Jinsi Rais Magufuli anavyowakandamiza wanyonge

Tujifunze kulipa kodi. Watu walipe kodi.
Huna unachojua kuhusu hiyo asilimia 4 kwa sasa ya kwenye madini ni nini. Tamko limekwisha toka la kuangalia migodi inayotangaza hasara.
TAMKO LA MIGODI ITAKAYOTANGAZA HASARA kumbe ndio maana ya ASILIMIA 4?
 
Funga gidamu tu mkuu kama sio wewe ni watoto au wajukuu zako ndio watafaididika hapo baadae, mbona unakuwa mbinafsi unataka wewe tu vizazi vijavyo je, acha hizo, kwenye nyumba usiwe na wasiwasi itatungwa sheria ya kusimamia yote hayo hivyo pango halitapanda la kuumiza wanyonge wenzie na Rais Mh JPM, vuta subra.
mkuu, hiyo sheria itakayotungwa kuwalinda wanyonge ni kama hii iliyotungwa kuwalinda watumiaji wa MPESA?
upload_2016-6-23_18-40-30.jpeg
 
Hizo stastics umetoa source wapi?

Simu fake maana yake hazina ubora na inabidi kuondoshwa. Hamna jema hakuna jema litakalo fanyika kwenye nchi hii..? Kasi ya Kansa ya ubongo imeongezeka barani Ulimwenguni kutokana na matumizi ya simu zisizo na ubora. Kama ww kiongozi wa nchi hii utaacha Wananchi wako ndani ya miaka ishirin wafe kwa tamaa za watu wachache??

Naomba kuwasilisha.

Simu fake - serikari iliwanufaisha watengeneza simu "real". Mwananchi wa kawaida amechapwa na amebebeshwa adhabu kumnufaisha bwana simu "real".
Sijui itafika siku tuambiwe magari fake, pikipiki fake nakadhalika vinakusanywa vikatiwe moto? Mbona tuna vyeti, stashahada na shahada fake, na wanye hizo wanaendelea kutuongoza?
 
Habari njema ni kwamba hata Mh Rais kaliona hili la kuwa kuna watu wana mkakati wa kumchelewesha ili asitimize yale yeye na chama chake waliyoya ahidi kuyatekeleza ndani ya miaka mitano. Hata humu jF ukisoma kuna wapotoshaji wanaendeleza huo mkakati. Na amini watadhibitiwa ni suala la muda tu.

Hata hao wa tumishi hewa wakichomekwa si wanalipwa na kujaza nafasi ambazo zingechukuliwa na wanaozunguka na vyeti mitaani.
mkuu, hujaelewa hoja yangu.....mbona wale MAFISADI papa waliochomekea WAFANYAKAZI HEWA hawaguswi?
 
Unajua hata mja mzito ikifika wakati wa kujifungua ndiyo uchungu una zidi. ..lakini mtoto akisha toka ni furaha ya ajabu. ...haya mateso yatapita tu...utakuja kaniambia. ...ubarikiwe sana Kwa hekima na busara
mkuu, mifano unayoitoa haisadifu hoja tunayoijadili hapa.
 
Nimejibu kwa hasira au nimebainisha upotoshaji uliofanywa kwa makusudi. And the good news is, Rais kesha liona hili, ya kuwa mna mikakati maalumu ya kumfungisha breki ashindwe kutimiza ahadi zake na kasema hata kubali, so mjiandae tu.

Na for your information kuchangia hapa jF hakuhitaji upitie stages kama za kukua kwa mtoto. Ila ni hekima na akili yako kama ulivyo jaliwa na Mungu wako. So utukufu na heshima zina Mungu mwenyewe.
mkuu, haikubaliki kutetea haki za WANYONGE kwa kuwakandamiza WANYONGE. umeelewa sasa?
 
mkuu

mkuu, kama hujui kusoma basi tazama picha hii hapa......hii ni mojawapo ya hoja niliyoiongelea....kwamba kuongezwa kodi ya ATM na kutuma pesa kwa simu, gharama zote zitahamishiwa kwa WANYONGE:

Sasa mlitegemee kupata maendeleo bila ya kodi?
 
Utawajua je wafanyakazi hewa bila kuwajua walio wachomeka?
swadakta! naona sasa somo limeeleweka, hawa ndio niliokuwa nahoji kwa nini hawaguswi...WACHOMEKWAJI wanabanwa wakati WACHOMEKAJI hawaguswi! sasa tumeenda sawa. sasa tujiulize...MBONA HAWA HAWAGUSWI? KUNA NINI HAPA?
 
Nitakuelewa vipi wewe mpotoshaji? Huwezi kunipotosha utawapata hao walio wajinga tu.
mkuu, kama hujui kusoma basi tazama picha hii hapa......hii ni mojawapo ya hoja niliyoiongelea....kwamba kuongezwa kodi ya ATM na kutuma pesa kwa simu, gharama zote zitahamishiwa kwa WANYONGE:
 

Attachments

  • upload_2016-6-23_19-50-56.jpeg
    upload_2016-6-23_19-50-56.jpeg
    24.6 KB · Views: 22
Mnaodhani kuwa Dr Magufuli ni mtetezi wa wanyonge (kama anvyojinukuuu mara kwa mara) mnapaswa kutafakari upya. Tangu Dr Magufuli alipoingia madarakani amefanikiwa kukanyaga haki mbalimbali za raia pamoja na kufanya maisha ya mamilioni ya watanzania wa kawaida yawe magumu zaidi kuliko ilivyokuwa katika utawala wa Dr JK.

Kuna baadhi ya maamuzi ya kikandamizaji ninayoweza kuyakumbuka ambayo madhara yake yamewaumiza wananchi huku wanafiki na wachochezi wachache wakichekelea wakati wanajua haki za msingi za wananchi zimekanyagwa:

KUINGILIA MFUMO WA BIASHARA HURIA

Ni dhahiri mfumo wa uchumi wa sasa ni wa BIASHARA HURIA – kwamba upatikanaji wa bidhaa (supply) na na mahitaji (demand) ndio huamua bei (price). Kazi ya serikali sio kufanya biashara ila kazi yake ni kurahisisha mazingira ya biashara na kukusanya kodi.

Lakini tumeshuhudia Dr Magufuli akizuia uagizaji wa sukari (intentional supply disruption) na kusababisha upungufu mkubwa wa sukari ambayo sasa huuzwa kati ya Tsh 6000 kwa kilo badala ya bei ya Tsh 1200 ya awali. Kwa lugha nyepesi naweza kusema uamuzi huu umekuza ugumu wa maisha ya wanyonge kwa 400% . Tazama sasa jinsi maamuzi ya mtu mmoja yanavyoweza kuathiri maisha ya mamilioni ya watanzania.

KODI YA MITUMBA, NYUMBA ZA KUPANGA, ATM NA MIAMALA YA SIMU

Kodi hizi zimelenga kuwaumiza wanyonge moja kwa moja. Viwanda vya nguo vya hapa ndani havijatosheleza mahitaji ya nguo kwa watanzania wote. Aidha, viwanda hivi bado havijawa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za nguo na imara kama za mitumba. Wananchi sio wajinga hadi wang’ang’anie kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Ni kwa sababu hakuna nguo mbadala zilizo maridadi na imara kama mitumba ndio maana wanaona ni afadhali waendelee kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Viatu vya mitumba vimekuwa ni mkombozi wa wanyonge kwa muda mrefu. Sasa inabidi wananchi tujiandae kuvaa YEBOYEBO nyeupe na njano zinazotengenezwa na makanjibai wa hapa nchini.

Utozaji wa kodi kwa wenye nyumba za kupanga ni msumali mwingine wa moto kwenye kidonda cha wanyonge. Asilimia 99% ya watanzania wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Kodi hii itawaumiza watanzania wanyonge na ambao hawana uwezo wa kujenga nyumba zao za kuishi kwa sababu ya ugumu wa maisha unaowakabili. Tutarajie baba wenye nyumba kupandisha kodi za pango maradufu. Hivyo, wapangaji wengi watashindwa kumudu kodi za pango na kuishi chini ya miti huku wengine wakikimbilia mapangoni kujihifadhi. Naona kasi ya watanzania kuanza kuishi mapangoni kama ilivyokuwa zama za kwanza za mawe imewadia. Tunatolewa kwenye maisha ya utu na kurudishwa kwenye maisha ya kinyama!

Kana kwamba hili halitoshi, bado mwananchi huyo huyo amebebeshwa zigo la kodi ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na kupitia ATM. Makampuni ya simu yote nchini Tanzania yameongeza gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na tayari marekebisho hayo yameishasambazwa kwa mawakala wote. Nimebahatika kuona nakala hiyo ila nilishindwa kuipiga picha na kuiattach humu kwa sababu simu yangu feki imefungiwa na TCRA.

Naomba mdau yeyote atakayeipata nakala hiyo aipige picha na kuitupia humu ili kila mtanzania aangalie maumvivu atakayopata. Na bado.....mabenki nayo yataongeza gharama za kuchukua fedha na kuangalia salio very soon....stay tuned.....tuko pamoja katika maumivu haya hadi mwisho wa dahari!

Tutarajie ukabaji na uporaji wa fedha majumbani kuongezeka kwa kuwa sasa wananchi wataamua kutunzia fedha zao kwenye michago na vibubu nyumbani badala ya kuzihifahi benki au kwenye simu.

KUVUNJA SHERIA YA KAZI

Kwa kisingizio cha kusaka wafanyakazi hewa, serikali ya Dr Magufuli imesema haitaongeza mishahara ya watumishi, imezuia upandaji wa vyeo na uhamisho wa watumishi kutoka kitengo kimoja hadi kingine (recategorization) au kutoka mwajili mmoja hadi mwajiri mwingine ambako atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa. Aidha, serikali imezuia ulipaji wa nauli kwa watumishi wanaoenda likizo au wanaostaafu. Kwa maana hiyo ni kwamba serikali imeaumua kuendesha nchi bila kuzingatia sheria za ajira. Hii ni hali ya hatari sana.

WAFANYAKAZI HEWA

Serikali imeanza kuwakamata baadhi ya watumishi wanaosadikiwa kuwa “wafanyakazi hewa” na kuwalazimisha kulipa fedha zilizongizwa (na mafisadi) kwenye akaunti zao. Inakuwaje mtumishi amestaafu lakini bado SERIKALI inaingiza fedha kwenye akaunti yake halafu leo serikali hiyo hiyo inakuja kumkamata na kumfungulia mashtaka? Na kibaya zaidi kuna baadhi ya watumishi ambao fedha zimeingizwa kwenye akaunti zao na kuchukuliwa na mafisadi walioziingiza pasipo mwenye akaunti kujua. Kwanini hao mafisadi waliongiza fedha kwenye akaunti hizo wasichuliwe hatua badala yake wananchi wanyonge wasiokuwa na hatia ndio wananyanyaswa? Na je, mbona hatujasikia wale mabingwa wa kuchomekea wafanyakazi hewa wakikamatwa mpaka leo hii wakati wameitia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi? Kwanini wahusika wanaachwa lakini wasiohusika wanaandamwa kila kukicha?


UKOSEFU WA FEDHA MTAANI

Kufuatia “ubanaji wa matumizi” unaofanywa na serikali ya Magufuli, mzunguko wa fedha umepungua sana hapa mtaani na kupelekea mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu kwa wananchi. Ukosefu huu wa fedha umeongeza ughali wa maisha kwa wanyonge, hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha. Wananchi wamekata tama kabisa ya maisha na wanajuta kuzaliwa katika nchi hii ya Tanganyika.

Uliyoyaongea naamini mweshiwa anayajua ila ameamua kuchukua uamzi aliouchukua...endapo utaonekana unaumiza wananchi, wapiga kura watafanya uamzi wa kutomrudisha kwenye uraisi 2020...nyie wengine ni wanafiki tu mlimpinga asiingie madarakani lakini alikomaa akawin kwa wananchi, leo mnamfundisha kazi....!! nakushauri urudi bungeni ukapambane na tulia
 
Katika hayo yote uloandika nadhani moja tu la kuingilia soko huria ndilo linamashiko, mengine unataka kutunywesha sumu kwa sababu ni mambo mtambuka.
 
Tuwe Na subira sufuria zilizo pikiwa Nyama zinaoshwa ili tupike ubwabwa,changamoto lazima zitokee. Tulikuwa pabaya,TRA kunamtu alikuwa kitengo cha kufanya usajiri wa magari kila Sikh so chini ya milioni tano alikuwa anakusanyia mfukoni make.
 
Someone once said, " If it doesn't hurt, it ain't working". Akajibiwa, "It hurts and it ain't working".
 
Back
Top Bottom