Jinsi mapenzi yalivyofanya ufalme wa Egypt/Mizraim kuanguka na kusambaratika

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,675
106,781
Hello...
Previous I wrote a topic centered on Greece and we discussed a bit about Egypt, So this Topic will be serving as a spin-off of that Topic. Will focus on Rise and fall of Egypt , Pharaoh's Dynasty Respectively

Baada ya gharika iliyoikumba dunia wakati wa Noah (Nuhu) watoto wake wakaanza kuzaliana. Ham alimzaa Mizraim (Misr) Misri alihamia eneo la kaskazini mwa afrika (NB. enzi hizo Mabara yalikua hayajagawanyika) kisha akaanza maisha eneo hilo, waliishi pembezoni mwa mto nile wakijishughulisha na kilimo watu wakazaliana na kuongezeka.

Watu walivyoongezeka wakaanzisha Ustaarabu (Civilization) na Tamaduni (Culture) zao wakachaguana viongozi wao kwa wao, Kulikua na misri ya chini (Lower Egypt) na misri ya Juu (Upper Egypt) Ila zote zilikua kitu kimoja. kwenye Lower Egypt ndio kulikua na miji mashuhuli kama Memphis nk. Wamisri walijaliwa akili nyingi sana katika kufikiria, walizitumia bongo zao vizuri sana katika kutatua shida mabalimbali zilizowakabili. Lakini huwezi kutaja maendeleo ya misri bila kuutaja mto Nile, huu mto umebeba dhima kubwa katika Mafanikio ya misri ya kale na ya sasa katika kila nyanja....Mto Nile ndio sababu kuu ya misri kua hivyo ilivyokua kipindi hicho, viongoz wao waliwaita Pharaoh.. waliwaheshimu,kuwaabudu na kuwaogopa kama miungu. maana wamisri waliamini mapharao huongea na Mungu (Mungu mkuu wa Misri huitwa Ra)

Miaka ikapita alizawa jamaa mmoja anaitwa Imhotep, huyu jamaa alikua ana akili sana sana, alikua ni kuhani mkuu/High priest wa Mungu Ra. alikua kabobea zaidi katika uhandisi wa majengo na Matibabu. pyramid nyingi unazoziona kajenga yeye kaandika maandiko mengi sana yanayohusu tiba na uhandisi
Misri ikawa misri katika ubora wake, miaka ikasonga mbele.

Mwaka 356 BC huko Ugiriki akazaliwa Alexander, alipoinukia baba yake akampeleka kwa Aristotle mwanafalsafa nguli wa kipindi hicho amfundishe hekima na matumizi ya akili katika kupanga na kutatua mambo, Alexander akaiva akawa very smart kichwani. baada ya miaka 16 muda wake wa kusoma ukawa umeisha siku moja baba yake (King Philip II) alienda vitani akamuacha Alexander kama ndio mfalme alinde ufalme. Wakati akiwa amebaki yeye kama mfalme kabilaona la
Thracian wakaasi wakataka kuanzisha vita na ufalme, Alexander akakusanya kikosi akawapa kichapo akafanya mjia wao kua Koloni lake na jina la mjia wao likabadirshwa na kua Alexandropolis.

Mengi yalitokea, alianzisha kupanua utawala wake kutoka huko Ulaya akaenda hadi Asia kisha akafika Misri.
Alexander alipanua himaya yake hadi kufika mirsi akawapa kichapo wamisri wakasarenda akachukua nchi. Kitu kimoja alichofanikiwa alexander ni kuheshimu na kufuata mila za sehemu anazotawala. Mfano alivyoichukua misri alitawazwa kua Farao wa Misri akawa aaweka muwakilishi wake halafu anasonga mbele kwenda kutanua himaya. Ila akirudi kwenye moja ya himaya zake anaheshimu mila zao na kuzifuata bila shida ndio maana alikua ana vyeo vingi sana

Enzi hizo Memphis ndio ilikua kitovu cha mirsi kila kitu kizuri kipo hapo kama nilivyoelezea sasa Alexander aliupend mji mmoja unaitwa Rhacotis akaubari jina ukaitwa Alexandria huu ulikua mji maarufu zaidi misri hadi mwaka 641AD walipokuja warabu kuivamia miri na kuufanya mji wa Fustat kua mji mkuu, Fustat ulibadirishwa ukawa unaitwa Cairo.

Sasa hapo Alexandria kulijengwa Maktaba ya kwanza duniani (World First Library) ambapo maarifa kutoka kila pemebe ya dunia yalikusaywa hapo. Alexandria ikawa kitovu cha dunia enzi hizo kama ilivyo NewYork sasa hivi, kila mtu ndoto yake ilikua kufika hapo Alexandria, wanafalsafa wengi na wanasayansi wengi wqliend kusomea hapo Alexandria... Daktar wa Kanisa Lucas ambae aliandika kitu cha Injili ya Luca nae amesomea hapo Alexandria.
Kiufupi Alexandria ilikua kitovu cha elimu duniani hadi wapuuzi wawili walivyokuja wakaharibu kila kitu.

Maisha yakazidi kusonga Alexander akafa 323 Ugiriki ikaanguka ikawa sio tena taifa lenye nguvu wala kutegemewa katika nyanja mbalimbali..Akaibuka mbabe Mrumi (Ufalme wa Rumi/a).

Wajinga wawili , Mapenzi kitovu cha uzembe.
Plotemy I Soter
Baada ya Alexander miaka kadhaa mbele (Mwaka 305BC) Moja kati ya majenerali waliokua nae huko mirsi alibadirisha mfumo wa utawala wa Misri akaibadiri misri kua Ufalme wa Plotemy (Plotemaic Dynasty) Waliweka sheria kua wafalme wanatakiwa kuyunza mila na desturi za nyumbani kwao Ugiriki (Makedonia) ili kutimiza hilo walioana wao kwa wao yaani kaka anamuoa dada au shangazi na ndugu wengine na walikua hawaruhusu kujigunza lugha wala tamaduni za wamisri.
Mwaka 69BC kadada kazuri kalizaliwa huko Alexandria Misri, kadada hako kaliitwa Cleopatra.

Cleopatra alikua anatoka kwenye huo ukoo wa Plotemy ila alikua anapenda kujifunza na kua na watu hivyo yeye ndio akawa wa kwanza kujifunza lugha na tamaduni za kimisri ndio maana wengi hua wqnadhani kua cleopatra alikua mmisri...inasemekana Cleopatra alikua anaongea lugha zaid ya 12 alipiga vitabu ipasavyo maana kalikua hapo Kwenye kitovu cha elimu duniani.

Kama kawaida Land alianation, forced labour, Huge tax, nk vilifanya waafrika tuwaimbize wakoloni basi na wamisri walipigwa Kodi ya kichwa hadi wakachanganyikiwa wakona hapa bila vita mura mambo hayaendi. wakaanza maandamano kumshinikiza Mfalme wa kipindi hicho ambae ni baba yake na Cleopatra atoke madarakani. Mfalme akaona mambo yameharibika akamchukua binti yake akakimbilia Roma, akaomba msaada arudi madarakani. Seneta ya Roma ikakubali kumpatia kiasi kikubwa cha fedha na wanajeshi akarudi misri akawapa kichapo waliochukua kiti cha ufalme akawa Mfalme tayari. Kama kawaida kukopa "sherehe kulipa matanga" mfalme alikosa pesa ikabidi arudise kodi kandamizi kwa wananchi ili alipe fedha za Watu hata hivyo ilishindikana alifanya madudu hapo hadi thamani ya pesa ikashuka kwa kiwango chan SGR.

Mwisho mzee akafa akaacha usia kwamba mtoto wake wa kiume na Myoto wake wa kike ambae ni Cleopatra ndio wawe watawala. Warumi hawakupinga wakaruhusu ila sheria ikawekwa kua pesa ilipwe na watakua wanalipa kiasi fulani cha dhahabu kwa mihula/terms. Sasa mpaka hapo Roma ikawa ina full control ya Misri, kama nilivyosema Cleopatra alipiga vitabu hasa hivyo alikia mjanja sana alikua mzuri kweye diplomasia, Alianza kutumia kila mbinu kuikuomboa nchi yake Misri kutoka kwa Warumi.

Chakwanza alianza kujipendekeza kwa bedui Julio Caesars akamdanganya dangaya Dikteta kashikika wakawa wapenzi mzee baba Kaisari akawa anajilia Mtoto mzuri with Classy Cleopatra. Hadi siku Caesars anachomwa visu na maseneta wake Cleopatra alikuwepo ikulu Roma wengine wanasema nae alishiriki kwenye njama za kumuua Julio Caesar ila uhusiano wao ulileta mtoto wa kiume aitwae Caesarion ambae nae alikuja kuwa mtawala wa Roma (?).

Bado mwanadada aliendelea kutumia uzuri wake kuwapagawisha viongozi wa rumi ili kutafuta jinsi ya kuikomboa nchi yake.

Second Triumvirate.
Baada ya maseneta kumuua Caesar walishindwa kukaa madarakani hivyo basi kiliundwa kikosi cha watu watatu ambao ni Gaius Ocatavian ambae alikua mtotowa Caesar wa kuasiliwa (Adopted), Mark Antony na Marcus Aemilius Lepidus.
Kuweka kumbukumbu sawa Huyu bwana Octavian ndio alikuja kuijiita Caesar Augustus (Kasiari Agusto) ambapo wakati Yesu anazaliwa yeye ndio alikua mtawala wa Yudea kwa kutumia muwakilishi wake ambae ni Gavana akaitisha watu wote waandikishwe yaani sensa ambapo Maria na Mumewe alihudhuria sensa hiyo huko Bethlehem kisha Yesu akazaliwa huko
usimachanganye na Tiberius. Caesar Tiberius Augustus (Kaisari Tiberio) huyu alimfuata Agusto ana alikua mwanae wa ku-Adopt (inaonekana waroma ndio ilikua kazi yao kuasili watoto)

Turudi kwenye mada.... Second Triumvirate
baada ya umoja huo kuundwa waliwashikisha adabu wote waliohusika kumuua Julio Caesar.
Sasa bwana Cleopatra kazama mapenzini na Marcus Antonius (Mark Anthony) yaani walipendana hadi Mark akamuacha mkewe Octavia amabe alikua dada wa Octavian/Agusto.

Mark Anthony akaagizwa aende misri kudai ile kodi ambayo watawala wamisri wanatakiwa wailipe Mark alipofika huko akazama penzini kwa Clepatra. wanakwambia Cleopatra alitumia mwaka mzima kula bata la nguvu (Luxury) na mpenzi wake Mark Anthony huku wakiwaacha wamisri/wananchi kwenye ufukara wa kiwango cha kabisa. Hawakuiahia hapo tu Mapenzi yaliwatuma kwamba ili wawe huru na penzi lao inabidi waivamie Roma waipige na kuichukua waendeleze kula bata la penzi lao.

Kule Roma taarifa zikamfikia Kaisari Agusto yaani aliyetumwa pesa kapewa penzi kanogewa kasahau kurudi lakini hajaishia hapo anapanga mbinu za kuvamia wenzake-Nchi yake kwa shinikizo la mapenzi/penzi la Cleopatra. Kaisari akaona dharau akatuma majeshi yakaenda misri yakagawa kichapo cha nguvu...Yaani Cleopatra na Mark walichapwa hadi wakakimbia wakajifungia ndani wakanywa sumu na kujiua. Octavian/Augusto alifika mwenyewe Alexandria na kuitawala hakuishia hapo kwa hasira alichoma ile Library/maktaba ya kwanza kujengwa duniani akaunguza kila kitu.. Ila hakua mjinga jamaa alibeba maarifa makubwa/Vitabu akahamishia Roma. Alexandria ukawa sio kitovu tena cha maarifa ulimwenguni hapo sasa ndio Rome ikawa kitovu cha maarifa.......ndio maana kwa kutumia tukio hili ndio maana kuliibuka wanafalsafa wengi wengi na watu wenye akili sana hapo Roma akiwemo Leonardo da vinci nadhani wengi mshasoma Renaissance. ambapo ilichagizwa pakubwa na tukio la Augusto kubeba vitu kutoka Alexandria kuja Roma. though hii fact hua wanaikataa wanasema kila kitu kilichomwa moto.

Cleopatra ndio Farao wa mwisho nchini misri...Japo historia inasema baada ya Octavian kuitawala misri anae alifanywa kua Farao

Baada ya Kaisari Constantine kufaya mageuzi makubwa sana kwenye kanisa la Kristo la mwanzo na kufanya kanisa hilo kuhamisha makazi kutoka Yerusalemu hadi Rome kanisa hilo lilichukua kumbukumbu na maarifa yote na kuyahifadhi mpaka leo hi. Jesuits wa Roman Catholic wamehifadhi kila aina ya maarifa kutoka pande zote za ulimwengu na kuzihifadhi Hapo Vatican ambapo ni moja kati ya sehemu ambazo ni haziruhusiwi watu kufika. Hata pope anaenda huko kwa sababu maalumu Labda Pope Francis aaweza kua anaingia Regularly kutokana naye ni mfuasi/member wa Jesuist.

Mapenzi ni matamu ila yasitufanye kusahau majukumu yetu kama hao wapendanao wawili Cleopatra na Mark Anthony.


Panapo majaaliwa I'll be focusing on different deities around the globe, Ares, Valkyrie,Jesus, Samson, Zeus, etc are slatted to appear and reprise their role as God of war, goddes, Masiah, judge respectively.

Mwisho...
Da'Vinci
-excelsior​
 
😁 😅 😅
"watu wenye akili nikiwemo mm mwenyewe..."
I referred Leonardo da Vinci not me mate.. ni moja katinya watu walioibuka kipindi au kabla ya Renaissance. Lakini Vinci ndio kichocheo kikubwa cha Renaissance huko Ulaya. Msinipige mawe bure
 
Tukiachana na kichwa cha mada na hitimisho lake, hii mada ina mambo mengi ndani yake ambayo yanaweza kuzaa mada nyingi sana.
Nimevutiwa na hio ya wajeisuit kumiliki karibu vitabu vya maarifa vyote vya dunia.

Ila hakuwa na wasiwasi na upeo wa maarifa kwa wanazuoni wa kikatoliki, lau kama wangekua na upana wa maarifa au tuseme wangekua na elimu juu wasingingekuwa wanafanya vitu vinavyo onekana vya kijinga kama kuabudu sanamu nk.
 
I referred Leonardo da Vinci not me mate.. ni moja katinya watu walioibuka kipindi au kabla ya Renaissance. Lakini Vinci ndio kichocheo kikubwa cha Renaissance huko Ulaya. Msinipige mawe bure
Nilikupata bingwa, huyo mwamba alikua hatar sana. Unaambiwa alkua na uwezo wa kutumia mikono miwili kwa pamoja kufanya kazi tofauti. Yaan huu unachora mwingine unapakaka rangi
 
Nilikupata bingwa, huyo mwamba alikua hatar sana. Unaambiwa alkua na uwezo wa kutumia mikono miwili kwa pamoja kufanya kazi tofauti. Yaan huu unachora mwingine unapakaka rangi
Kabisa aliweza kufanya hivyo na alikua anaandika kinyume nyume yaani kutoka kulia kwenda kushoto. Kwa lugha za kiitaliano ni ngumu sana kuandika hivyo labda kwa kiarabu ambapo herufi zake zipo muundo huo.
The guy was Pure Polymath
Angalia hapo maneno yalivyogeuzwa, Hakufanya hivyo kwa urembo bali kuziwia watu wasikopi kazi yake.
images (8).jpeg
 
Mbona unasema hivyo, je Wewe Uliwahi kuonja mbususu yake??---- wewe si ndio Da vinci wa zama za Cleopatra ??!!
Jamani Jamani
Mimi niionjee wapi?? Nimezaliwa 1400+ AD. Cleopatra kafa wakati wa enzi za Augusto 30s BC ningempataje mimi?? Katika vumbuzi zangu sikugundua Time Traveling Machine niliacha ideas tu
 
Jamani Jamani
Mimi niionjee wapi?? Nimezaliwa 1400+ AD. Cleopatra kafa wakati wa enzi za Augusto 30s BC ningempataje mimi?? Katika vumbuzi zangu sikugundua Time Traveling Machine niliacha ideas tu


Thus, you don't have moral authority to discredit Cleopatra beauty.
 
Kwahiyo unataka kusema Cleopatra alikua Mwanamke mzuri zaidi duniani kama wanavyosema?


Alikuwa miongoni mwa wanawake wazuri aliyepata kuishi katika zama zake, na ndio maana hata wewe umetuletea hadithi hii kuonyesha jinsi alivyowapagawisha madume kiasi kwamba wakajisahau katika majukumu yao, hiyo ni ishara kwamba licha ya mvuto wake (sexy) lakini pia ni dhahir shahir alikuwa "hot in bed".
 
Alikuwa miongoni mwa wanawake wazuri aliyepata kuishi katika zama zake, na ndio maana hata wewe umetuletea hadithi hii kuonyesha jinsi alivyowapagawisha madume kiasi kwamba wakajisahau katika majukumu yao, hiyo ni ishara kwamba licha ya mvuto wake (sexy) lakini pia ni dhahir shahir alikuwa "hot in bed".
Mimi sio expert sana wa kwenye mahusiano/mapenzi btw naamini walimuona mzuri Kwakua alikua ni kiongozi. Unajua pride ya Mwanaume kua Dorminant na mwanamke kua submissive. Hii ndio iliwafanya wanaume wampende na kumtaka.. trust me kuna me wanamuona samia ni mzuri na wanamtamani ajili ya pride hiyo.
Mada hii sikuileta ajili ya uzuri wake nali ajili ya mapenzi na falme za kipindi cha and their motive behind.
Utamu na ubaya wa mwanamke upo kichwani kwa Mwanaume
 
Alooo Da'Vinci asimwambie mutuu Cleopatra alikuwa mxuri sana watu wanadai alikuwa akioga kwenye maziwa ya ngamia.

Hiyo library ya Roma ni hatari na nusu humo ndo kuna vile vitabu vingine vya biblia vilivyo pigwa ban, na baraza moja wslilokaa waroma. Unakuta mkristo tofauti na mromani anadhani anajua Bible kuliko Waroma! Heheeee... Yaani watu waliochagua hiki kiende uraiani hiki kisiende.

Kuhusu mafarao kwanza kulikuwa na farao wa juu na wa kusini lkini kuna farao mmoja aliungsnisha utawala na akawa anavaa kofia mbili kuonyesha msisitizo kuwa yeye wa juu na kusini. Huwa sipati picha endapo wamisri wangekuja hadi Victoria tungekuwa mbali sana.
 
Kuhusu mafarao kwanza kulikuwa na farao wa juu na wa kusini lkini kuna farao mmoja aliungsnisha utawala na akawa anavaa kofia mbili kuonyesha msisitizo kuwa yeye wa juu na kusini. Huwa sipati picha endapo wamisri wangekuja hadi Victoria tungekuwa mbali sana.
Ile kofia iliitwa Double Crown Iliunganisha kofia nyeupe ya Upper Egypt na nyekundu ya lower Egypt. Ila mimi kofia ninayoipenda ni ile inayoitwa Nemes ipo poa halafu inaswagger kama msemavyo vijana.
Wamisri ilitakiwa watuabudu maana sisi (Ziwa victoria) ndio chanzo cha. maendeleo yao.
Lakini Wakazi wa mwanza mbona wananuka umaskini??😄
images (9).jpeg
 
Wamisri ilitakiwa watuabudu maana sisi
Kabisa ilibidi iwe hivyo lakini walichokuwa wakifanya achaa tuuu, this world is full of comedy. Kwa sababu maji ya mto nile yalikuwa yanajaa na kupungua hili jambo liliwashangaza sana wamisri hawakuweza kupata majibu sahii kinini linapelekea maji kujaa na kupungua. Wamisri kama tamaduni nyingine ilibidi faster waje n majibu na jibu lao lilikuwa ni mungu wao anayafungua maji anajaza na uhai. Hivyo basi kwa kuwa walijua bao / sprem ina uhai farao ilibidi kila mwaka kwenda kupiga puchu/punyeto na kumwaga shahawa zake kwenye maji hii ni kama ishara nae kama mungu anajazia uhai.

Kumbe mvua zinazonyesha rwanda n kagera ndio zinapelekea ziwa Victoria kujazwa maji in turn maji yanadukumiwa Nile
 
Kabisa ilibidi iwe hivyo lakini walichokuwa wakifanya achaa tuuu, this world is full of comedy. Kwa sababu maji ya mto nile yalikuwa yanajaa na kupungua hili jambo liliwashangaza sana wamisri hawakuweza kupata majibu sahii kinini linapelekea maji kujaa na kupungua. Wamisri kama tamaduni nyingine ilibidi faster waje n majibu na jibu lao lilikuwa ni mungu wao anayafungua maji anajaza na uhai. Hivyo basi kwa kuwa walijua bao / sprem ina uhai farao ilibidi kila mwaka kwenda kupiga puchu/punyeto na kumwaga shahawa zake kwenye maji hii ni kama ishara nae kama mungu anajazia uhai.

Kumbe mvua zinazonyesha rwanda n kagera ndio zinapelekea ziwa Victoria kujazwa maji in turn maji yanadukumiwa Nile
Aisee umenijuza kitu kipya😄
Sijawahi kujua hili kabisa daah, ila mafarao walikua wanaituko sana. Hasa ukihusianisha na miungu yao sikutaka kugusia miungu maana niaingemaliza. Ila hawa majamaa walikua wanaujinga fulani wa hovyo kama huo.
Walishindwa kujua chanzo cha uhai wao nile kipo bongo haku kwa bhagosha mpaka wapelelezi wa kikoloni walivyokuja kugundua na kubadiri jina
 
Mimi sio expert sana wa kwenye mahusiano/mapenzi btw naamini walimuona mzuri Kwakua alikua ni kiongozi. Unajua pride ya Mwanaume kua Dorminant na mwanamke kua submissive. Hii ndio iliwafanya wanaume wampende na kumtaka.. trust me kuna me wanamuona samia ni mzuri na wanamtamani ajili ya pride hiyo.
Mada hii sikuileta ajili ya uzuri wake nali ajili ya mapenzi na falme za kipindi cha and their motive behind.
Utamu na ubaya wa mwanamke upo kichwani kwa Mwanaume


Ni kweli uzuri wa mwanamke upo machoni pa muonaji, lakini huwezi kupinga kwamba kuna wanawake wenye mvuto kiasi kwamba hata wanawake wenzao wanawahusudu.
Kwa maana hiyo huyo Cleopatra alikuwa ni miongoni Mwanamke wa aina hiyo ya mvuto na added advantage yake ikawa ni kuwepo kwake madarakani na akawa public figure na ndio maana historia leo imemuandika na tunamsoma, narudia kusema huyo alikuwa ni mrembo mwenye madaraka katika zama zake na hii haina maana kwamba hawakuwepo warembo wengine kama yeye au kumpita yeye katika zama hizo.
 
Back
Top Bottom