Jinsi tunavyosumbuka na maisha yasio halisi

Christiba

Member
May 27, 2020
24
32
Ukijifunza kuyachungulia mawazo yako utaona si kitu ila ni mzigo wa mambo yaliyopita na matarajio yajayo, ukifikiria kwa makini utagundua yaliyopita na yajayo yote ni taswira ya fikra tu ila sio maisha yako halisi ni maisha fake kwasababu hakuna anaeishi wakati uliopita wala anaeishi wakati ujao bali sote tunaishi wakati huu uliopo tunaishi sasa hivi unapotoa hewa nje na kuiingiza ndani

Maisha ya binadamu yanasongwa na matatizo, mawazo, visasi na chuki ambayo ukichunguza kwa makini sio vitu halisi bali huletwa na fikra au kwa jina lingine maisha fake(mkusanyiko wa yaliopita (past) na matarajio (future))na kusahau kuwa maisha yako ni haya ya muda huu unaposoma hapa huyo ndiyo wewe. Mtu anatumia maisha yake halisi vibaya(maisha haya ya wakati huu) kuwaza na kukosa raha kuhusu maisha fake yajayo au yaliopita.

Ukitaka furaha na amani inakupasa kuishi kwenye maisha yako halisi ya sasa, jana imepita na kesho hatuijui usitarajie chochote kutoka kwa mtu maana utakuwa mfungwa wa matarajio mpaka kifo, mfano tu maisha ya matajiri si ya kutulia kwasababu ya utu fake kila siku anajitafuta kuwa zaidi ya leo kwenye future anautafuta utu wa taswira za fikra zake anaishi mpaka kufa bila kuwa na amani na furaha ya utajiri wake.

Ishi leo tengeneza hatua nzuri leo weka mawazo yako kwenye leo kwenye wakati huu wa sasa, mfano ukiwa unasafiri kutoka sehemu A kwenda B, kuweka mawazo kwenye hatua unazo piga wakati huo ni muhimu kuliko kuweka mawazo kwenye sehemu B, hatua sahihi ndizo zitakazokufikisha sehemu B, vivyo hivyo kwenye maisha ni kuweka nguvu kwenye kuishi sasa hivi vizuri ili uifikie sehemu B, chuki, msongo wa mawazo na visasi ni vikwazo vya kupiga hatua sahihi kwenye maisha halisi ya sasa. Jitafute leo.
 
Nikilipa deni la mtu au kumsaidia mtu najisikia amani na furaha kubwa moyoni mwangu lakni wapo watu furaha yake moyoni ukamilika anapotenda kinyume chake, unasemaje juu ya hilo.
Post ya Amani ipitayo mema na mabaya imejibu hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom