Jinsi mabenki yanavyonyonya na kuleta umaskini

Jinsi mabenki yanavyonyonya na kuleta umaskini

Haya ni majibu ambayo ni very general mkuu. Mimi naomba utusaidie jambo moja, inawezekana kabisa tunashindwa kuelewa au watu wanapoteza muelekeo kwa kuwa haijulikani inatakiwa tuchangie uzi huu katika angle/pembe gani.

Je, 1.tuchangie kwa kuweka uelewa na taaluma/profesionalism ya maswala ya fedha na benki kama kigezo cha kujadili bandiko lako?. Na je tunalijadili kama mfumo wa kibenki dunia bila kuhusisha nchi zetu?, kama ni la Elite wa dunia ya kwanza basi ujue kuna kitu cha NWO ambacho huwezi exclude nchi za dunia ya tatu.

2. Swala hili tulijadili kwa minajili ya kiimani tu kuwa kuna watu wanaendesha hii dunia. Kuwa kila tukionacho basi kiko nyuma ya watu fulani na tunapaswa amini tu hivyo bila kuhoji.

3. Swala hili tulijadili kwa maana ya kama "story za mitaani" ambazo tunazisikia huko mitandaoni lakini mimi na wewe hatuwezi dhibitisha kama ni kweli au lah.

Tupe muongozo kiongozi, vinginevyo utaona kama watu wanapingana na kile unacho kiamini na kila mtu ukamuona yuko "brain washed".
Mkuu sidhani kama nina jukumu la kukueleza jinsi ya kuchangia unless unaniambia hujaelewa bandiko.Katika bandiko nimezungumzia maeneo mbalimbali, ni jukumu lako kuyadadavua na kuchangia katika hayo. Kwa mfano nimesema bankers wanaohusika na kuwafanya some of our leaders wawe lousy, je una hoja mbadala? Au katika nchi fulani fulani duniani banks ndizo zinazochapa fedha, je una hoja mbadala nk.nk.
 
Mtoa mada bila shaka anamatatizo anatoa mada asio ielewa.kwanza haiwezekani bank kuchapa pesa haita kuja tokea na kanuni za mafanikio ili upige hatua angalau kwa kasi lazima ukope muulize mengi baharesa matajiri wote duniani karibu walikopa ndio leo tunawaona matajiri tatizo wengi huzilaumu bank kwa kua tunaingia kukopa wakati mifumo yetu haiko vizuri binafs bank imenisogeza sana tena sana labda afafanue vizuri anamaana gani mtoa mada.
 
Mkuu sidhani kama nina jukumu la kukueleza jinsi ya kuchangia unless unaniambia hujaelewa bandiko.Katika bandiko nimezungumzia maeneo mbalimbali, ni jukumu lako kuyadadavua na kuchangia katika hayo. Kwa mfano nimesema bankers wanaohusika na kuwafanya some of our leaders wawe lousy, je una hoja mbadala? Au katika nchi fulani fulani duniani banks ndizo zinazochapa fedha, je una hoja mbadala nk.nk.
1.Maana tukikwambia ni conspiracy theories umeishia sema watawala wa dunia wananitumia kwa kujua au kutokujua --- kwangu hili ni swala la kiimani zaidi.

2. Umelalamika sana kwa swala la mabenki in general na hakuna mahali katika bango lako la awali ulisema swala la uchapishaji wa fedha ni kwa nchi fulani na uzitaje majina na kuiondoa Tz. Ulichofanya ni kujumuisha, tukahoji ukatuambia wewe huzungumzii mambo haya katika upeo mdogo bali mfumo wa kibenki duniani.

3. Umekuja na vitu unavyo viita reference ambavyo kiuhalisia sio. Unasema nenda kagoogle neno flani, yakija mia nasoma lipi?. Wewe umesoma yote na kuyajengea hoja hapa?. Je ni kwa nini hutoi links za webs kama unavyoombwa?. Kile unacho kuamini wewe unataka sisi ndicho tukiamini, tukikupa links unasema hao hawawezi sema ukweli, hao wewe ulikosoma ambazo sio taasisi husika unaamini vipi na unajiridhisha vipi kama ni kweli?.

Je swala hili sio la kiimani mkuu?. Unataaluma yoyote ya mambo ya kibenki na fedha au maswala ya uchambuzi wa mambo?. Au ndiyo kusema sisi tusio amini ulicho tuandikia ndiyo bongo zetu zimekwisha safishwa?, au tunatumika kama usemavyo?
 
Mkuu Marekani wanachapa Federal Reserve Bank ambayo ni private institution,which is owned by the Rothschild family, Uingereza Bank of England ambayo pia ni private institution also owned by the Rothschilds!

Ndugu pata muda ukasome zaidi na kufanya reference zako kwa usahihi...Hakuna any Central Bank popote duniani ambayo ni Private Bank.....Ni vizuri ukauliza kwa sisi wataalamu wa maswala hayo ambao tumo humu, kabla ya kupost articles ambazo zinamwelekeo potofu kabisa...
 
kitengo cha mikopo ndo kinaongoza kwa unyonyaji kwa wateja sijapata ona. mfano unaenda kukopa 60m. kuna kitu kinaitwa processing fee, loan insurance, compulsory sarving,valuation,search fee, legal hapo bado hujamtoa credit officer. waweza kuta kwenye 60m unaondoka na 53m lakini rejesho lako linakua ni la 60m ambalo humo ndani na riba juu. kama huna biashara za uhakika usikope utakwisha kuna uwizi mkubwa kwenye mabenki hasa kwenye mikopo
 
45df0f69eda4efdf6747927c55a0d73c.jpg
 
Hivi kwa nini ma-bank ambayo hayazalishi chochote (isipokuwa kuwapatia wateja wao huduma zisizo za viwango) nimatajiri kuliko taasisi zingine?Angalia Chase nManhattan,Goldman Sacks, Barcklays nk. Na inakuaje kila biashara inakabiliwa na madeni ya bank?
Na inakuaje bank ndizo zenye majengo mazuri mjini tena bila mortgage au mkopo wa aina yeyote,wakati viwanda na watu wengine wanahangaika usiku na mchana ili kuweza kulipa mikopo ya ma-bank waliyopata kwa kuweka dhamana mali zao?

Mtu angedhani watu wa viwanda na Kilimo ambao wanazalisha bidhaa muhimu kwa maisha ya watu,ndio ambao wangekuwa matajiri zaidi ya wenye mabenki ambao kwa asili walikuwa wawekaji tu na watunzaji wa fedha za wateja wao na wenye mabenki wangekuwa watumishi tu,tena wa chini wa wenye viwanda nk,lakini sio. Siri ni nini?

Siri ni kwamba bank zina "leseni"ya kuchapa fedha,fedha ambazo hazitokani na kufanya kazi,au fake money, au money created out of nothing! Wenye viwanda na wateja wengine wamebanwa na ukweli huu mchungu mno.

Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mtu anayetaka kuongelea ukweli huu,ambao unaonekana kama taboo. Wataalam wetu wa uchumi,wana siasa,wana habari, watawala,wanaelekea kutokuwa tayari kuzungumzia swala hili. Vitabu vyote, makala zote, mikataba, majarida, documentaries za TV,vikundi mbali mbali vya majadiliano,vyuo vikuu,taasisi zingine mbali mbali,wote wako kimya kuhusu uonevu huu, kana kwamba haupo.

Rothschild Brothers(London,1863)wamesema,
"Wachache wanaoelewa mfumo huu hawataki kabisa kuuongelea kwa sababu ya faida wanazozipata."

Njia rahisi ya kuona jinsi bank zinavyofanya kazi ni kufikiria piramidi iliyogeuzwa, upande uliochongoka chini na upande bapa juu. Sehemu iliochongoka inawakilisha fedha halisi za bank,ambazo zamani zilikuwa ni coins za dhahabu na fedha.Juu ya hapo ni viwango mbali mbali vya mikopo kwa wateja wa mabenki.

Mikopo hii sio fedha halisi,kwa kuwa haikupatiiokana kwa kufanya kazi! Hata hivyo wateja waliochukua mikopo hii, inabidi walipe mikopo hiyo na faida kutumia fedha halisi ambazo wamevuja jasho kuzipata!Huu ndio mfumo wa ajabu ambao tunautumikia kwa miaka mingi na mfumo ambao ndio kwa kweli unaofanya thamani ya fedha ipungue.

Ingekuwa busara kama serikali za dunia zingekuwa na vitengo maalum vinayvohusika na uchapaji wa fedha. Kwa namna hiyo serikali zisingehangaika na madeni ya ndani.Ni jambo la ajabu kwamba tumeruhusu bank zichapishe fedha na kubadili riba wanavyotaka.Si ajabu kwa hiyo kwamba tunakuwa na vipindi vya hali nzuri ya uchumi (boom and slumps or financial crises and depressions),vitu ambavyo vinasababishwa na kuongezeka au kupunguza fedha kwenye circulation,hali ambayo imeyapa mabenki mamlaka kubwa mno juu yetu.Hii imeleta hali ya kuwa na watu ndani ya mabank wenye mamlaka kubwa mno.Watu hawa hawawajibiki kwa yeyote isipokuwa kwao wenyewe.Kwa kutumia nguvu ya pesa waliyo nayo wamenunua wana siasa na kuwa na ajenda za ajabu zenye nia ya kuendelea kujilimbikizia mamlaka na madaraka ili wasiguswe.Hatimaye wanaishi maisha ambayo sisi wengine tunayaota tu.
Kupitia kwa wanasiasa hao na kutoa misaada kwa vikundi mbali mbali kama Freemasons,Club of Rome,Council of Foreign Relations,Media na Charities mbalimbali,mabenki yameweza kuwa na maamuzi makubwa kwenye nchi nyisecrengi duniani.Wako nyuma ya uanzishwaji wa tu kama European Union,African Union na jumuiya zingine za kikanda.Hawa pia ndio wanaohusika kwa kiwango kikubwa kuwafanya viongozi wengi wawe wasioeleweka na kusema ukweli.
References:
Google
1.The hidden secrets money.
2.Ancient banking secret.
3.The FED(The Federal Reserve Bank) is a commercial privately owned bank.
4.Federal Reserve Bank ownership. Factcheck.org
5.Google pia "Quotes on Banking and the Federal Reserve system FRAUD"upate ukweli zaidi.Hizi quotes kama zitasomwa zitaleta uelewa mkubwa sana juu ya mada iliyoko mezani.
Naomba nikumbushe kwamba mada hii kwa kawaida hakuna mtu aliyeko tayari kuzungumzia,kwa hiyo haifundishwi darasani!Come with an open mind kwa nia ya kujifunza.Ubishi bila facts hautatusaidia sana.
Ndefuuu afu hakuna kinachoeleweka
 
kitengo cha mikopo ndo kinaongoza kwa unyonyaji kwa wateja sijapata ona. mfano unaenda kukopa 60m. kuna kitu kinaitwa processing fee, loan insurance, compulsory sarving,valuation,search fee, legal hapo bado hujamtoa credit officer. waweza kuta kwenye 60m unaondoka na 53m lakini rejesho lako linakua ni la 60m ambalo humo ndani na riba juu. kama huna biashara za uhakika usikope utakwisha kuna uwizi mkubwa kwenye mabenki hasa kwenye mikopo
Mkuu, inawezekana kweli kabisa usemayo yana ukweli kwa kiasi fulani. Embu ngoja tuyaorozeshe haya uliyoyataja alafu utuambie kama unaelewa kwanini hufanyika hivyo.

1. Processing /application fee - unaelewa ni ya nini?.

2. Loan insurance fee - unajua no ya nini na unajua iko kisheria?.

3. Compulsory Savings - unaelewa maana ya hii?, mikopo inayochajiwa hii ni ya asili ipi?. hapa nashindwa kuelewa huo mkopo wa 60m unakuwa na cumpulsory savings ya nini na ni wa asili gani.

4. Valuation fee - Je hii ni bank wanafanya au ni fedha unamlipa valuer?. Unaelewa kwanini valuation huhitajika haswa kwa mikopo ya kati na mikubwa katika mabenki?.

5. Search fee - Je hii unajua hufanyika kwa nini?. Je ni lazima uwape bank wakafanye search au waweza fanya wewe kisha wewe uwapelekee ripoti?.

6. Legal fee - Hii unazungumzia ipi?. Unailipa bank au huko unakoenda kufanya hizo taratibu za kisheria?.

7. Hilo la kumtoa afisa - hiyo ni rushwa ndugu yangu, kuwa makini.

Embu eleza mkuu vile unaelewa walau tusaidiane hapa kujua mawili matatu
 
oky kuna vitu nimejaribu ku generalize. kwanza ifahamike kwamba kila benki ina utaratibu wake katika utoaji wa mikopo, mfano benki nyingine zina compulsory sarving na zingine hazina. Valuation na search pia hutofautiana ktk mabenki au taasisi za kifedha pia hivi vitu hutegemea na nyaraka za mkopaji na kiwango anachoomba. nirudi kwwnye masuli
1. Processing fees/app fee hizi ni gharama za kushughulikia ombi la mkopo ( ufatiliaji, ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa mteja, uchanganuzi wa taarifa za mteja, uaandaaji wa nyaraka mblmbali)
2. loan insurance hii ni kwa ajili ya mkopo uliotolewa kwa mteja pindi ikitokea janga kwa mteja ambalo huweza kupelekea mteja kushidwa kulipa mkopo basi kuna asilimia ambayo hutegwa kwa ajili hio either na benki yenyewe au third part( insurance company) kuongezea hapo kuna life insurance hii ni endapo ikitokea mteja akifa hawezi kudaiwa mkopo aliokopa bali ile asilimia ya mkopo wake aliochajiwa ndio ita cover risk
3. Compulsory sarving ( kiwango cha lazima cha fedha ambacho kinatakiwa kibaki au kiwekwe na mteja kabla ya kupewa mkopo) hapa mabenki hutofautiana kwa aina tatu, kuna wanaotaka cumpulsory sarving iwekwe na mteja kabl hajapewa mkopo, kuna wanaomkata mteja kwenye kiwango cha mkopo alichoomba, kuna ambao hawataki.
4. Valuation na Search, kwanza inategemea na nyaraka za mteja alizokua nazo pia kiwango cha pesa anachoomba. Hili hufanywa ili kujua thamani yana uhakiki wa mali iliyowekwa (dhamana ya mteja) kwa ajili ya kuchukulia mkopo Mabenki yanatofautiana sana kwenye hili swala na ni pana kidogo. hizi ni direct cost mteja atakazolipa kwa benki au third part.
Uwizi/unyonyaji unakuja wp
1. Processing fee mf 5% ya mkopo uliomba huo ni unyonyaji live
2. Upande wa insurance sitapenda kuongelea sana maana ni ulinzi kwa both part (benki na mteja)
3. Valuation na search ( hapa kuna uwizi wa kiaina)
4.Cumpulsory sarving napo kuna janja janja hapo kwani hutegemea nyaraka za mali( collateral) alizotoa mteja kwa mkopo
NB:Nini lengo la kuchaji sustainable Interest Rate SIR
Hapo sijagusa riba ambapo ndo hapo watu wnapoliwa zaidi
 
Mkuu, inawezekana kweli kabisa usemayo yana ukweli kwa kiasi fulani. Embu ngoja tuyaorozeshe haya uliyoyataja alafu utuambie kama unaelewa kwanini hufanyika hivyo.

1. Processing /application fee - unaelewa ni ya nini?.

2. Loan insurance fee - unajua no ya nini na unajua iko kisheria?.

3. Compulsory Savings - unaelewa maana ya hii?, mikopo inayochajiwa hii ni ya asili ipi?. hapa nashindwa kuelewa huo mkopo wa 60m unakuwa na cumpulsory savings ya nini na ni wa asili gani.

4. Valuation fee - Je hii ni bank wanafanya au ni fedha unamlipa valuer?. Unaelewa kwanini valuation huhitajika haswa kwa mikopo ya kati na mikubwa katika mabenki?.

5. Search fee - Je hii unajua hufanyika kwa nini?. Je ni lazima uwape bank wakafanye search au waweza fanya wewe kisha wewe uwapelekee ripoti?.

6. Legal fee - Hii unazungumzia ipi?. Unailipa bank au huko unakoenda kufanya hizo taratibu za kisheria?.

7. Hilo la kumtoa afisa - hiyo ni rushwa ndugu yangu, kuwa makini.

Embu eleza mkuu vile unaelewa walau tusaidiane hapa kujua mawili matatu
5. Valuation na Search ukisema ufanye mwenyewe upeleke riporti si utatoa ripot za uongo ili ionekane dhamana yako inafaa kupewa kiasi cha mkopo ulichoomba. Mara nyingi benki wanafanya wenyewe au wnatafuta third part wanayoiamin wao na kuwapa hio kazi. Hapo pia kuna ujanja hufanyika mkuu
6. Legal fee benki nyingine hutafuta wnasheria wa nje kwa ajili ya kumsainisha mteja pindi kunapotokea mgogoro na benki basi mteja huweza kusaidiwa na huyo mwanasheria
7. Ndugu yangu Credit Officer ndo kila kitu anaweza kukusaidia kwenye nambo mengi ambayo ww huna vigezo vya kupewa hela.
 
Mada iko very clear kuhusu Mabenki duniani na fedha.Ni biashara nzuri sana ya fedha kwa wenye Benki.

Ingawaje kila nchi ina Sheria na Sera zake za Fedha ila fedha zote zilizopo Benki zinatoka kwa Wateja wao.
 
5. Valuation na Search ukisema ufanye mwenyewe upeleke riporti si utatoa ripot za uongo ili ionekane dhamana yako inafaa kupewa kiasi cha mkopo ulichoomba. Mara nyingi benki wanafanya wenyewe au wnatafuta third part wanayoiamin wao na kuwapa hio kazi. Hapo pia kuna ujanja hufanyika mkuu
6. Legal fee benki nyingine hutafuta wnasheria wa nje kwa ajili ya kumsainisha mteja pindi kunapotokea mgogoro na benki basi mteja huweza kusaidiwa na huyo mwanasheria
7. Ndugu yangu Credit Officer ndo kila kitu anaweza kukusaidia kwenye nambo mengi ambayo ww huna vigezo vya kupewa hela.
Kuna mengi umeyazungumza hapo mkuu, mengine kifedha yako correct kabisa. Ila kuna ambayo kimsingi ndiyo unasema kila benki ina taratibu zake. Sio kila benki ina longolongo zote hizo, na sio kila mkopo basi officer wa mkopo lazima apewe fedha. Mambo mengine ni urasimu tu wa watu ndiyo umetufikisha hapo.

Pia wajua mabenki walikuwa wanakopa kwa asilimia ngapi huko BoT?. Na imeathiri vipi riba ambayo mabenki walichaji wateja wao pindi wanapokopesha hizi fedha?.
 
Mkuu vipi una hangover nini??? Benki gani hizo unazungumzia wana chapisha fedha??

Kiufupi bank wanaingiza pesa nyingi sana kupitia unyonyaji wa mikopo ambao serikali imeufimbia macho, pesa zetu hizi hizi wanakopesha at around 20% interest, wanakatia bima mkopo yaani kwa kifupi hela yao haipotei hata kidogo

Benki zinatajirika kwa kutunyonya wananchi lakini kusema kwamba wanachapisha fedha.... Man, that's a joke!
20% kwa mwaka ni riba nafuu sana
 
Mwandishi kasikia sikia hbr hii kakimbilia kuja kuipost hata yeye mwenyewe haielew. ETI BANKS ZINACHAPA PESA? HALAF HAELEWI KUWA KUANZISHA BANK KUNAHITAJ MTAJI AU UWEKEZAJI. mwandishi hafaham na ndo maana haeleweki. Bank zingekuwa zinachapa pesa basi zisingefilisika. Na pesa zingekuwa nying sana. Haelewi anazungumzia nini.
 
Hi mchumi kutoka kolomije naomba niulize swali, kama benki zinapewa leseni ya kuchapa fedha zake nini kazi ya BOT katika hilo, na kwa nini Twinga Bank hivi karibuni ilikubali kufa kifo cha mende wakati kuna option hiyo?
Inawezekana kuchapisha kuna gharama kubwa zilizopelekea hiyo benki kukwama (Mtoa mada kazusha hili haliwezekani)
 
Kuna mengi umeyazungumza hapo mkuu, mengine kifedha yako correct kabisa. Ila kuna ambayo kimsingi ndiyo unasema kila benki ina taratibu zake. Sio kila benki ina longolongo zote hizo, na sio kila mkopo basi officer wa mkopo lazima apewe fedha. Mambo mengine ni urasimu tu wa watu ndiyo umetufikisha hapo.

Pia wajua mabenki walikuwa wanakopa kwa asilimia ngapi huko BoT?. Na imeathiri vipi riba ambayo mabenki walichaji wateja wao pindi wanapokopesha hizi fedha?.
Kwanza nilikua naweka wazi ni namna gn hizo taratibu zinavyo muathiri mteja kabla hata hajauchukua huo mkopo na ukifuatilia kwa makini utajua ni unyonyaji wa hali ya juu hapo ni kabla hata hujachajiwa riba ambapo ndani ya riba napo kuna madudu.
Nikweli swala la kumtoa officer haliko kiutaratib, lakin muda mwingi wateja wanapwaya kwenye vigezo vya kupatiwa mkopo hivyo afisa hufanya kazi ya ziada
Swala la kukopa benki kuu au benki nyingine za kibiashara linaathiri riba kwa maana kiwango cha riba ambacho atachajiwa mteja kitakua kikubwa. Kwa riba itakayolipwa inatakiwa itoshe kulipa benki 2. Mf km benki A imekopa kwa benki B kwa 14% riba atakayochajiwa mteja huenda ikapaa hadi 22% ili benki A iweze kupata faida na pia kuilipa benki B. Kwa mfano huo benki A huenda ikaathirika endapo wateja wake hawatalipa kwa wakati au km hawatalipa kabisa, pia endapo kiwango cha riba kitabadilika kutokana na mfumuko wa bei katika soko la fedha, hapa itategemea makubaliano baina ya benki A na B. NB ukopaji wa benki moja kutoka benki nyingine sio njia nzuri ya kujiendesha kifedha japo benki au taasisi za kibenki hufanya hvyo. Mfano mzur ni kwa SACCOS nying hufa kwa kutumia mbinu hiyo
 
Back
Top Bottom