Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,035
- 22,713
Hivi kwa nini ma-bank ambayo hayazalishi chochote (isipokuwa kuwapatia wateja wao huduma zisizo za viwango) nimatajiri kuliko taasisi zingine?Angalia Wells Fargo & Co., HSBC Holdings,JP Morgan Chase, CitiGroup,Bank of America,Morgan Stanley nk. Na inakuaje kila biashara inakabiliwa na madeni ya bank?
Na inakuaje bank ndizo zenye majengo mazuri mjini tena bila mortgage au mkopo wa aina yeyote,wakati viwanda na watu wengine wanahangaika usiku na mchana ili kuweza kulipa mikopo ya ma-bank waliyopata kwa kuweka dhamana mali zao?
Mtu angedhani watu wa viwanda na Kilimo ambao wanazalisha bidhaa muhimu kwa maisha ya watu,ndio ambao wangekuwa matajiri zaidi ya wenye mabenki ambao kwa asili walikuwa wawekaji tu na watunzaji wa fedha za wateja wao na wenye mabenki wangekuwa watumishi tu,tena wa chini wa wenye viwanda nk,lakini sio. Siri ni nini?
Siri ni kwamba bank zina ndizo zinazochapa fedha,fedha ambazo hazitokani na kufanya kazi au money, created out of nothing! Wenye viwanda na wateja wengine wamebanwa na ukweli huu mchungu mno.
Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mtu anayetaka kuongelea ukweli huu,ambao unaonekana kama taboo. Wataalam wetu wa uchumi,wana siasa,wana habari, watawala,wanaelekea kutokuwa tayari kuzungumzia swala hili. Vitabu vyote, makala zote, mikataba, majarida, documentaries za TV,vikundi mbali mbali vya majadiliano,vyuo vikuu,taasisi zingine mbali mbali,wote wako kimya kuhusu mfumo huu mbovu, kana kwamba haupo.
Rothschild Brothers(London,1863)wamesema,
"Wachache wanaoelewa mfumo huu hawataki kabisa kuuongelea kwa sababu ya faida wanazozipata."
Njia rahisi ya kuona jinsi bank zinavyofanya kazi ni kufikiria piramidi iliyogeuzwa, upande uliochongoka chini na upande bapa juu. Sehemu iliochongoka inawakilisha fedha halisi za bank,ambazo zamani zilikuwa ni coins za dhahabu na fedha.Juu ya hapo ni viwango mbali mbali vya mikopo kwa wateja wa mabenki.
Mikopo hii sio fedha halisi,kwa kuwa haikupatikana kwa kufanya kazi! Hata hivyo wateja waliochukua mikopo hii, inabidi walipe mikopo hiyo na faida kutumia fedha halisi ambazo wamevuja jasho kuzipata!Huu ndio mfumo wa ajabu ambao tunautumikia kwa miaka mingi na mfumo ambao ndio kwa kweli unaofanya thamani ya fedha ipungue.
Ingekuwa busara kama serikali za dunia zingekuwa na vitengo maalum vinayvohusika na uchapaji wa fedha. Kwa namna hii serikali zisingehangaika na madeni ya ndani.Ni jambo la ajabu kwamba tumeruhusu bank zichapishe fedha na kubadili riba wanavyotaka.Si ajabu kwa hiyo kwamba tunakuwa na vipindi vya hali nzuri ya uchumi (boom and slumps or financial crises and depressions),vitu ambavyo vinasababishwa na kuongezeka au kupunguza fedha kwenye circulation,hali ambayo imeyapa mabenki mamlaka kubwa mno juu yetu.Hii imeleta hali ya kuwa na watu ndani ya mabank wenye mamlaka kubwa mno.Watu hawa hawawajibiki kwa yeyote isipokuwa kwao wenyewe.Kwa kutumia nguvu ya pesa waliyo nayo wamenunua wana siasa na kuwa na ajenda za ajabu zenye nia ya kuendelea kujilimbikizia mamlaka na madaraka ili wasiguswe.Hatimaye wanaishi maisha ambayo sisi wengine tunayaota tu.
Kupitia kwa wanasiasa hao na kutoa misaada kwa vikundi mbali mbali kama Freemasons,Club of Rome,Council of Foreign Relations,Media na Charities mbalimbali,mabenki yameweza kuwa na maamuzi makubwa kwenye nchi nyingi duniani(kama Ugiriki:Goldman Sacks) .Wako nyuma ya uanzishwaji wa mamlaka kama European Union,African Union na jumuiya zingine za kikanda.Hawa pia ndio wanaohusika kwa kiwango kikubwa kuwafanya viongozi wengi wawe wasioeleweka na kusema ukweli.
References:
Google
1.The hidden secrets money.
2.Ancient banking secret.
3.The FED(The Federal Reserve Bank) is a commercial privately owned bank.
4.Federal Reserve Bank ownership. Factcheck.org
5.Google pia "Quotes on Banking and the Federal Reserve system FRAUD"upate ukweli zaidi.Hizi quotes kama zitasomwa zitaleta uelewa mkubwa sana juu ya mada iliyoko mezani.
Naomba nikumbushe kwamba mada hii kwa kawaida hakuna mtu aliyeko tayari kuzungumzia,kwa hiyo haifundishwi darasani!Come with an open mind kwa nia ya kujifunza.Ubishi bila facts hautatusaidia sana.Ikumbukwe pia kwamba naongelea banking kama ilivyo duniani especially kwenye bank ambazo zinaweza ku-influence world agenda kama Wells Fargo & Co, HSBC Holdings,JP Morgan Chase,CitiGroup,Bank of America,Morgan Stanley, Standard Chartered, UBS nk.Hata hivyo iwe noted kwamba bank hizi kubwa either zina own the other smaller banks au zina influence indirectly.