Jinsi wanachuo wanavyoweza kufaidika na Mkopo

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Habari wakuu jukwaani leo tutaangalia vipi Mwanachuo anavyo weza kufaidika na Mkopo wa elimu ya juu kwenye kuwekeza. Awali ya yote Turudi nyuma kidogo kwa kuelewesha haya.

Hakuna mwanachuo Miaka hii asiyejua kwamba kuna tatizo la ajira nchini Tanzania na hilo ndo limekufanya ukaumiza kichwa sana kwenye kozi ipi ya kusomea hivyo Mwanachuo akiniambia hajui hilo nitashangaa maana huenda hajui hata anacho somea. Uwa nasema kama nikiambiwa nitaje kundi la watu masikini itakuwa kazi ngumu sana kuacha kundi la wanachuo kwa sababu kwanza wengi wao bado ni tegemezi kwa wazazi na walezi wao yaani hawana sehemu mbadala ya kuwaingizia kipato mbali na hilo wanadeni na wengine wanaendelea kukopeshwa na HESLB kwa hali hii siwezi kuacha hili kundi kama kundi lililopo tano bora ya umasikini. Si kwamba najaribu kuwakebehi wanachuo hapana bali ni maisha yaliyopo huenda na mimi nilikuwa au bado ni Mwanachuo. yani nimesoma vizuri hesabu ya hasi na chanya kwamba (0) Ni Kubwa Kuliko (-1) . Na yaha ndio maisha yaliyo baki.


Wanachuo wengi wanapenda kuwekeza lakini tatizo utakuta wanalalamikia muda na mazingira sio rafiki kwao na kweli muda unaweza kuwa tatizo kutokana na ratiba ya chuo lakini leo napenda kukushirikisha uwekezaji mzuri na ambao unaweza kukuinua kichumi sio kitu kingine ni uwekezaji katika HISA, huu ni uwekezaji ambao utakupa muda wa kufanya mambo yako mengine na pia utaweza kufatlia kile ulichowekeza popote pale ulipo ni kuwa na simu ya mkononi inayokuwezesha kuingia mtandaoni, ni uwekezaji ambao unaweza kukupa fursa ya kujua hata masoko mengine ya biashara yanaendaje yaani hapa uwe mtundu wa mitandao kama ulivyo ijua JamiiForums.

jinsi ya kuwekeza cha kwanza fahamu soko la hisa la dar es salaam ni nini.? Bila shaka upo uzi wake humu.
pili je kampuni unayotaka kuwekeza imejiandikisha kwenye soko la hisa la dar es salaam.? tatu fahamu kampuni Ipi inafanya vizuri kwenye mauzo.? nne kiasi gani cha fedha kwa kila hisa moja.? au unaweza tembelea kwa mawakala wakakuelewesha .

kwanini mwanachuo?
Nimekushauri wewe mwanachuo hasa unayefaidika na mkopo kwa sababu unapata pesa kwa mkupuo kwahiyo unaweza kufanya uwekezaji wa muda mrefu na wengi Hutumia si zaidi ya 5000 kwa siku na wakati pesa unayopewa ni sh.8000 kwa siku kwhiyo unabakiwa na 3000 kwa siku ambayo kwa miezi miwili inakuwa ni laki na themanini(180000) na kama ukitumia 80000 tsh kuwekeza kila boom linapotoka ndani ya miaka mitatu utakuwa umefanya uwekezaji wa zaidi ya hisa 200 katika kampuni ambayo imekufaa maana kuna kampuni kama CRDB inauza hisa kwa Kiasi kidogo cha fedha na kuna kampuni nyingi zenye hisa ya bei ya chini ambayo unaweza kuwekeza na badae ukapata pesa yako mar
adufu.

changamoto.
kila biashara au uwekezaji unachangamoto katika hisa changamoto ya kwanza ni kwenye kutambua ni kampuni Ipiipi inafanya vizuri kwenye manunuzi hii ni changamoto kwako maana itakuitaji muda kupitia takwimu za kifedha za kampuni husika (financial statement), uimara wa uongozi wa kampuni historia ya kampuni katika mauzo kwahiyo itachukua muda kidogo na umakini unahitajika kabla ya kuwekeza.

•changamoto ya pili ni kwamba unapokuwa mwanahisa wa kampuni fulani unakuwa ni sehemu ya umiliki wa kampuni kwahiyo ukubali vyote faida na hasara kampuni ikipata hasara na wewe umepata hasara ikipata faida na wewe umepta faida kwahiyo hiyo nayo ni changamoto ya kujiaandaa kwa mapokeo.

Hitimisho na ushauri
unaposema neno mwanachuo katika miaka hii ya kizazi kipya kwenye jamii zetu kwa bahati mbaya unajenga picha ya Mbaya katika fikra za watu ambao hawajafika chuo ni dhana ambayo tumeijenga sisi wenyewe wanachuo wala siwezi wahukumu wanajamii ni haki yao kusema hivyo maana wanachuo wenyewe wameamua hivyo kuwa maisha yao kuyajenga kwa muonekano huo. lakini ukweli ni kwamba hayo maisha unayoishi sio yako ebu jaribu kuangalia wenzako waliomaliza chuo wapo mtaani wakiishi maisha yao halisa maisha ya kujipaka mafuta ya mgando sio Mafuta ya gharama tena maisha ya kuvaa nguo mpauko sio jinsi kali, tena maisha ya kukosa hata mia tano ya vocha, nausijifanye huwaoni hilo ni darasa tosha kwako haitaji tena ubishi na kwamba nitoe maneno mengi kuhusu hilo.maana unajua kabisa kwamba utaondoka tu chuoni na muda wa boom utaisha na utarudi tena mtaani utake usitake.

Tumia Mkopo wa chuo kuwekeza kwenye maisha ya baadae.
Kataa Maisha ya starehe chuoni wekeza kwenye maisha ya kawaida.
 
Back
Top Bottom