tpaul hizi hapa jioneee
Unaona hizo screenshots? Jana nilitaka kununua muda wa maongezi ili nijiunge na kifurushi cha week. Wakanizingua weeeeeee hadi muda ukafika kika expire. Kila nikijaribu kununua inagoma, night ikawa imekubali kununua muda wa maongezi wa buku Tatu unusu, asubuhi najaribu kujiunga wanasema salio halitoshi kucheki wamekula kama buku shilingi Tatu, kwa kipi nilichokifanya sijui....
hahaaaaaaMkuu kama Mimi simu yangu nikijiunga na kifurushi halafu nikaweka buku lina zurura tu kwenye simu kesho nakuta 250 kesho kutwa nakutashillings 0 kabisa.ila siku hiz nimeshtuka nawaachia shillings 5 tu kwenye salio wakakate Mbele ya safari huko.
Vodacom ndio mtandao unao ongoza kwa wizi yani sitaki hata kuwasikia wame niibia sana hawa jamaa mpk line nimeichoma moto kwa hasira.
Hahahaa
Ss umehamia wapi?
Manaake mi hapa ndo nipo mbioni kuhama sema m-pesa inasaidia
Voda wamezidi ni matepeli wakubwa kutumia laini yao ni janga.hawana hata huruma wamekaa kitapeli tapeli.
Hivi mnajua hii mitandao ya simu nchini inakichangia Chama Tawala shs ngapi kwenye Uchaguzi mkuu? Voda ndio partner mkubwa wa CCM.
Mnafikiri hizi Kampuni za simu zitafidia vipi michango mikubwa zinazodaiwa na CCM.?
Mnafikiri TCRA haifahamu huu wizi unaofanywa na hizi Kampuni?
Mkuu usidanganyike kuna jamaa namfahamu anademu wake anapiga kazi voda tena anakitengo kikubwa tu,sasa basi jamaa kila droo za washindi jamaa lazima achukue jamaa ameshawai kupata Hyundai,pesa na droo kama za simu.tena demu wake ndiyo anamuambia "nimekuingiza kwenye droo watakupigia simu" hapo ndiyo nikagundua haa kumbe.
Hongera, naona na wewe ulichukua chako mapema ukajiongeza.
Pili, una maanisha hutumii simu ya mkononi?