Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Nimekuelewa mkuu, niwie radhi. Na pia naomba kwa leo tuishie hapo maana hata mimi akili imevurugika kidogo, nimekosa amani ya moyo. Tutaendelea kesho panapo majaliwa.
Mkuu unaweza kuiedit iyo episode kuondoa ayo maudhui. Fanya ivyo mkuu
 
Wote mnaofatilia huu mkasa. Naomba niwaombe samahani sana kwa kuongelea mambo ya chumbani. Najisikia vibaya kuwa so explicit. Natamani kuifuta hiyo episod ya chumbani maana najisikia hatia kidogo. Unajua binadamu tuna ile nature flani ya kutambua kama kuna kitu flani umekifanya hakiko sawa kinakufanya ujisikie vibaya. Na huenda humu kuna wasomaji hawajakifurahia hicho kipengele cha mambo ya chumbani, kama wapo naomba wanisamehe na ikiwezekana tunaweza tukawaomba na moderators wakakifuta hicho kipande. Ila kama hakuna mtu aliyekwazika na hicho kipande basi tuendelee na episodi nyingine ingawa mimi binafsi sitaongelea tena mambo ya chumbani. Kwa maana hiyo hata kile kipengele cha 071 zitakielezea tena. By the way hakuna mtu aliyenifata na kuniambia labda hicho kipengele sikutakiwa kukiandika bali ni mimi tu nimejisikia vibaya.
Mkuu hakuna mtoto humu
 
Nimekuelewa mkuu, niwie radhi. Na pia naomba kwa leo tuishie hapo maana hata mimi akili imevurugika kidogo, nimekosa amani ya moyo. Tutaendelea kesho panapo majaliwa.
Mambo ya telagram yameanza tayar na wenzio wanaanzaga hivi hivi Mara bando sina
 
Mkuu kwanza nikupe hongera kwa mtiririko mzuri wa story.
Unajitahidi sana.
Kuhusu hizo explicit events (maudhui ya chumbani) wewe yaandike tu na wala huna sababu ya kumuomba mtu radhi.
Najua you made peace with your mind, kitambo, na haimaanishi kama uliyafanya huko nyuma, hata sasa unayafanya. HAPANA.
Tupo hapa kujifunza kwa mazuri na mabaya kupitia watu, hakuna mtu mkamilifu, atakayeona kutopendezwa na unachokiandika, ni vema akauacha huu uzi na kuelekea kunakomfaa yeye.
Kuna mengi sana ya kujifunza kupitia uzi wako, lakin kuna mtu hapa atakuja kuanza kukandia baadhi ya matukio, jaman we are not Gods, sisi ni binadamu, na hakuna aliekamilika, na ni vema huyo mtu akaanzishe uzi wake huko, nan kamuita aje hapa?

Mkuu endelea kushusha vitu, tuko pamoja na wewe.
 
Nimekuelewa mkuu, niwie radhi. Na pia naomba kwa leo tuishie hapo maana hata mimi akili imevurugika kidogo, nimekosa amani ya moyo. Tutaendelea kesho panapo majaliwa.
Konda na Wewe sasa hueleweki.

Topic inazungumzia mapenz, Mwanzo hadi mwisho. Anayekuja ku soma uzi wa mapenz ategemee nini sasa zaidi ya kukutana na mambo ya mapenzi.

Sasa, ww sijui unakwazika nini hasa? Yaani ishu ya mapenz unataka uzungumzie mpira badala ya mapenzi?

Topic ni ya mapenz, ukizungumzia mapenz unakuwa umemkwaza mtu? Huoni kutokuzungumzia mapenz kwenye mada ya mapenz ndo utakuwa umewakwaza wasomaji?

Halafu, hii forum tena tupo anonymous mtu akiona hii topic inamkwaza si anaenda kusoma uzi za jukwaa la siasa, ama historia? Kwa nn aje akwazike na mapenz kwenye topic ya mapenz?

Ingekuwa topic ya mpira ndo unazungumzia mapenz ndo ungejisikia vibaya labda kidogo!

TULETEE story acha uboya! (Sijakutukana nimekupa live tu kama mwanetu)
 
Inaendelea...

Nikawa naumiza kichwa ni namna gani naweza kumtafuta na kuonana na Khumbu bila Sandile kujua. Pia nikawa najiuliza kumtafuta ni swala jingine na kukubali kuonana na mimi nalo ni swala jingine. Kumbuka mara ya mwisho kuwasiliana naye ni kipindi nilipomtolea matusi mpaka akanitishia kunipeleka mahakamani, na mara ya mwisho kuonana ni pale tulipokutana workshop akiwa kabambiwa na msela. Nikawa hata sielewi cha kufanya.

Kwenye yale maeneo ya kuonyeshea mpira kwa ajili ya public pia kulikuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali kama vile inavyokuwa maonyesho ya sabasaba pale Kilwa road. Kulikuwa na shughuli nyingi tu zinaendelea na watu walikuwa wanajaa hasa. Kabla ya mpira kuanza kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali locally and internationally wanatumbuiza kwa zamu.

Sandile alikuwa anatoka na kwenda kutafuta matukio kwa ajili ya kuripoti kwenye gazeti hivyo muda mwingi alikuwa akitoka toka na kuniacha peke yangu kwenye tent la VIP, haimaanishi kabisa kuwa nilikuwa nabaki peke yangu, si mnajua burudani ya world cup, lazima upate company nyingi tu humo mnaoshabikia timu moja. Nakumbuka ile siku mchezaji wa Ghana alipokosa penalty kwenye robo finali, tent zima tulijikuta tumekuwa kitu kimoja tunaomboleza. Ilikuwa ni majonzi, ninachotaka kusema hapa company ilikuwa ya kutosha hata pale Sandile alipokuwa ameenda kutafuta matukio.

Kuna muda Sandile alitoka kwenda kutafuta matukio nikaona huu ndio muda wa kumtafuta Khumbu. Nikapiga simu akapokea, nikamwambia nipo hapa kwenye hii sehemu wanapoonyesha mpira kwa ajili ya public kama hatojali tuonane. Akasema yeye yupo nyumbani anachekia mpira nyumbani.

Nikamwomba aje huku tuonane. Akasema anakuja ila akasema tukutane huku kwenye shopping mall hivi iliyokuwa pembeni mwa hiyo sehemu tuliyokuwepo. Basi mimi fasta nikachomoka kwenda kwenye hiyo mall. Akanipigia simu kunielekeza upande tutakaokutania. Basi nikawa nimefika sehemu ya tukio nikawa namsubiria. Haijapita muda nikamuona kwa mbali akija akiwa na rafiki yake. Walivyofika Khumbu akanitambulisha kwa rafiki yake kama mimi ni mtu wake.

Khumbu alikuwa amevaa kikaputula cha jean na jezi ya timu ya taifa ya South africa. Alikuwa amependeza hatari. Kile kikaputula kilikuwa kimemkaa vizuri hatari. Tako lilikuwa linaning'inia kama mzinga wa nyuki. Haraka haraka nilinotice Khumbu amebadirika sana kimuonekano, hakuwa Khumbu yule niliyekutana naye kwa mara ya kwanza.

Alikuwa na muonekano mmoja wa matawi wa juu. Unajua mwanamke anayejijua status yake, anayejijua thamani yake kuna namna flani ana behave kuonyesha ni quality. Halafu nikimcheki tu hata ngozi yake unaona kabisa huyu kwa sasa life lake lipo njema. Kichwani alikuwa amebana nywele zake hivyo kumfanya kuonekana ana sura ndefu nyembamba amazing. Basi baada ya utambulisho akapendekeza tuingia ndani ya mall tutafute sehemu tukae tuongee.

Tukaingia ndani, akamwomba rafiki yake atupe privacy ili tuongee mambo yetu. Tuliongea mengi ila kubwa akaniambia kwa sasa kama ninamtaka nifanye mpango wa kumuoa. Akasema haitaji tena mahusiano ya kutiana tu. Akaniambia nitafute pesa, au nisubiri nimalize chuo nipate kazi. Nakumbuka alisema haya maneno. "Babe South african girls need money". Akaniambia akipata nafasi atanitembelea ila nizingatie alichoniambia. Tukaagana, nikarudi zangu kuendelea kuangalia mpira.
very true alichokuambia hahahahaha nakumbuka mbali sana ughaibuni acheni tuu mambo mengi hawa viumbe hata ukutane nao Europe wana behave hivyo watoto wa mzansi
 
Konda na Wewe sasa hueleweki.

Topic inazungumzia mapenz, Mwanzo hadi mwisho. Anayekuja ku soma uzi wa mapenz ategemee nini sasa zaidi ya kukutana na mambo ya mapenzi.

Sasa, ww sijui unakwazika nini hasa? Yaani ishu ya mapenz unataka uzungumzie mpira badala ya mapenzi?

Topic ni ya mapenz, ukizungumzia mapenz unakuwa umemkwaza mtu? Huoni kutokuzungumzia mapenz kwenye mada ya mapenz ndo utakuwa umewakwaza wasomaji?

Halafu, hii forum tena tupo anonymous mtu akiona hii topic inamkwaza si anaenda kusoma uzi za jukwaa la siasa, ama historia? Kwa nn aje akwazike na mapenz kwenye topic ya mapenz?

Ingekuwa topic ya mpira ndo unazungumzia mapenz ndo ungejisikia vibaya labda kidogo!

TULETEE story acha uboya! (Sijakutukana nimekupa live tu kama mwanetu)
Nimekuelewa mwana. Hapo kwenye kuniambia uboya wala usihofu maana hizo ndio zilikuwa lugha zetu huko Dizonga. Kule mnaongea kwa kutukanana na ni sehemu ya mawasiliano. Ukiwa mshamba unaweza ukawa unagombana na watu kila siku kwa kudhani wanakutukana kumbe watu ndio ongea yao. Kipindi niliporudi bongo nikawa naongea na watu kwa mtindo huo, si unajua mazoea yana tabu. Watu wakawa hawanielewi ila nilikuja kubadilika baadae baada ya kutambua sasa nipo bongo na sio Sauzi tena. Stori itaendelea usijali, acha nipate utulivu kwanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom