SEHEMU YA TATU (3)
"Ina maana tungeshindwa kuongea tukiwa pale? Kwanini unapenda kunipelekesha. Kama sikutaka kuondoka, yani kuongea vile ndio ukasirike Stan?" Aggy aliniambia kwa sauti ya Upole; nikamtazama usoni nikiwa nimekasirika, nikamwambia "Twende nikupeleke kwako"
..............................................................................
Aggy aliniambia kitu ambacho nilijisikia vibaya kama Mwanamume, nilijaribu kumuwaza Mumewe, roho ilikuwa ikinisuta. Alizungumza mambo mawili.
La kwanza, Kwa sababu ya kutompenda Mumewe, mtoto anayelea jamaa si wa kwake! Naam, umesikia sawa sawa, si wake, wa nani?
Baada ya kuachana na mimi mwaka 2019, Aggy ananiambia alipoteza dira ya maisha hususan kwenye mahusiano, alisema alikuwa akiwachukia Wanaume wote duniani hata wale aliokuwa nao kwenye mahusiano, moyo wake ulikufa ganzi, jeraha la moyo wake lilisababisha ageuke kuwa Mwanamke mwenye kaliba ya Umalaya, yaani kutoka 2020 mpaka 2021 tayari alikuwa na Wanaume zaidi ya Watano, na anadai alitamani hata kujiuza; hakujihisi kuwa Salama tena, alinitazama mimi kama Mwangalizi, Kiongozi na Mlinzi wake.
Akasema alikuwa na jamaa aliyekuwa anaishi nae karibu, kule maeneo ya Tegeta; huyo Jirani yake ni Mfanyakazi mwenzie kwenye taasisi moja mitaa ya Mbezi beach, walikuja kujuana kama Wanakaa karibu baadae kidogo, na huyo jamaa alihamia kutoka Chang'ombe ili kidogo akae karibu na anapofanyia kazi. Ndipo waliingia kwenye Mahusiano, anadai si kwamba alimpenda, ila mahusiano yao yalitokana na Ukaribu wao.
Anadai jamaa hakuwa anaeleweka, na ni Malaya, so alipata sababu nyepesi ya kumuacha, ndipo mwanzoni mwa mwaka 2022 ukaanza mzozo na mfanyakazi mwenzie, zikaanza harakati za kuhamia kwenye mahusiano na mwanamume aliyekutana nae kupitia harakati zake za mapambo kwenye shughuli kama harusi, jamaa ni mmiliki wa Kampuni, so alipoona mambo yanaeleweka kwa upande wake akaona sio shida atulie sasa.
Yule mfanyakazi mwenzie alikuwa akimsumbua rafiki yake Aggy anayeitwa Stella (jina si halisi), na alikuwa akimuomba warudiane kwamba angetulia, na pale Ofisini wapo waliomuunga mkono, hivyo wakamshawishi Aggy arudiane nae, ila Aggy alishaanza mahusiano na mwengine; huyu wa Pili, ambaye ndiye James (mumewe) alikuwa yupo serious na anataka Mke, alimuona Aggy anamfaa. Aggy alikuwa kwenye dillema, na alichanganyikiwa, dada zake na nyumbani wakawa wanamshauri kama yupo wa kumuoa akubaliane nae, japo yeye hakuwa amempenda yeyote, ikabidi akubali tu. Ila alikuja kujua kama Mjamzito kipindi yupo kwenye mahusiano na wote, ingawa anadai anaijua ni ya nani; alipoona jamaa amekuwa serious kwenda kuposa ndipo akaona shida inazidi kuwa kubwa, hakuwaza, alihisi Wanaume wote wangemzingua tu.
Na Jamaa alimwambia amemposa mapema vile kwa sababu ya ujauzito akijua ni wa kwake. So Aggy alibaki kuchanganyikiwa, akaniambia mpaka ananitafuta mimi alikuwa anataka faraja, akiamini mimi ndiye naweza kumpa (Japo simuamini).
LA PILI, aliniambia kwamba anatamani leo kesho avunje ndoa yake ila tu, nikikubali kuishi nae, na mimi sina maisha, japo akaniambia hilo sio tatizo, tatizo ni kama angenikosa. Hapa ndipo alinitibua. Yeye anadai hana furaha, maisha yapo lakini hataki kuendelea kuwa naye, lakini mzigo wa aibu anaoamini ataubeba ndio unamsukuma kubeba hilo jambo.
Nilichokuja kuelewa ni kwamba; hapa aneyelinda ndoa ni Mume, huyu mwenzangu hajali kama kaolewa.
Mimi kwa upande wangu sitaki kabisa kumrudia Mwanamke niliyemuacha, hata hivyo nipo kwenye mahusiano.
................................................................................
SIKU NANE BAADA YA ULE USIKU.
"Sipendi sana unavyonifokea, nashindwa tu kukujia juu kwa sababu sina ujanja; ila unaniumiza" Ujumbe wa Aggy uliingia jioni mida ya saa 11, nikiwa natoka Magomeni.
"Unadhani nitakuwa nakubembeleza tangu mwanzo? Wewe ni mke wa mtu, siwezi kuleta ukaribu wa mwanzo kama unavyodai, tulia kwako" Nikamjibu.
"Naona imeshindikana njia ya amani, ila Stan wewe ni Shetani na huyo Mtoto wa watu uliye nae usije kumuumiza, una roho mbaya, na kama umegoma hivi utaona" Akanitisha.
Mimi nilisoma zile meseji nikiwa naamini zimeandikwa kweye Mwili mmoja, ila Nafsi tofauti; napokwambia namjua Aggy, namjua namaanisha, nimeishi nae pika pakua kule Arusha wakati anasoma, namjua, tangu 2015. Niliwahi mpaka kumtoa kwao, nikampeleka kwetu; na dada yake alimuuliza ameenda wapi, akamwambia yupo kwangu. Dada yake alipanic, "Stani ni nani wewe mpumbavu, umekuja Dar ili uende kwa Stan?" Alimuuliza nikimsikia kupitia Simu yake aliyoweka LoudSpeaker.
Sasa siku hii nilijua huyu ni Aggy Mwengine; siku ambayo James (Mumewe) ananipigia simu alinipigia kupitia namba yangu ambayo mimi mwenyewe siitumii kupitia WhatsApp, na yeye huwa nachat nae kupitia WhatsApp.
Maswali ambayo niliyojiuliza, ambayo nilitamani hata mumewe ayajue ni haya.
1. Alinipigia kwenye namba yangu ya Halotel, wakati Aggy nilikuwa nachat nae kwa WhatsApp na hiyo namba haipo WhatsApp. This means alimpa.
2. Kwanini alikuwa anachat na mimi meseji nyingine romantic kwa kutumia Tablet ya Mumewe? Got me?
3. Baada ya mumewe kunipigia nilimalizana nae, japo alinipa vitisho ila niliamua kuwa mpole na kumueleza kilichotokea ili asijisikia vibaya, nikakiri kosa, nikamuomba radhi, na baada ya hapo nikamtumia meseji ya "Kutowasiliana nae tena" ila mwanzoni mwa mwezi huu wa kwanza, alinitumia birthday ya Mwanae, sikuijibu nikafuta. Anataka nini?
Nilichokuja kudhihirisha, nikahitimisha kwamba; anataka kumtumia mume wake kulipiza kisasi alichokipanga muda mrefu, labda ndio mana alitaka kupajua kwangu. Alitaka kupafahamu Ofisini kwangu nilimkatalia.
Hiki cha kunitafuta Mwezi huu kuna red flags kilinipa. Nilichoamua kukifanya, nahisi wameshanielewa huko kuwa nipo mbele ya muda kuliko wamavyofikiria wao.
Ijumaa iliyopita; mumewe alinipigia, sikuwa karibu na simu hivyo sikupokea, nikakuta na ya kwake. Ila nilikuta meseji ya jamaa anataka tuongee aniombe radhi, ili tuyamalize.
Huwa sipendi mambo ya Kis*** kama Mwanamume unatumika na mkeo kulipa visasi vyake, mbaya zaidi ukanitishia.
Nitawaambia nilichofanya Mjifunze!
.........................