Ras John I
Member
- Oct 3, 2017
- 39
- 22
Asubuhi ya leo nilipoamka baada ya kusali na kufanya tafakari fupi niliamka na kwenda nje ili niweze kuliwahi jua la asubuhi ambalo kwa kweli huifanya siku yangu iwe nzuri sana nilitoa simu yangu na kuanza kuangalia ni nini kimeendelea mitandaoni kwani mara nyingi niendapo kulala huwa nazima simu yangu na kuiweka mbali na nilipolala kwani Imani yangu inaniambia kulala na simu kuna madhara makubwa kiafya ambayo si rahisi mno kuyajua kwa mtu wa kawaida.
Wakati naangalia nilipokea ujumbe kutoka kwa rafiki yangu wa karibu ujumbe huo ulikuwa unasomeka kama ifuatavyo “Rasta naomba unisaidie nifanye nini ili niweze kumsahau mtu ni mpendaye” mimi kama binadamu wa kawaida na ambaye nimepitia mahusiano mbalimbali ya kimapenzi na kirafiki na yakaniumiza niliwaza juu ya huyu rafiki yangu na kujaribu kufikiria sasa atakuwa kwenye hali gani, nikajaribu kukumbuka nyakati hizo na jinsi gani nilivyokuwa na umia, hivyo nikaomba muda kidogo niweze kuandaa kitu ambacho kilinisaidia mimi na huenda kikamsaidia yeye na wengine ambao wako katika wakati ambao anapitia yeye.
JINSI KUACHA KUMUWAZA YULE UMPENDAYE.
a) Kukubali kuwa unamkumbuka huyo mtu,
Lazima kwanza ukubali kuwa unamkumbuka huyo mtu na nib ado yupo kwenye kichwa chako na fikira zako ondoa tabia ya majisifu (egoism) na ruhusu fikra zako na wewe mwenyewe kumkumbuka mtu huyo, na tambua kwamba si jambo baya kumkumbuka mtu na jisikie fahari kwamba unao uwezo wa kumkumbuka mtu.
b) Ishi kwenye wakati uliopo,
Fanya kila jambo kwa wakati husika, wakati wakula ufanye uwe wakati wa kula na sio ule huku ukiwa unamawazo manne kwa wakati mmoja amini kuwa kila jambo lina wakati wake na mwisho wa nyakati ufikapo lazima kuwe na matokeo flani, na pia kumbuka kuwa( mawazo yaliyopitiliza humdhoofisha mwanadamu kwnye shughuli zake za kila siku) hivyo tambua wakati umefika na huna budi kukubaliana na matokeo hayo kwani mwisho wa siku maisha lazima yataendelea tu.
c) Tambua hakuna mahusiano makubwa kama mahusiano yako mwenyewe.
Hakuna mahusiano makubwa kama mahusiano ya mwanadamu na nafsi yake mwenyewe, na hivyo lazima ukumbuke kuwa mara nyingi mahusiano kati ya mwanadamu na mwanadamu yakivunjika kinachotuumiza sio yule mtu bali ni zile nyakati tofauti ambazo tulikuwa tukifurahia kwa pamoja. Na pia lazima kujiuliza ni kitu gani haswa ambacho tunakikumbuka kutoka kwa mtu yule ambaye tumevunja nae uhusiano, tengeneza usawa kati ya zile nyakati nzuri na nyakati mbaya ambazo mlizipitia kwa pamoja wakati mkiwa wote.
d) Furahi kuwa unao uwezo wa kumkumbuka mtu.
Unapokuwa na uwezo wa kumkumbuka mtu kiasi cha kupata maumivu hicho ni kiashiria kuwa unazo HISIA, kuna watu wengi kwenye huu ulimwengu ambao hawana hisia, na kuwa na hisia ni kiashiria pia kuwa UNAO UWEZO WA KUMPENDA MTU MWINGINE, na pia jiulize kuwa “kama uliweza kumpenda mtu asiye sahihi kwa kiasi hicho, Je itakuwaje utakavyo mpenda mtu sahihi? Lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu SAHIHI na ASIYE SAHIHI kwenye huu ulimwengu lakini ukweli ni kuwa wapo watu ambao wanatusaidia sisi kukua na kuwa watu imara, kila mtu unayekutana naye kwenye maisha aliyekuumiza na ambaye hajakuumiza wote wana kitu kipaya cha kukufundisha.
e) Muda hutibu kila kitu.
Amini kuwa muda ni tabibu wa kila kitu na kwamba muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa sawa na maumivu yatakuwa hayapo na yalisha sahaulika yote, unakumbuka miaka miwili iliyopita ambapo mpenzi wako au rafiki yako alikuumiza na ukaamua kuwa sitokuwa na mpenzi au rafiki tena? Muda mfupi uliofuata ukasahau kila kitu na ukawa mtu mpya tena, hivyo amini kwenye muda na kwamba muda si mrefu kila kitu kitakuwa sawa.
f) Kutana nao(naye) uso kwa uso.
Usimkimbie yule aliyekuumiza na mwenye kukufanya umuwaze na kumkumbuka mara kwa mara kutana nae uso kwani huenda kuna kitu kikubwa ndani yake ambacho kinakufanya wewe uendelee kumkumbuka mara kwa mara.
[HASHTAG]#Kumbuka[/HASHTAG] pia sio kila mtu unayetengana naye kwenye maisha yako huleta hasara, na pia sio hasara hasa pale unapojifunza kitu kipya kutoka kwa watu, kuwa na furaha kwamba umepata ujuzi Fulani kutoka kwa watu ambao umekutana nao kwenye maisha yako, kwani utakusaidia katika wakati huu na ujao kwenye haya maisha yako.
Rasta John