Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Unaona ulivyo mweupe kichwani...kwa hiyoo Mpaka Leo Hii hujui Katibu ndo inayotuongoza kutenda mambo na sio yanayotoka kichwani tu..sijibizani na wewe tena ngoja nikuache na akina BAK
Sasa umesoma ibara ya 30(1)
 
Inabidi watu waelishwe kuhusu kuijua katiba yao. Maana akina Tundu wanawahadaa wananchi.
 

Uko sahihi Mkuu. TL anatumia utaalamu wake wa sheria vibaya
 
Acha kujidharirisha... Gusa sheria ya vyama vya siasa 4 na 5 alafu utuambie niwapi rais aamepewa mamlaka ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano? Ilo ndo jambo la msingi
 
Acha kujidharirisha... Gusa sheria ya vyama vya siasa 4 na 5 alafu utuambie niwapi rais aamepewa mamlaka ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano? Ilo ndo jambo la msingi
Nimeshakueleza tayari. Kwamba hapa tunaongelea katiba.
Katiba inatoa limit ya uhuru na haki kwenye ibara ya 30(1).
Usilazishe kilichopo kichwani mwako kiwe katiba.
 
Nguvu kubwa inayotumiwa na ccm,ungalidhani wao ndio minority..........
 
Lisu anatumia itaalamu wake wa sheria kupotosha watu. Mwisho wake utafika.
 
Nguvu kubwa inayotumiwa na ccm,ungalidhani wao ndio minority..........
Hapa tunajaribu kuelimisha wananchi kuhusu katiba yao.
 
Acha kujidharirisha... Gusa sheria ya vyama vya siasa 4 na 5 alafu utuambie niwapi rais aamepewa mamlaka ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano? Ilo ndo jambo la msingi
sheria ya vyama vya siasa na katiba IPI IPO juu ya kingine? Kwa taarifa yako sheria ya vyama vya siasa ina derive its aotomasy kutoka kwenye katiba, hence the that law is applicable subject to the provisions of the constitution and other laws, and among these provision ni Article 30, na ikitokea sheria ya kawaida inakinzana na katiba badi katiba inasimama.

Sasa katiba imeweka limitations kwenye kufurahia haki zote za msingi zinazopatikana from Article 13 hadi 27-28, hako kasheria kako unakosema ambako ni matokeo ya katiba hiyo kanakwepaje kuathiriwa na limiatations zilinaxoainishwa under Article 30.
Acha porojo kasome Article 30, japo cjui hiyo katiba yenyewe kama hata unajua inafananaje
 

Haya na wewe ni kichwa...
 
Serikali pamoja na Rais wameapa kuilinda Katiba.Hivi ukiwapa Haki CDM ya kisheria ya kuandamna na kufanya mikutano wanapoteza nini??Wa kwanza kujishtaki ni Rais na Serikali yake ifuate Sheria na Katiba waliyoaapa kuilinda Mengine ni blahblah.
Katiba imeweka wazi kama Rais anaenda kinyume na katiba Mtanzania yeyote anayo haki ya kufungua kesi mahakamani dhidi yake.

CDM mbona hawaendi mahakamani kufanya hivo, maana mahakama ndo chombo pekee chenye mamlaka ya kutafisiri katiba na swala sio Tundu Lissu!
 
Haya na wewe ni kichwa...
Mm siyo kichwa lkn atleast bado nimebaki na uwezo wangu wa kufikiri, kuliko ww ambaye imeweka rehani haki yako ya kufikiri na kuwaacha wanaume wenzako wafikiri kwa ajiri yako!
 
Mm siyo kichwa lkn atleast bado nimebaki na uwezo wangu wa kufikiri, kuliko ww ambaye imeweka rehani haki yako ya kufikiri na kuwaacha wanaume wenzako wafikiri kwa ajiri yako!

Nimekupongeza wewe kichwa sasa unajidhalilisha.. haya sijibu mtu anayeandika hivyo...
 
Vipengele vyote alivyo viainisha hapo havitoi mwanya kwa Rais wala taasisi nyingine kuzuia shughuli za vyama vya siasa kama zilivyoainishwa ktk katiba.
 
Vipengele vyote alivyo viainisha hapo havitoi mwanya kwa Rais wala taasisi nyingine kuzuia shughuli za vyama vya siasa kama zilivyoainishwa ktk katiba.
Ndugu hapa elewa tunaongelea katiba. Kwenye katiba hakuna sehemu iliyoongelea haki ya vyama vya siasa. Isipokuwa haki hizo zipo kwenye katiba kwa ujumla kwenye ibara ya 18 hii hapa

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.


Sasa haki hizo zinakuwa na limitation kulingana na ibara 30(1)
 
Wapi ktk katiba mamlaka hizo zimepata uwezo wa kuzuia shughuli za vyama vya siasa?
Ni mpaka itokee hali ya dharula ambayo ni vita,mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa wakati mmoja na nk.Tena kwa idhini ya bunge ndipo rais wa jamuhuri ataweza kuzuia shughuli za kisiasa na ni kila baada ya miezi 3 ataomba Tena kibali cha bunge .Nakama bunge likiona hamna haja. Basi haruhusiwi kutangaza hali ya hatari.
Kwahiyo hivyo vipengele ulivyotoa havioneshi wapi mamlaka hizo zinapewa uwezo wa kuzuia shughuli za vyama vya siasa.
 
Wewe acha kuongea vitu hewani. Mimi nimeweka vifungu hapo. Hebu weka hivyo vifungu unavyodai kinyume na hicho cha 30.
 
Sijaona sehemu inayoiumbua CHADEMA labda kama mleta hoja anataka kuiweka CHADEMA katika nafasi ya serekali nitamwelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…