Jinsi mabenki yanavyonyonya na kuleta umaskini

Jinsi mabenki yanavyonyonya na kuleta umaskini

Hii imekataa kumezeka Mkuu, kuna point yenye mantiki katika hoja yako, ila hujaishape vizuri, halafu huu uzi uhamishiwe jamii intelligence JamiiForums plz
 
Mwandishi kasikia sikia hbr hii kakimbilia kuja kuipost hata yeye mwenyewe haielew. ETI BANKS ZINACHAPA PESA? HALAF HAELEWI KUWA KUANZISHA BANK KUNAHITAJ MTAJI AU UWEKEZAJI. mwandishi hafaham na ndo maana haeleweki. Bank zingekuwa zinachapa pesa basi zisingefilisika. Na pesa zingekuwa nying sana. Haelewi anazungumzia nini.
Niliyegemea
Mwandishi kasikia sikia hbr hii kakimbilia kuja kuipost hata yeye mwenyewe haielew. ETI BANKS ZINACHAPA PESA? HALAF HAELEWI KUWA KUANZISHA BANK KUNAHITAJ MTAJI AU UWEKEZAJI. mwandishi hafaham na ndo maana haeleweki. Bank zingekuwa zinachapa pesa basi zisingefilisika. Na pesa zingekuwa nying sana. Haelewi anazungumzia nini.
Mkuu nimetoa ushahidi wa wazi wa Federal Reserve.Matatizo yetu Watanzania ni kuendelea starehe bila kupenda kujisomea, eventually tunakuwa na very shallow knowledge kuhusu issues.Worse still we think what we are taught in school is correct.Believe me most of it is rubbish. Tumeingizwa mkenge sana.Some of us are just trying to open your eyes,lakini kwa kuwa mnashupaza shingo chapweni.
 
1.Maana tukikwambia ni conspiracy theories umeishia sema watawala wa dunia wananitumia kwa kujua au kutokujua --- kwangu hili ni swala la kiimani zaidi.

2. Umelalamika sana kwa swala la mabenki in general na hakuna mahali katika bango lako la awali ulisema swala la uchapishaji wa fedha ni kwa nchi fulani na uzitaje majina na kuiondoa Tz. Ulichofanya ni kujumuisha, tukahoji ukatuambia wewe huzungumzii mambo haya katika upeo mdogo bali mfumo wa kibenki duniani.

3. Umekuja na vitu unavyo viita reference ambavyo kiuhalisia sio. Unasema nenda kagoogle neno flani, yakija mia nasoma lipi?. Wewe umesoma yote na kuyajengea hoja hapa?. Je ni kwa nini hutoi links za webs kama unavyoombwa?. Kile unacho kuamini wewe unataka sisi ndicho tukiamini, tukikupa links unasema hao hawawezi sema ukweli, hao wewe ulikosoma ambazo sio taasisi husika unaamini vipi na unajiridhisha vipi kama ni kweli?.

Je swala hili sio la kiimani mkuu?. Unataaluma yoyote ya mambo ya kibenki na fedha au maswala ya uchambuzi wa mambo?. Au ndiyo kusema sisi tusio amini ulicho tuandikia ndiyo bongo zetu zimekwisha safishwa?, au tunatumika kama usemavyo?
Mkuu Nilitegemea madongo kuhusiana na mada hii hasa kwa watu wa banks.Mada hii narudia ni taboo!Nilichoandika hapa ni kweli na nilishasema wengi wanafumbia macho kwa kuwa wana maslahi huko.Na wewe inawezekana una maslahi huko. Kama hata Marais wa Marekani wanakiri kwamba this is true, who are you to deny this truth. Ni ajabu sana.
 
Unapata ukakasi kwa kuwa issue hii ni taboo.Mfumo unaoitawala dunia umetuaminisha kwamba serikali zote za dunia zinachapa fedha zao,lakini si kweli.

Nilitaka kupita kimya ila umelilazimisha kukuuliza swali.
Hivi kila bank ikiwa na Uhuru was kuchapisha pesa unazani nini kitatokea?
 
oky kuna vitu nimejaribu ku generalize. kwanza ifahamike kwamba kila benki ina utaratibu wake katika utoaji wa mikopo, mfano benki nyingine zina compulsory sarving na zingine hazina. Valuation na search pia hutofautiana ktk mabenki au taasisi za kifedha pia hivi vitu hutegemea na nyaraka za mkopaji na kiwango anachoomba. nirudi kwwnye masuli
1. Processing fees/app fee hizi ni gharama za kushughulikia ombi la mkopo ( ufatiliaji, ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa mteja, uchanganuzi wa taarifa za mteja, uaandaaji wa nyaraka mblmbali)
2. loan insurance hii ni kwa ajili ya mkopo uliotolewa kwa mteja pindi ikitokea janga kwa mteja ambalo huweza kupelekea mteja kushidwa kulipa mkopo basi kuna asilimia ambayo hutegwa kwa ajili hio either na benki yenyewe au third part( insurance company) kuongezea hapo kuna life insurance hii ni endapo ikitokea mteja akifa hawezi kudaiwa mkopo aliokopa bali ile asilimia ya mkopo wake aliochajiwa ndio ita cover risk
3. Compulsory sarving ( kiwango cha lazima cha fedha ambacho kinatakiwa kibaki au kiwekwe na mteja kabla ya kupewa mkopo) hapa mabenki hutofautiana kwa aina tatu, kuna wanaotaka cumpulsory sarving iwekwe na mteja kabl hajapewa mkopo, kuna wanaomkata mteja kwenye kiwango cha mkopo alichoomba, kuna ambao hawataki.
4. Valuation na Search, kwanza inategemea na nyaraka za mteja alizokua nazo pia kiwango cha pesa anachoomba. Hili hufanywa ili kujua thamani yana uhakiki wa mali iliyowekwa (dhamana ya mteja) kwa ajili ya kuchukulia mkopo Mabenki yanatofautiana sana kwenye hili swala na ni pana kidogo. hizi ni direct cost mteja atakazolipa kwa benki au third part.
Uwizi/unyonyaji unakuja wp
1. Processing fee mf 5% ya mkopo uliomba huo ni unyonyaji live
2. Upande wa insurance sitapenda kuongelea sana maana ni ulinzi kwa both part (benki na mteja)
3. Valuation na search ( hapa kuna uwizi wa kiaina)
4.Cumpulsory sarving napo kuna janja janja hapo kwani hutegemea nyaraka za mali( collateral) alizotoa mteja kwa mkopo
NB:Nini lengo la kuchaji sustainable Interest Rate SIR
Hapo sijagusa riba ambapo ndo hapo watu wnapoliwa zaidi
Nina hakika hujui kwamba hata hiyo bank note inayokuwa issued na Bank yako ni fake,lakini huo ndio ukweli!Na Nina hakika pia hujui kwamba hizi bank notes zinapaswa kuwa only receipts received after depositing an equally valued amount of gold and silver and not money!Hivi mkuu unajua kwamba a bank note is paper like any other paper! Pole.
 
Nilitaka kupita kimya ila umelilazimisha kukuuliza swali.
Hivi kila bank ikiwa na Uhuru was kuchapisha pesa unazani nini kitatokea?
Hii inaonyesha mkuu kwamba you do not know what is going on. I thought you would read between the lines. Bank nyingi zinachapishiwa fedha zao Uingereza.Je unajua anayechapa huko ni nani na kuna makubaliano gani?Seated in Lilongwe kwa mfano Mmalawi anaambiwa Bank of Malawi inachapa fedha,but the money is printed in London!Mkuu can't you see the discrepancy.Huhitaji alot of brain to make sense out of it all.
 
Basi naona tunatofautiana kile tunaamini mkuu. Unaamini katika conspiracy theories without questioning. Wengine tunazisoma na kujaribu pia compare na other sources then tunaamini kwa namna hiyo. So kama feds bank hawajasema usemalo wewe, wewe una uhakika gani na usemacho?. Kumbuka wewe sio mfanyakazi wala founder wa hizo banks.

Kinyume na hapo utuambie hili ni swala la kiimani mkuu.
Mkuu unataka kuniambia Marais wa Marekani hawajui kinachoendelea Marekani,nakushangaa.But why are you denying plain truth.

Nyerere aliona utumwa huu,akakiri kwamba utakuwa mbaya kwa kuwa mtu ataambiwa ni mtumwa na hatakubali kwamba ni mtumwa.Some will even try to set him free, but he will still cling to the slavery because he does not know that he is a slave.I am just trying to make sense out of it all, but people don't seem to understand.
 
"I believe that banking institutions are more dangerous than standing armies...
If the american people will ever allow private banks to control the issue of currency... the banks and corporations that will grow around them will deprive the people of their own property until their children wake up homeless in the continent their fathers conquered"
~ Thomas jefferson
1743-1826
"If you want to remain slave of the bankers and pay for the costs of your own slavery, let them continue create money and control the nation's credit"
~ sir josiah stamp
1880-1941
Asante mkuu.Wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawasikii.
 
Hii inaonyesha mkuu kwamba you do not know what is going on. I thought you would read between the lines. Bank nyingi zinachapishiwa fedha zao Uingereza.Je unajua anayechapa huko ni nani na kuna makubaliano gani?Seated in Lilongwe kwa mfano Mmalawi anaambiwa Bank of Malawi inachapa fedha,but the money is printed in London!Mkuu can't you see the discrepancy.Huhitaji alot of brain to make sense out of it all.
Mbona unakataa bandiko lako??. Umesema benki zina leseni yakuchapisha pesa bila kuzifanyia kazi (wezi).
Huku kenye majibu unasema zinachapishiwa.
Sasa tujadili leseni ya kuchapisha au kuchapishiwa?????!.
Napia Mimi sijuli kiingilishi na kiswahili chenyewe shida. Hapo ndio umenitukana au umenisifia?.
 
Wakuu,
Mimi naona hapa aliyeanzisha uzi, makala hii ilikuwa ktk lugha ya kigeni na usipokuwa makini ukifanya tafsiri ya Kiswahili unapoteza maana na dhima nzima ya makala hii iliyokuwa ktk lugha ya kigeni.

Pia bank financial management (banking finance) ni utalaamu unaoupata kwa kusomea au kufanya kazi kwa muda mrefu ktk taasisi za kifedha na mabenki huku ukipata mafunzo kazini.

Sasa Mdau areafiftyone pamoja na nia yake nzuri ya kufanya tafsiri toka kugha ya kigeni kuja Kiswahili ktk uzi wake ametuchanganya na kuzua maswali mengi sana. Kufanya tafsiri inatakiwa kutulia na kuchukua muda pamoja na kuwa na uelewa wa kitaalamu ili tafsiri isipoteze maana ya makala halisi hasa ikiwa ni makala za utaalamu kama hii ili wasomaji waelewe tunachowasilisha.
Kama nimekosea kutafsiri mahali wewe rekebisha basi,sasa mbona hakuna input uliyoweka mkuu. Sana sana umewafurahisha tu wachangiaji wa bank,ambao ukweli huu kwao ni mchungu sana.
 
Mbona unakataa bandiko lako??. Umesema benki zina leseni yakuchapisha pesa bila kuzifanyia kazi (wezi).
Huku kenye majibu unasema zinachapishiwa.
Sasa tujadili leseni ya kuchapisha au kuchapishiwa?????!.
Akili za panzi hizi. Kama hawakuchapa Bank of Malawi wakachapa Bank of England si mfumo huo huo wa bank! Wake up Mtanzania.Who owns the Bank of Malawi and the Bank of England! Blind indeed.
 
Mtoa mada bila shaka anamatatizo anatoa mada asio ielewa.kwanza haiwezekani bank kuchapa pesa haita kuja tokea na kanuni za mafanikio ili upige hatua angalau kwa kasi lazima ukope muulize mengi baharesa matajiri wote duniani karibu walikopa ndio leo tunawaona matajiri tatizo wengi huzilaumu bank kwa kua tunaingia kukopa wakati mifumo yetu haiko vizuri binafs bank imenisogeza sana tena sana labda afafanue vizuri anamaana gani mtoa mada.
Umeshawahi kusikia juu ya mchezo wa madogori?Piga picha jinsi unavyoendeshwa unapata jibu.There is nothing scientific about banking, ni mchezo tu " watoto wa mjini"
 
Nina hakika hujui kwamba hata hiyo bank note inayokuwa issued na Bank yako ni fake,lakini huo ndio ukweli!Na Nina hakika pia hujui kwamba hizi bank notes zinapaswa kuwa only receipts received after depositing an equally valued amount of gold and silver and not money!Hivi mkuu unajua kwamba a bank note is paper like any other paper! Pole.
Muulize mtoa mada mm nimetoa mchango wangu kuhusiana na mambo ya mikopo, uzi sio wng usiniletee nyenyenyee ambayo sijaiongelea mm
 
Akili za panzi hizi. Kama hawakuchapa Bank of Malawi wakachapa Bank of England si mfumo huo huo wa bank! Wake up Mtanzania.Who owns the Bank of Malawi and the Bank of England! Blind indeed.

Nimegundua mwisho was upeo was akili zako.
Kama ishu ilikua kuchapishiwa ungetoa neno benki zina leseni ya kuchapisha pesa. pia majibu yako na bandiko lako hayaendani, ulijua tulip huku wrote ni mabashite?. endelea kusema tuamke huku ukuwa unaota,
Au zekebisha ulichoandika.
Vinginevyo hujui unajadili nini na nani.
 
Alafu mkuu kua makini, hii serikali ya mitandaoni hawakawii kukuleta pale kati udhibitishe haya madai
Sijazungumzia Tanzania mkuu,nimezungumzia bank kubwa ambazo zina impact kwenye agendas za dunia kama China Construction Bank, Wells Fargo & Co., HSBC Holdings,JP Morgan Chase, CitiGroup, Bank of America,Morgan Stanley, Standard Chartered,UBS,Barklays, nk.sio vibenki kama Umoja, NBC nk.
 
Akili za panzi hizi. Kama hawakuchapa Bank of Malawi wakachapa Bank of England si mfumo huo huo wa bank! Wake up Mtanzania.Who owns the Bank of Malawi and the Bank of England! Blind indeed.
Mkuu sidhani kama ni busara kumwambia mwenzako ana akili za panzi. Labda kuna jambo moja ambalo unapaswa kujua. Serikali ya Tanzania kwa hapa kwetu ndiyo yenye mamlaka kupitia BoT ya kuchapisha fedha.

Tunachopaswa kujua ni kwamba sisi kama nchi hatuna kiwanda cha kuchapa fedha, hivyo kazi hiyo huwa outsourced kwa makampuni ambayo ndiyo wataalam wa kuchapisha fedha hiyo. Nchi husika hutaja kiwango cha fedha wanacho hitaji kuchapwa, katika denominations zipi na ni features na materials gani wanataka ili kuweka durability, kuwa ngumu kufojiwa n.k

Fuatilia tu kwa hayo mataifa makubwa uyasemayo wewe. Marekani unajua kitengo chao cha kuchapa fedha?..

Pitia hapa chini.

U.S. Bureau of Engraving and Printing
 
Sijazungumzia Tanzania mkuu,nimezungumzia bank kubwa ambazo zina impact kwenye agendas za dunia kama Goldman Sachs, Barklays,Chase Manhattan nk.sio vibenki kama Umoja NBC nk.
Something is wrong somewhere. Hivi ni nani asiyejua kuwa kuna maswala ya Gold reserve kwa kila Central bank in relation to banking industry?.

Ni nani asiyejua mchango wa Gold kama means ya kutransact since miaka ya zamani sana?. Unaujua mchango wa Rothschild kwenye bank kuu ya uingereza ulitokana na nini kipindi hicho uingereza iko vitani?.

Sio kila mtu ni mjinga huku kwenye mitandao mkuu, huku kuna watu wa kila caliber. Na kwa mtu yoyote mstaarabu ni lazima ujenge hoja ili watu wakuelewe. Hayo uliyoyakuta kwenye mitandao kila mtu anaweza kuyasoma kiongozi, ila swala la ni kweli au lah ndo linabaki katika upeo wa kuamini na kung'amua sasa.

Kama maswala haya hutaki tujadili kisomi basi tupe mwelekeo as i once said. Maana tukienda kisomi tunaambiwa haya hayafundishwi darasani ni taboo. Tunayapata wapi basi, utaishia ambiwa kagoogle. Wewe mwenyewe wafahamu fika, ni kila kitu kilichoko kwenye mtandao ni sahihi?. Kama sio, kile kilichosahihi wewe una prove vipi?. Maswala mengine kuyaamini ni kama itikadi tu
 
Niliyegemea

Mkuu nimetoa ushahidi wa wazi wa Federal Reserve.Matatizo yetu Watanzania ni kuendelea starehe bila kupenda kujisomea, eventually tunakuwa na very shallow knowledge kuhusu issues.Worse still we think what we are taught in school is correct.Believe me most of it is rubbish. Tumeingizwa mkenge sana.Some of us are just trying to open your eyes,lakini kwa kuwa mnashupaza shingo chapweni.
Kwa hiyo mkuu unachotaka kutushauri kuhusu yanayofundishwa darasani ni nini?. Unataka tuambia kuwa formal education ni uongo mtupu?. Tugeukie kwenye aina ipi ya elimu?.

Na pia ni vyema utuwejee field basi ambazo elimu ya darasani haitusaidii. Unaposoma unapaswa elimika kwanza mkuu. Elimu ikupe uwezo wa kudeal na matatizo uliyonayo au yanayo izunguka jamii yako. Uwe na uwezo wa kutoa majawabu ambayo yatatua matatizo.

Ni wengi wamesoma ila bado hawajaelimika. Kuwa msomi sio kukariri mambo, unapaswa uwe na uwezo wa logical reasoning. Ndiyo maana tukaomba tupewe hizo sources nasi tukasome kama ulivyo soma wewe, tuzichambue pia na kufanya reasoning. Nadhani hapo tungeelewana sana.
 
Mleta mada, nakupongeza kwa sababu umefanya kazi kubwa ya kuwafumbua watu macho na masikio, tatizo lililopo ni kuwa Watanzania wengi hatuna uelewa juu ya maswala ya Fedha, sasa unapata shida kubwa kuelezea jambo ambalo kwanza watu hawataki kulielewa kwa kuwa wanaelewa kwa utaratibu wao.
Nachukua nafasi hii tena kukupongeza sana.
 
Back
Top Bottom