Jinsi unavyoweza kuwageuza wajinga kuwa fursa

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,692
Wiki iliyopita nilileta uzi wa kumuelezea rafiki yangu Hosea Chamungu aliyetumia ujinga wa Watanzania wengi kujikwamua kimaisha, baada ya kutoka masomoni Kenya na kurudi Tanzania na kukumbana na Sakata la uhaba wa ajira.

Leo, nawaletea mtu wangu wa karibu tuliyesoma nae chuo kikuu Mlimani (UDSM), japo Mimi mwaka wa pili sikuendelea na chuo kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wangu , japo kwasasa nimeshahitimu Degree .

Huyu bwana anaitwa Mwasha , tumepishana mwaka mmoja, mimi nimezaliwa 1993 yeye 1992, alinitangulia kuhitimu Elimu ya juu hapo UDSM kama nilivyosema awali,

Alipohitimu Na yeye alikutana na Sakata lile lile linalotukumbuka vijana linaloitwa UHABA WA AJIRA ,

Hakumlalamikia mtu wala serikali, nilipotezana nae kwa muda kidogo maana mimi masomo niliishia njiani .

Mwaka jana nimekutana nae akiwa ndani ya Range Rover nyekundu na mkewe.Tukasalimiana akanialika kwake, nilipanga siku nikaenda kuonana nae.

Nilimuuliza siri ya utajiri wake wa haraka hivo, majibu yake yalikuwa ya shortcut sana ila main point ilikuwa ni kuwatumia wajinga kama fursa na kunisihi niache kulialia na kuilalamikia serikali.

Anauza mafuta, maji, vitambaa kwa mgongo kuwa vina upako na anavitoa Israeli, maji anasema anayachukua mto Yordan.

Na sasa tayari ameshafungua kanisa ana waumini wengi sana hapa Dar. Maombi yake kuna kulipia kiasi cha pesa.

Kwasasa tayari ameshajenga nyumba ya kisasa, na ana magari ya kubadilisha ana miaka 27 tu.

Kitu ambacho najiuliza hadi leo kuanzia kwa Hosea Chamungu na huyu Mwasha hii sayansi ya kunena, hizi wanazoita kunena kwa lugha na kuwaangusha chini watu kwa kigezo wana mapepo wanajifunzia wapi, hili swali wote waligoma kufunguka.

Kwasasa yupo Dar -Bunju, Kilimani. Ana kanisa na anafanya hapo mazingaombwe (miujiza fake) na kuuza mafuta, maji na vitambaa.

Jina alishabadilisha anajiita NABII NA MTUME Mwasha

SWALI: Ni halali kuwageuza wajinga fursa?


Yeremia 14:14,16

“Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao. Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.”

Yeremia 23:31-32

“Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.”

KUNA MWINGINE NILISOMA NAE SECONDARY, CHUO KIKUU AMEMALIZA SUA, TAYARI SASA NI NABII.

Nitamtembelea kuendelea na utafiti wa WAJINGA KUGEUZWA FURSA

FB_IMG_1574938016858.jpeg
FB_IMG_1574937997902.jpeg
FB_IMG_1574937975467.jpeg
FB_IMG_1574937953069.jpeg
FB_IMG_1574937911441.jpeg
 
huu ni wivu!ndo mana wengne wakikutana na watu walikuwa wakiwafahamu huwakanamkuu kwenye maswala haya huwezi kumbadilisha mtu kirahisi,kuna watu walimuona live nabii akivunja amri 6 na kondoo na wakakataa si yeye!
Nilijua watu kama nyie lazima muwepo

Lazima mkiona mambo kama haya yakiwekwa wazi mtakimbilia

NI WIVU

MARA USIMSEME MPAKWA MAFUTA

MARA USIHUKUMU

nategemea majibu kama haya

Mimi hawa manabii na mitume waliopo dar wananijua huwa nawaweka kitimoto ,

Maandiko yametupa Mandate kuwachunguza , Na wengi ni watu wangu wa karibu
 
kwanza elewa mimi ni muislam,na siwatetei hao manabii feki kwa sababu kila mwenye akili timamu anajua ni feki,point yangu ni kwamba huyu si mwanao mshkaji wako kwa nini unamchomasasa mtu anapewa mafuta amwage shamban ili mazao wawe mengi nae anafanya hivyo unadhani mzima kichwani huyo??
Nilijua watu kama nyie lazima muwepo

Lazima mkiona mambo kama haya yakiwekwa wazi mtakimbilia

NI WIVU

MARA USIMSEME MPAKWA MAFUTA

MARA USIHUKUMU

nategemea majibu kama haya

Mimi hawa manabii na mitume waliopo dar wananijua huwa nawaweka kitimoto ,

Maandiko yametupa Mandate kuwachunguza , Na wengi ni watu wangu wa karibu
 
kwanza elewa mimi ni muislam,na siwatetei hao manabii feki kwa sababu kila mwenye akili timamu anajua ni feki,point yangu ni kwamba huyu si mwanao mshkaji wako kwa nini unamchomasasa mtu anapewa mafuta amwage shamban ili mazao wawe mengi nae anafanya hivyo unadhani mzima kichwani huyo??
KAMA MUISLAMU SAWA

Ila sisi wakristo biblia inatupa mandate ya kuwaweka hadharan bila kupepesa macho
 
Acha kila mtu aamini anacho amini,nchi yetu imefika hapa kwasababu ya misingi hiyo hao unaowaita wajinga hawaji kuomba ugali kwako,ukiwa unaumizwa na mambo yasiyokuhusu unajitafutia kufa mapema,yapo mambo mengi mabaya unayoyafanya ila Mungu anakuvumilia,usijifanye kutoa mabolit kwenye macho ya wenzio ikiwa wewe una banzi.
 
...nimependa sana ujasiri wako;..unawapepeta manabii feki with evidence.
....hiyo ndio karama yako Mungu kakupa na unaitumia vema - God bless you and don't give up the fight.
Ngoja nikariri jina lake kabisa...
 
Acha kila mtu aamini anacho amini,nchi yetu imefika hapa kwasababu ya misingi hiyo hao unaowaita wajinga hawaji kuomba ugali kwako,ukiwa unaumizwa na mambo yasiyokuhusu unajitafutia kufa mapema,yapo mambo mengi mabaya unayoyafanya ila Mungu anakuvumilia,usijifanye kutoa mabolit kwenye macho ya wenzio ikiwa wewe una banzi.
Najua nagusa maslahi yenu

Hivo tulieni hivo hivo
 
SISI WAKATOLIKI tunataka watumishi wa kipentekoste waishi kimaskini kama MAPADRE wetu kwakuwa sadaka zao wanapeleka ROMA kwa MABEBERU,

Wakatoliki tuache kuwaonea wivu walokole, kitu ni kimoja , watu wamjue kristo, no mattter what, Mbona mleta post hajasema DIAMOND PLATINUMZ abnavyoimba matusi tena anawatukana mama zenu kwenye nyimbo, sijui ipke mate iteleze kama nyoka alafu mnapiga makofi huku mkishindwa kujua anawatukania, anawapigisha makofi huku hamuoni?
 
Back
Top Bottom