Nazungumzia mfumo wa dunia kwa ujumla.Ndio maana sijataja Tanzania.Marekani dola inachapwa na Federal Reserve Bank ambayo ni private institution.
Mkuu, hicho ulichokiandika una uhakika nacho?, kuwa federal reserve bank ni privately owned bank in America?. Je unajua mfumo wa federal reserve bank ya marekani inavyofanya kazi na iko chini ya utaratibu upi.
Narudia tena jiongezee maarifa. Mfano mdogo tu kwa hapa kwetu, Benki kuu ya taifa ndiye msimamizi mkuu wa mabenki nchini. Ndiyo benki inayo angalia mzunguko wa fedha nchini, ndiyo benki yenye mamlaka ya ku "issue" notes na coins zote tunazo tumia nchini.
Pia kuna mambo mengine ya kujifunza. Inawezekana kabisa ni kweli mabenki yanapata faida kubwa kutokana na huduma wanazo zitoa. Ila tunapaswa tujue pia benki ni lazima iwe na mtaji. Hamna benki inayoanzishwa kwa kutegemea eti tutapata mtaji au fedha za kukopesha pindi tutakapo anza pokea deposits.
Ni muhimu kujua kwamba benki nazo huko kutoka mabenki mengine makubwa. Na wanapo kopeshwa fedha hizo hutolewa kwa riba/cost of fund. Haya mabenki wanapo ziingiza fedha hizi kwenye mzunguko kwa njia ya mikopo basi hupanga riba kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na cost of fund iliyokuwa incurred kupata fedha hiyo, pia huangalia maswala ya mfumuko wa bei/inflation, na pia huweka faida.
Pia sehemu ya fedha hutoka kwa wananchi ambao kimsingi wao huweka akiba. Na akiba zinazo zungumziwa hapa ni zile fixed deposits na zifananazo na hizo. Wamiliki wa akaunti hizi hupata faida kutokana na fedha ambazo wao wameweka benki na benki wanatumia kukopesha.
Pia benki yaweza ongeza mtaji kwa kupitia kuuza hisa kwenye soko la hisa. Hii huifanya benki iweze kukuza mtaji na faida itakayo patikana katika shughuli za kila siku za kibenki basi kuja kugawiwa kwa wananchi walio wekeza mitaji yao, gawio hili hufanyika kwa kuangalia pia mambo mbalimbali.
Ni kweli riba zaweza kuwa juu kwa mabenki hapa nchini na kuwaumiza wananchi, lakini twapaswa pia tujielimishe kwa kile tunacho kuja kuandika humu. Tuangalie tusije fanya upotoshaji kwa mambo yaliyo wazi kabisa.