Jinsi Rais anavyookota vitu bandarini

Jinsi Rais anavyookota vitu bandarini

```Naye akawajibu "Msinililie Mimi, jililieni ninyi na kura zenu, kwa maana hakuna aliyewalazimisha mpange foleni siku ile." Basi wakainamisha nyuso zao kwa huzuni, wala wasiweze kumjibu. Naye akiisha kusema hayo akapita katikati yao akaenda zake bandarini``` *_(Watanzania 5:20)_*
Umenifanya nicheke Mkuu
 
Sizonje ana bahati ya kuokota vitu. Wafanyakaz wa bandar hawaoni vitu vya kuokota lkn mheshimiwa akija anaokota tu
 
Naombeni kujua wakuu wa JF

Napata shida sana kujua namna Rais wetu anavyoweza kuokota vitu kama magari,vichwa vya treni nk pale bandarini

Je, anakuwa katika ziara za kawaita tu then katika mizunguko ya hapa na pale ndio anapata kuokota?

Natambua kuwa Rais ana vyanzo na intelijensia kuwa katika maeneo nyeti. Hivyo taarifa humuijia. Lakini najiuliza kwa nini mpaka yeye tu ndio akaokote?

Nini maana ya mgawanyo wa majukumu?Hakuna vyombo vingine vya udhibiti. Kwa nini isiwe Mabosi wa bandari wenyewe,au PCCB na pengine waziri?

Naona kama watendaji wa Rais mnamkumbatisha Rais kila kitu matokeo yake anakuwa busy mpaka anakosa mda wa kuhudhuria misiba mizito. Matokeo yake mamlaka zingine zinadharaulika kwa kuwa hazina nguvu( Kama TCRA inavyodhalaulika na zile Channel 5)

Anyway kufupisha maelezo

Naomba kujua jinsi Rais anavyookota vitu pale bandarini
We unashangaa hilo watu wanaokota mpaka makampuni kana CELTEL, IPP
 
Back
Top Bottom