Jinsi Rais Magufuli anavyowakandamiza wanyonge

Mkuu usiwe mvivu wa kusoma . Upandishwaji vyeo umesitishwa kwa muda maalum kwa kazi maalum ya kuhakiki orodha ya wafanyakazi wote. Usiwe mpotoshaji wa hoja. Too little knowledge is dangerous!
hvi umesoma uzi kweli au unakurupuka tu kujibu bila kuelewa jambo linaloongelewa hapa? hivi, kwa mfano Dr Makufuri anapozuia watumishi wasipandishwe vyeo wala kulipwa fedha za likizo unaona yuko sawa? labda twende na hoja moja moja ndipo utanielewa.
 
Mkuu usiwe mvivu wa kusoma . Upandishwaji vyeo umesitishwa kwa muda maalum kwa kazi maalum ya kuhakiki orodha ya wafanyakazi wote. Usiwe mpotoshaji wa hoja. Too little knowledge is dangerous!
wewe unaona hiyo miezi 2 haina athari kwa watumishi wa umma? hv wafanyakazi wanaoajiriwa na wafanyakazi hewa wanahusianaje? una upeo mdogo sana wa kuelewa na kuchambua mambo.
 
Ndio mafisadi wamewatuma muwatete kwa dizaini hii??
Kwamba ati Magufuli akibana mafisadi watakaoumia ni wanyonge???
Kadanganyaneni wenyewe na wanaowatuma.
hivi, kwa mfano, dr makufuri anapopandisha kodi ya miamala ya simu, halafu gharama zote zinahamishiwa kwa mnyonge, ni MAFISADI wanaumia au ni WANYONGE?
 
mkuu, inaonekan wewe hujaelewa malengo ya serikali bado....je, matumizi ya sukari yakipungua familia za wakulima wanaolima utazilisha wewe? unajua madhara ya TUMBAKU ukilinganisha na madhara ya SUKARI? serikali inahamasisha watu walime tumbaku na inatoa ruzuku kwa wakulima kila msimu wa kilimo unapowadia. unasemajw kuhusu hili? je, unataka wakulima wa tumbaku waache kilimo hiki familia zao zife kwa njaa na uchumi wa nchi ushue?

tunarejea kwenye madhara ya sukari....nitajie hata ugonjwa mmoja unaosababishwa na matumizi sukari. ukiutaja ugonjwa huo, nakupa zawadi sasa hivi.

Hizo Point zako sija kupata na sidhani kama kuna mtu anaekuelewa kwa sisi tuliokaa hapa. Hizo familia unazo sema za kuwalisha unamaanisha hao wanao lima miwa?
Kwani hata leo si wana lima na sukari bado haipatikani? na bado hiyo miwa haitoshelezi mahitaji ya viwanda. Na suali lingine ukiagiza sukari nje inamaana hawa wakulima watapeleka kuuza hiyo sukari huko ngombo? Wacha basi tuagize na tujaze sukari ya nje halafu wewe uwalishe hizo familia kama unaona wao watapungukiwa.
Na suala la afya kwa ajili ya sukari. Sukari inahitajika mwili lakini kwa kiasi, Ukizidisha hicho kiasindio utapata madhara. Watu wengi wanatumia sukari kwenye chai, kahawa au uji na inatakiwa kiwango kidogo tu lakini ililadha ikolee ndipo watu wanapo zidisha kile kiwango cha sukari. Madhara ya sukari ni kudhofisha kinga ya mwili na metabolic dysfunction, kudhofisha viongo,kuharibu Ngozi na kusababisha unene ambao huo unene utakuletea madhara mengineo kama type 2 diabet, ugonjwa wa moyo n.k. Kuna madhara mengi sana, mmoja huzalisha lingine.
Sasa nataka wewe unifahamishe lengo la serikali ni nini kuzuia sukari ya nje? Labda unaweza ukanfahamisha, ni vizuri kujua badala ya kupinga tu.
 
na wale wenye viwanda wanaotegemea sukari kwa ajili ya matumizi mbalimbali wakisimamisha uzalishaji na kupunguza wafanyakazi familia za wafanyakazi watakaopunguzwa utazitunza wewe?
Mimi nilikuwa na bakery ya kutengeneza keki, ila kwa sasa nimefunga rasmi
 
wewe unaona hiyo miezi 2 haina athari kwa watumishi wa umma? hv wafanyakazi wanaoajiriwa na wafanyakazi hewa wanahusianaje? una upeo mdogo sana wa kuelewa na kuchambua mambo.
Mkuu, naona ni mzito wa kuelewa. Kila pambano lina maumivu. Unapoenda vitani hata ukishinda hasara lazima upate. Kwa hiyo, ili kuweka vizuri masuala ya watumishi lazima hayo unayosema yawepo. Ni maumivu lkn mfumo bora wa ufuatiliaji wa utumishi serikalini utapatikana! Wake up!
 
hivi, kwa mfano, dr makufuri anapopandisha kodi ya miamala ya simu, halafu gharama zote zinahamishiwa kwa mnyonge, ni MAFISADI wanaumia au ni WANYONGE?
kuna watu sijui wamelishwa nini,maamuzi mengi yanamuumiza maskini lakini wamekazana tu,mfano mdogo tu wa sukari mpaka leo maumivu,inakuja ishu ya mitumba hawashtuki
 
Mnaodhani kuwa Dr Magufuli ni mtetezi wa wanyonge (kama anvyojinukuuu mara kwa mara) mnapaswa kutafakari upya. Tangu Dr Magufuli alipoingia madarakani amefanikiwa kukanyaga haki mbalimbali za raia pamoja na kufanya maisha ya mamilioni ya watanzania wa kawaida yawe magumu zaidi kuliko ilivyokuwa katika utawala wa Dr JK.

Kuna baadhi ya maamuzi ya kikandamizaji ninayoweza kuyakumbuka ambayo madhara yake yamewaumiza wananchi huku wanafiki na wachochezi wachache wakichekelea wakati wanajua haki za msingi za wananchi zimekanyagwa:

KUINGILIA MFUMO WA BIASHARA HURIA

Ni dhahiri mfumo wa uchumi wa sasa ni wa BIASHARA HURIA – kwamba upatikanaji wa bidhaa (supply) na na mahitaji (demand) ndio huamua bei (price). Kazi ya serikali sio kufanya biashara ila kazi yake ni kurahisisha mazingira ya biashara na kukusanya kodi.

Lakini tumeshuhudia Dr Magufuli akizuia uagizaji wa sukari (intentional supply disruption) na kusababisha upungufu mkubwa wa sukari ambayo sasa huuzwa kati ya Tsh 6000 kwa kilo badala ya bei ya Tsh 1200 ya awali. Kwa lugha nyepesi naweza kusema uamuzi huu umekuza ugumu wa maisha ya wanyonge kwa 400% . Tazama sasa jinsi maamuzi ya mtu mmoja yanavyoweza kuathiri maisha ya mamilioni ya watanzania.

KODI YA MITUMBA, NYUMBA ZA KUPANGA, ATM NA MIAMALA YA SIMU

Kodi hizi zimelenga kuwaumiza wanyonge moja kwa moja. Viwanda vya nguo vya hapa ndani havijatosheleza mahitaji ya nguo kwa watanzania wote. Aidha, viwanda hivi bado havijawa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za nguo na imara kama za mitumba. Wananchi sio wajinga hadi wang’ang’anie kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Ni kwa sababu hakuna nguo mbadala zilizo maridadi na imara kama mitumba ndio maana wanaona ni afadhali waendelee kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Viatu vya mitumba vimekuwa ni mkombozi wa wanyonge kwa muda mrefu. Sasa inabidi wananchi tujiandae kuvaa YEBOYEBO nyeupe na njano zinazotengenezwa na makanjibai wa hapa nchini.

Utozaji wa kodi kwa wenye nyumba za kupanga ni msumali mwingine wa moto kwenye kidonda cha wanyonge. Asilimia 99% ya watanzania wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Kodi hii itawaumiza watanzania wanyonge na ambao hawana uwezo wa kujenga nyumba zao za kuishi kwa sababu ya ugumu wa maisha unaowakabili. Tutarajie baba wenye nyumba kupandisha kodi za pango maradufu. Hivyo, wapangaji wengi watashindwa kumudu kodi za pango na kuishi chini ya miti huku wengine wakikimbilia mapangoni kujihifadhi. Naona kasi ya watanzania kuanza kuishi mapangoni kama ilivyokuwa zama za kwanza za mawe imewadia. Tunatolewa kwenye maisha ya utu na kurudishwa kwenye maisha ya kinyama!

Kana kwamba hili halitoshi, bado mwananchi huyo huyo amebebeshwa zigo la kodi ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na kupitia ATM. Makampuni ya simu yote nchini Tanzania yameongeza gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na tayari marekebisho hayo yameishasambazwa kwa mawakala wote. Nimebahatika kuona nakala hiyo ila nilishindwa kuipiga picha na kuiattach humu kwa sababu simu yangu feki imefungiwa na TCRA.

Naomba mdau yeyote atakayeipata nakala hiyo aipige picha na kuitupia humu ili kila mtanzania aangalie maumvivu atakayopata. Na bado.....mabenki nayo yataongeza gharama za kuchukua fedha na kuangalia salio very soon....stay tuned.....tuko pamoja katika maumivu haya hadi mwisho wa dahari!

Tutarajie ukabaji na uporaji wa fedha majumbani kuongezeka kwa kuwa sasa wananchi wataamua kutunzia fedha zao kwenye michago na vibubu nyumbani badala ya kuzihifahi benki au kwenye simu.

KUVUNJA SHERIA YA KAZI

Kwa kisingizio cha kusaka wafanyakazi hewa, serikali ya Dr Magufuli imesema haitaongeza mishahara ya watumishi, imezuia upandaji wa vyeo na uhamisho wa watumishi kutoka kitengo kimoja hadi kingine (recategorization) au kutoka mwajili mmoja hadi mwajiri mwingine ambako atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa. Aidha, serikali imezuia ulipaji wa nauli kwa watumishi wanaoenda likizo au wanaostaafu. Kwa maana hiyo ni kwamba serikali imeaumua kuendesha nchi bila kuzingatia sheria za ajira. Hii ni hali ya hatari sana.

WAFANYAKAZI HEWA

Serikali imeanza kuwakamata baadhi ya watumishi wanaosadikiwa kuwa “wafanyakazi hewa” na kuwalazimisha kulipa fedha zilizongizwa (na mafisadi) kwenye akaunti zao. Inakuwaje mtumishi amestaafu lakini bado SERIKALI inaingiza fedha kwenye akaunti yake halafu leo serikali hiyo hiyo inakuja kumkamata na kumfungulia mashtaka? Na kibaya zaidi kuna baadhi ya watumishi ambao fedha zimeingizwa kwenye akaunti zao na kuchukuliwa na mafisadi walioziingiza pasipo mwenye akaunti kujua. Kwanini hao mafisadi waliongiza fedha kwenye akaunti hizo wasichuliwe hatua badala yake wananchi wanyonge wasiokuwa na hatia ndio wananyanyaswa? Na je, mbona hatujasikia wale mabingwa wa kuchomekea wafanyakazi hewa wakikamatwa mpaka leo hii wakati wameitia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi? Kwanini wahusika wanaachwa lakini wasiohusika wanaandamwa kila kukicha?


UKOSEFU WA FEDHA MTAANI

Kufuatia “ubanaji wa matumizi” unaofanywa na serikali ya Magufuli, mzunguko wa fedha umepungua sana hapa mtaani na kupelekea mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu kwa wananchi. Ukosefu huu wa fedha umeongeza ughali wa maisha kwa wanyonge, hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha. Wananchi wamekata tama kabisa ya maisha na wanajuta kuzaliwa katika nchi hii ya Tanganyika.
Ingekuwa vizuri ukaonesha hizo sheria zinazovunjwa.
 
Mkuu, naona ni mzito wa kuelewa. Kila pambano lina maumivu. Unapoenda vitani hata ukishinda hasara lazima upate. Kwa hiyo, ili kuweka vizuri masuala ya watumishi lazima hayo unayosema yawepo. Ni maumivu lkn mfumo bora wa ufuatiliaji wa utumishi serikalini utapatikana! Wake up!
bado hujajibu swali.....KUZUIA WATUMISHI HALALI WA UMMA KUPANDA VYEO KUNA UHUSIANO GANI NA WATUMISHI HEWA?
 
Hizo stastics umetoa source wapi?

Simu fake maana yake hazina ubora na inabidi kuondoshwa. Hamna jema hakuna jema litakalo fanyika kwenye nchi hii..? Kasi ya Kansa ya ubongo imeongezeka barani Ulimwenguni kutokana na matumizi ya simu zisizo na ubora. Kama ww kiongozi wa nchi hii utaacha Wananchi wako ndani ya miaka ishirin wafe kwa tamaa za watu wachache??

Kama hiyo hautoshi kila kilicho fake na vitoke kabisaaa kwenye biashara hiyo unayoiita huria. Kuanzia vipuri vya magari mpk viongozi vya akina mama.

We kama mfanyabiashara Na mzalendo lipa kodi yako.. Tatizo lipo wapi?

Ukosefu wa fedha mtaani.. Maana ulikuwa ukiamka asubuhi unaenda mtaa wa tatu unaziokota. FANYA KAZI!

Wafanyakazi hewa.. Seriously?? Tunawatumishi wangap serikalini mbona hawajakamatwa? Mbinu za kihuni zinazofanywa na baadhi ya Wafanyakazi wasio waaminifu kuiibia serikali LAZIMA WACHUKULIWE HATUA za kisheria.

Mi sidhani kama tunaelewana kwenye hilo.. Naona umedhamiria kupotosha umma wa watanzania.

Asante kwa kuleta mada. Ila kwa upande wangu, mi nafikiri SIASA muda wake umeisha.. Tupige kazi!! Tumezoea mteremko kwenye kila jambo. Naomba kuwasilisha.
Huyu tpaul ni wa kupuuza.
 
Back
Top Bottom