Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Inaendelea

Khumbu alinipeleka nilikofikia kuchukua vitu vyangu kisha akanipeleka stand kuangalia usafiri wa kunirudisha Bloemfontein. Katika mizunguko yote hiyo niliweza kunotice kuwa Khumbu bado alikuwa ananipenda ila ni kama alikuwa na commitment flani hivi zinanamfanya kuwa na wakati mgumu kunisikiliza kila ninachomwambia, maana kuna kipindi alikuwa kama anazama kwenye lindi la mawazo hivi, halafu nikiwa namweleza ni jinsi gani anayafanya maisha yangu kuwa magumu kimahusiano nilikuwa namuona kama mtu anayejutia hivi. Kulikuwa na zile moments ukimya unatawala halafu mkija kuangaliana unaona kama kila mtu machozi yanamlengalenga. Aliponifikisha stand, nikashuka na yeye akashuka, tukaagana kwa kukumbatiana, sikuweza kuongea chochote maana kitendo cha kumkumbatia na kuushika mwili wake kilinifanya niingiwe na huzuni sana, nilimsikia tu akitamka maneno mawili “I’m sorry” na akaanza kujitoa mikononi mwangu, nilikuwa nimemkumbatia kuzungusha mikono yangu kiunoni kwake mpaka ikakutana, kwa hiyo akawa anaishika kwa kuiachanisha ili niweze kumuachia. Baada ya kujitoa mikononi mwangu akaingia garini akaondoka. Niliendelea kusimama pale nikimwangalia mpaka alipojichanganya kwenye magari mengine ndio nikaondoka hilo eneo.

Njiani nikiwa kwenye basi nilianza kufikiria vitu vingi sana vya kimaisha. Mojawapo nilianza kufikiria je nieendelee kuishi Bloemfontein nijenge maisha na huyu mwanamke wa Bloemfontein? Je nirudi Durban nikatafute kazi huko ili niweze kuwa karibu na Khumbu? Je nirudi Tanzania nikamthaminishe Amina na yule demu wa Sinza kisha atakayelipa zaidi nije naye South Africa? Baada ya hii graduation je niendelee kuishi South Africa yaani nijichanganye kabisa hapa niachane na mawazo ya kurudi Tanzania yaani hapa Sauzi yawe ndio maisha yangu permanent? Je nirudi Tanzania nikatafute kazi, nikaishi tu nyumbani huenda nikaishi kwa furaha zaidi? Maswali yalikuwa mengi na sikujua lipi niamue.

Baada ya graduation niliendelea na kazi huku nikiwa na huyu mwanamke wa Bloemfontein. Pia niliendelea kuwasiliana na Amina na huyu wa Sinza. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti moja amazing. Kipindi naonana naye alikuwa mzuri sana ila kwa kuwa ilikuwa ishapita miaka mingi nilikuwa na wasiwasi kama bado ni mrembo maana wanawake huwa wanabadirika haraka sana, miaka sita kwa wanawake ni miaka mingi sana. Amina alikuwa ananitumia picha na alionekana bado analipa sana tu ila huyu wa Sinza kila nikimwomba anitumie picha alikuwa anadai nije nimuone mwenyewe kwa macho yangu ila kwa maoni yeke yeye ni mrembo wa haja. Huyu wa Sinza kitendo cha kukataa kunitumia picha kilianza kunitia wasiwasi hivyo nikaamua kutuma mtu kwenda kukutana naye ili anipe feedback. Kuna mdogo wangu alikuwa anasoma chuo flani nikampigia simu nikamwomba akamcheki huyu demu. Nikampa namba ya huyo demu na pia nikampigia simu huyo demu nikamwambia shemeji yako nimemwomba aje akusalimie ili mjuane pia apajue unapoishi ili hata kama kuna shida yoyote iwe rahisi kupatikana kwako. Demu akakubali. Dogo akaenda kumcheki na baada ya kumcheki akanipigia simu kunijulisha matokeo. Dogo akaniambia demu ni wa kawaida sana hana maajabu yoyote. Kama ni wa kula na kusepa fresh ila kama unataka kufanya naye maisha na kwa jinsi ninavyokujua unapenda kula vilivyo bora huyo hajafikia viwango vyako. Hiyo ilikuwa tathimini ya dogo. Dah! nikawa najiuliza labda huyu dogo ana jambo lake tu. Mbona demu alikuwa kifaa hivi enzi hizo, iweje awe mbovu tena? Nikasema huyu dogo anazingua, acha niendelee na mchakato wa kuwa naye karibu huyu demu. After all nishatumia gharama za kupiga simu karibia kila siku hivyo hata kama atakuwa halipi acha angalau nikafidie gharama zangu kwa kumla. Hivyo maisha ya kuendelea kuwasiliana na wote hawa wawili yaliendelea hadi niliporudi Tanzania.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo nilivyozidi kupata moto wa kurudi nyumbani. Picha za Amina na Sauti ya demu wa Sinza zilikuwa zinanipa matumaini mapya ya kimapenzi. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti nzuri hatari, nikiwa naongea naye nilikuwa hadi dushe linasimama. Amina naye hivyo hivyo, picha zilikuwa zinanichangaya sana.

Siku moja usiku mwezi wa 10, 2012 nikakata shauri la kurudi nyumbani. Niliamka usiku wa manane, nikachukua diary yangu nikaandika tarehe ya hiyo siku nikasema hii tarehe ndio tarehe niliyokata shauri na kuamua kurudi Bongo.

Kesho yake asubuhi nilipofika ofisini nikamfuata Boss wa kampuni, ni mmoja wa madirectors, nikamwambia “Leo naacha kazi”. Aliniangalia akiwa kama anashangaa, akasema nirudie tena nilichokisema, nikarudia tena “Leo naacha kazi” nilimuona kama kaduwaa. Alikuwa ana kikombe cha kahawa mkononi akakiweka kwenye mezani kisha akaniuliza vipi unaumwa? Umechanganyikiwa? Nikamjibu siumwi wala sijachanganyikiwa. Nimeamua tu niache kazi, nimeamua kurudi nyumbani. I miss home. Akasema wewe Konda msafi unacheza na maisha. Unarudi Tanzania kufanya nini? Akaanza kunipa ushauri, nakumbuka kuna maneno nayakumbuka mpaka leo aliniambia, alisema “All these achievements I have I never got them in one day I have acquired them in years. If you serve God, God will take care of you” . Akaniomba jioni baada ya kazi nisiondoke ili tupate muda wa kuzungumza zaidi. Jioni baada ya kazi nikaenda ofisini kwake. Jamaa alinishauri mambo mengi sana ya kimaisha. Akawa ananiambia sio jambo la kushangaza kama siku moja ataniona namiliki kampuni yangu hapa South Africa kama nitakuwa na nidhamu ya kazi. Pale kwenye kampuni nilikuwa nadili na suppliers wa materials na payroll. Auditor wa kampuni alikuwa Ernst and Young kwa hiyo queries zote za auditor kuhusu suppliers na payroll nilikuwa nazi-attend. Kila mwisho wa mwezi nilikuwa napelekwa na dereva wa kampuni kwa auditor. Suppliers wakipiga simu kuulizia malipo yao mimi ndio nilikuwa nadili nao au mimi kuwapigia simu kama kuna mzigo una shida au umechelewa kufika. Kuhakikisha materials yamepokelewa na kampuni ilikuwa ni kazi yangu, invoice za suppliers lazima nizihakiki kabla ya malipo. Jamaa akawa ananiambia hatashangaa siku moja akiniona nimeshakuwa Chartered Accountant kama nitavumilia, na akasema ataniunganisha na CAs ili wanipe muongozo jinsi ya kufika hapo. Kiufupi jamaa alianza kunipa elimu ya maisha mpaka nikaghairi maamuzi yangu.

Itaendelea
Tupo Pamoja Mkuu, Ngoja tuendelee na kisa mkasa
 
Mkuu konda msafi,usipo weka picha ya khumbu utakuwa hujatutendea haki kabisa natumai kwa ustaarabu ulionao utatuekea
 
Hiyo ni page ya kwanza na ya pili ya academic records. Mnaweza mkaona performance ilivyobadirika ya mwaka wa kwanza ukilinganisha na miaka iliyofuatia kabla Khumbu hajanichanganya na miaka iliyofuatia baada ya Khumbu kunichanganya. Masomo ya mwaka wa kwanza yameandikwa I, wa pili II na wa tatu III. Na hicho kingine ni ile siku niliyoaindika kwenye diary kuwa narudi Bongo.
fanya urud SA konda msafi
 
Hiyo ni page ya kwanza na ya pili ya academic records. Mnaweza mkaona performance ilivyobadirika ya mwaka wa kwanza ukilinganisha na miaka iliyofuatia kabla Khumbu hajanichanganya na miaka iliyofuatia baada ya Khumbu kunichanganya. Masomo ya mwaka wa kwanza yameandikwa I, wa pili II na wa tatu III. Na hicho kingine ni ile siku niliyoaindika kwenye diary kuwa narudi Bongo.
Mkuu hii signecha mbn Kama Kuna mahali imenikatalia ombi langu la kazi
 
Tunaendelea,

Guess what happened baada ya Khumbu kunikimbia?
Nikiwa nimerukwa na akili baada ya kushuhudia hicho kitendo cha kutokwa nduki na demu mara simu yangu ikaita, kucheki nani ananipigia, namkuta msela wangu wa workshop ndio anapiga. Nikawa najiuliza sijui nipokee au nisipokee, maana kwa muda ule nilitakuwa kutosumbuliwa na chochote.

Akili ilikuwa kama imeduwaa hivi halafu nipo kwenye maumivu makali. Simu ikazidi kuita non stop. Nikaona acha nipokee nijue jamaa anataka kusemaje. Baada ya kupokea akaanza kucheka, nikawa najiuliza huyu anacheka nini? Nikaona kama anazingua bangi tu, jamaa akaacha kucheka akaniambia "vipi wa kusoma umemfanyaje Khumbu? Nikapigwa na butwaa, mambo ya Khumbu ameyajuaje huyu. Jamaa akaendelea kusema Khumbu huyu hapa anasema amekukuta kama umechanganyikiwa hivi? ....

Simu imeisha chaji baadae.

Wakusoma... Jina nakumbka mbali sana hili Nikiwa shule My brothers used to call me, Lina kadharau kwa Mbali hv.
 
Mleta mada ulikuwa teja wa khumbu
Mleta mada khumbu aliutwaa ubongo wako akakuwekea ukawa unaitumia kufikiri ikiwa kama ndio ubongo wako.

Hapa nimefungasha mizigo yangu naelekea kwa madiba, baada ya kusoma uzi wako nimeazimia nihamishie Makazi yangu huko. Pengine na mimi siku moja nitaleta visa nitakavyokutana navyo huko

Nenda Baba.
 
Nashangaa mnaninyoshea kidole kanakwamba mimi ndo nlikuwa namfanya khumbu awe hayupo active sana kwa konda msafi

Seems watu humu ndani mnapenda sana uzinzi si wanawake si wanaume, sasa jamaa akielezea xxx kwenye uzi mnafaidika nini kama sio kuchukua sabuni na kufanya yenu? Kesho mnakuja na nyuzi ati nguvu za kiume zimekata,

Vijana acheni ngono haina faida yoyote ni kujilisha upepo.

Kaa kule mimi ntakutukana Afu ntakula Bann
Sina hasara
 
Hahahaha! Hiyo picha ni ya Khumbu. Picha nimeshawawekea, ambaye haamini kama huyo sio Khumbu anitajie huyo ni nani? Kwa hiyo suala la picha tushamalizana. Bado matukio mawili tu nimalize stori. 1.Siku ya kuagana, 2. Kifo chake.
Dah! Mkuu mimi sijaiona! 😥😥
 
Mkuu hiyo comment ni ya kitambo. Usimtukane jamaa bhana. Nadhani wewe umeanza kuisoma hii stori karibuni. Hizo comments za jamaa ni za muda sana hivyo huna haja ya kugombana naye. In fact jamaa ni mtu poa sana usimtukane.
Mkuu tupia nondo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom