Jinsi nilivyoanza maisha!!

Jinsi nilivyoanza maisha!!

Kabla sija comment neno, ebu kwanza weka picha ya huo mkebe na banda lako kwanza tuone....[emoji30][emoji30][emoji30]
Aaah! Mkuu! Katika vitu ambavyo sipendi kupost mtandaoni ni nyumba yangu na kagari kangu!!
 
Jambo la kwanza hongera.
Nawafahamu vijana wengi sana walioajiriwa zaidi ya miaka kumi hawajaanza kujenga.

Kila siku wanakwambia mshahara hautoshi. Kwa hiyo hongera. Kaza moyo, safari bado inaendelea.

Jambo la pili,
Fanya ufanyalo, tafuta njia nyingine ya kipato, sijui unashughulika na nini ila biashara siyo bar tu mjini hapa, au siyo lazima utoke kwenye uwanja unaoujua na vile vile siyo lazima uache kazi au itumie muda wako mwingi.

Depending na kazi unayofanya, hicho hicho unacho kifanya kazini unaweza fanya kama consultant nje ya masaa ya kazi.

Mfano, kuna mtandao unaitwa ajiras.com huu ni mtandao wa freelancing. Unaweza jiunga bure kabisa na kupost kazi unayoweza mfanyia mtu na gharama zako.

Unaweza mfanyia mtu kazi on your free time na kupata kipato cha pembeni. Huhitaji mtaji wala ofisi. Fanya kazi popote vyovyote.

Cha kuzingatia ni kuwa na njia nyingine ya kupata kipato maana majukumu haya pungui, bali yanaongezeka.

Najua muda hautoshi na probably unawaza unachoka sana. Fanya mapambano sasa, in two years unaweza kuta una kampuni yako.

All in all, hongera na endelea kupambana. Maisha ndo haya haya.
Dah! Mkuu umetema madini kama yote aisee! Hapa najipanga kuingia kwny agribizness mkuu ndo focus yangu itakuwa huko mpk kustaafu kwangu Mungu akijaalia uhai. Asante sana
 
Mi sijaajiriwa nna miaka 25 ninamiliki kampuni mbili moja ya mavazi nyyingine ya technology

Kampuni zangu zina miaka mwili kwenye market I hope zitaanza kunilipa vyyema baada ya kutengemaa

Nimepanga chumba kimoja well furnished teh teh teh.......

Maisha sio haba

Natamani niajiri watu wengi zaidi kampuni zangu zikikuwa na kutanuka zaidi
Technology hipi mkuu maana I'm interest in tech
 
nilianza.maisha baada ya kufumaniwa na mtoto wa mwenye nyumba.
tuliyokuwa tumepanga na wazazi
wale watu kumbe waislamu wakanifungisha ndoa ya mkeka.
mwenye nyumba alikuwa na chumba k1 na sebule na sisi mshua alipanga chumba na sebule so kulala home ikawa haiwezekani.
hapo mtoto wa watu nishamtia na kamimba ka miezi m3 nikiwa ndiyo kidato cha 6 nimerudi likizo
daah nashukuru Mungu nilipata post ya Jkt nikapiga baada ya kumaliza mafunzo sikutaka kurudi home.nikawa mzururaji kwa wadau niliokutana nao pasipo kuelewa kipi na kwepa
mambo siyo haba nilipopata chuo nikala na 90% heslb
hapo nikaanza kupanga na kumleta .Yule mwanamke ghetto.
mwishowe mpaka namaliza chuo nikajikuta nimejenga pasipo kuelewa nimejengaje.
nika note kuwa unaweza kuwa na mwanamke lakini akawa amebeba NGUVU ya mafanikio yako.
 
Technology hipi mkuu maana I'm interest in tech
Tunadesign na kuunda vifaa vya kielecteonic, electromechanic n. K

Mfano saivi tuna computer mouse zetu, hair drier ndo ipo kwenye hatua za mwisho za design steps

Tuna lists ndefu za bidhaa zetu ambazo Zipo on progress kuna mambo madogo madogo tu yanakwamisha

Pia tunafanya project za building services, waste water treatment design and construction kwa kifupi Hali ndo hiyo mkuu

Karibu sana
 
We acha tu mkuu, kama wewe umeanza maisha ya kujitegemea na una kipato mshukuru Mungu, kuna watu wanapigika kitaa
.....Kumbeee!!??, ila kuanza maisha ni 'dhana' pana kidogo, Mimi nilifikiri kitendo cha wewe kuzaliwa tu inakuwa tayari umeanza maisha

Mathalani naweza kusema kuanza maisha ni kutoka kwa wazazi au walezu kumbe sivyo, Naweza kutoka kwa wazazi ila bado nikawa tegemezi! kwa mantiki hiyo nitakuwa sijaanza maisha!

Unajua watu wanashidwa kutofautisha kati ya Kuanza maisha na Kuanza kujitegemea, Mara nyingi huchanganya mambo, Mtu anapotoka kwa mlezi ama mzazi kwa minajili ya Kujitegemea huyo Tunasema ameanza maisha ya kujitegemea na si vinginevyo!

Kuanza maisha ni mchakato unaohusisha vitu vingi, Kitendo cha mtu kuzaliwa tunasema ameanza maisha yake ya Duniani.
 
Safi sana. Kikubwa kumshukuru Mungu. Japo umenikumbusha mbali sana ila cha ajabu mwisho wa siku inabaki kama hivi yani ni story tu. Niseme tu huwa ni moja kati ya kumbukumbu nzuri sana.
 
Swallamah wakuu,
Maisha ni safari ndefu leo nimetimiza miaka 10 toka nisaini mkataba wa ajira hapa ninapofanya kazi, na cjawahi kujuta kufanyia kazi hapa.
Ngoja niende moja kwa moja kwa point. Basi bana nilipopata mshahara wangu wa kwanza nikanunua godoro(bila kitanda), kajiko ka mchina,sufuria mbili,miko miwili,kisu na vijiko! Nikanunua na "home theatre" yenye thamani ya kitanda cha 6*6,naomba ku"declare interest" hapa, yaani mimi ni mlevi wa muziki(ulevi huu unazidi ule wa papuchi, pombe, madawa, sigara na mengineyo). Nafikiri nisingepata hii kazi ningekuwa mwanamuziki. Namshukuru Mungu ndani ya miaka hii kumi nimeweza kujenga kanyumba kwny skwata japo hakajaisha, nina kausafiri(baby walker ila sio passo) na watoto wanaenda shule na kupishana njia ya msalani kila siku. Maisha ni mapambano ndg zangu nawe endelea kupambana.
Wages yako kwa mwezi bei gani mkuu
 
Tunadesign na kuunda vifaa vya kielecteonic, electromechanic n. K

Mfano saivi tuna computer mouse zetu, hair drier ndo ipo kwenye hatua za mwisho za design steps

Tuna lists ndefu za bidhaa zetu ambazo Zipo on progress kuna mambo madogo madogo tu yanakwamisha

Pia tunafanya project za building services, waste water treatment design and construction kwa kifupi Hali ndo hiyo mkuu

Karibu sana
hongera sana mkuu Naomba utupie picha ya hizo items
 
Back
Top Bottom