsi Wanaigeria wanayowatapeli Waafrika wengine mitandaoni

thegreat1510

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,525
Reaction score
4,047
Wakuu,

Mimi ni miongoni mwa wahanga wa ishu za online, katika harakati zangu za kutafuta side hustle online nilichokuja kukigundua job za online zina ma scammers wengi sana na wengi ni Wanaijeria

Wanaigeria wengi unakuta wanatumia profile za wazungu na wanadai kabisa wako USA ndivyo wanavyojitambulisha

Nimepata madili kadhaa fiver lakini pia Facebook kwenye ukurasa wa freelancers, anatokea mtu anadai anatafuta freelancer mfano wa typing, translation, logo design nk. lakini deal 9 Kati ya 10 ni feki.

Unapewa kazi unapiga then anakwambia umtumie bank details akulipe cha ajabu anaomba Hadi kitambulisho chako Cha nida ndio akulipe ukiona hivo ujue huyo ni fraudster.

Utawajuaje ni matapeli hasa wa kinaijeria?

👉Akidai yupo located US mwombe namba za WhatsApp ukiona inaanza na +234, ondoka!

👉Akikuambia umcheki telegram na sio by emails, ondoka! telegram imejaa matapeli.

Pia Kuna wabongo wanaopiga ishu za affiliate marketing, nawaona nawao wamekaa kitapeli Sana! Anakufuata inbox anakuambia ukijiunga unapata pesa kwa njia nyingi Kama ku watch videos za YouTube, au status views lakini actually njia pekee ya kuingiza pesa kwenye hizi platform ni by referral.

Ukijiunga unatoa elf 12 Ila unaambiwa utapewa sh. 5000 kumbe baada ya Kutoa hiyo elfu 12 unapewa sh.300 tu ili urudishe pesa yako unapaswa ualike mtu , mtu mmoja unapokea sh. 5000, naye utamtapeli hivohivo.

Kwa ishu za forex nazo Kuna watu wanapiga forex bila knowledge yoyote wakidai wanapiga copy trading wanatumia broker.

Unakuta Kuna mnaijeria somewhere ametulia anajitangaza anapiga forex wewe unadeposit tu pesa yeye ndiye anatrade ila utakuwa unampa percent kadhaa kwenye faida yako, wengi wanapgwa.

The fact kwamba uelewa wa wanaigeria kuhusu matumizi ya mtandao upo juu kuliko Waafrika wengine, wanatumia fulsa hiyo kuwa scam Waafrika wenzao.
 
Kuna wapopo, wamesababisha teeneger kujiua huko state, wana warubuni vijana wadogo wa high school au college wakijidai ni wadada wanatumia picha fake za watu, huyo mmoja wakamshawishi huyo dogo wa kiume hadi akawatumia nudes, mziki ukageuka wakaanza kum blackmail kwamba wanajua followers wote wa huyo dogo na wata post hizo nudes kwenye social media, walimtaka awape 1000$ dogo akawaambia mnasababisha nijiue, jamaa wakamjibu tena ufanye haraka kujiua kama hutumi hizo pesa hapo walishampa na paypal ac ili atume huo mpunga, dogo alijiua, wapopo wakadakwa walipelekwa state kula mashataka.
 
Unakuta Kuna mnaijeria somewhere ametulia anajitangaza anapiga forex wewe unadeposit tu pesa yeye ndiye anatrade ila utakuwa unampa percent kadhaa kwenye faida yako, wengi wanapgwa.
Unapigwaje hapa wakati huwezi kutoa pesa kwenye account...

Hii kuna dogo anafanya sema yeye anakuwa safe maana account ikipata hasara yeye anakuwa hakuna alichopoteza.
Wewe mwenye account ndio unakuwa umekula hasara.
 
Kwa mfano umepiga dili ya online ya ukweli mfano translation, ikitokea mteja anataka akulipe unatakiwa umpe njia gani ya malipo ambayo ni salama?

Je, ukituma benk akaunti bila taarifa nyingine unaweza kuibiwa pesa?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Unajua Mimi nashangaa sana unakuta mtu anakuamasisha sana ujiunge na Forex au network marketing..na usipojiunga anakuchukia kweli kweli
Unakuta kashapigwa , kwahiyo ili arudishe pesa yake inabidi nayeye apige wengine
 
Kuna wapopo, wamesababisha teeneger kujiua huko state, wana warubuni vijana wadogo wa high school au college wakijidai ni wadada wanatumia picha fake za watu, huyo mmoja wakamshawishi huyo dogo wa kiume hadi akawatumia nudes, mziki ukageuka wakaanza kum blackmail kwamba wanajua followers wote wa huyo dogo na wata post hizo nudes kwenye social media, walimtaka awape 1000$ dogo akawaambia mnasababisha nijiue, jamaa wakamjibu tena ufanye haraka kujiua kama hutumi hizo pesa hapo walishampa na paypal ac ili atume huo mpunga, dogo alijiua, wapopo wakadakwa walipelekwa state kula mashataka.
dah! inasikitisha sana
 
Kwa mfano umepiga dili ya online ya ukweli mfano translation, ikitokea mteja anataka akulipe unatakiwa umpe njia gani ya malipo ambayo ni salama?

Je, ukituma benk akaunti bila taarifa nyingine unaweza kuibiwa pesa?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Bank transfer iko safe , Ila mpe namba tu na jina la bank labda , hakuna fraudster anaweza kuhack bank account yako kwa kutumia number yako tu
 
Ukijiunga unatoa elf 12 Ila unaambiwa utapewa sh. 5000 kumbe baada ya Kutoa hiyo elfu 12 unapewa sh.300 tu ili urudishe pesa yako unapaswa ualike mtu , mtu mmoja unapokea sh. 5000, naye utamtapeli hivohivo.
Hahaha...
Wizi wa hivyo umekithiri WhatsApp wakitumia picha za pisi kali
 
Wanigeria ndio wamechafua sifa za waafrika pote Duniani,hata ukivaa suti nchi za watu uaminiki wote mnaonekana ni vibaka tu
 
always pay attention...otherwise you will end up paying somebody.
 
Back
Top Bottom