Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Mkuu T umeandika ukweli kabisa na zaidi umenigusa hapo kwenye kukatwa kwa dakika wakati simu inahesabu sekunde unapoongea.
Kwa mfano ukampigia mtu, ukaongea kwa dk 1:01, hiyo itahesabika kama dk 2 na utakuwa umeliwa sekunde 59 sawa na dk 1.
Hivyo basi, kama ulipiga simu 8 na zote ulizikatia katika mazingira kama hayo yaani dk kadha na sek 01 hadi tisa hivi, utakuwa umeshakamuliwa dk 8.
Hiyo tabia head master ni voda na second master ni airtel.
 
Mleta mada unaweza kufanya kazi kwenye kampuni ya simu zaidi ya miaka 30 ila usijue chchte kuhusu simu na makato...Inawezekana alikuwa anafanyia H.R or finance !!
 
TTcl je? Maana hao wengine wameoza kila kukicha wanabuni promoshen kumbe ndio tunapigwa pesa zetu
 
Watz kwa kulalamika tu hamjambo. Chukueni hatua pumbav ninyi.
umenena kaka...Mara utaskia ooh voda walaaniwe,ooh tigo walaaniwe hawapendi kuchukua hatua mbulula hawa; tutaendelea kuwaibia mpaka watie akili.
 
Watz kwa kulalamika tu hamjambo. Chukueni hatua pumbav ninyi.
umenena kaka...Mara utaskia ooh voda walaaniwe,ooh tigo walaaniwe hawapendi kuchukua hatua mbulula hawa; tutaendelea kuwaibia mpaka watie akili pumbav zao
 
juzi jumamosi nilikopa voda tsh 650 ilipofika jioni nikachukua buku vocha nikalipa deni lao tsh 750 nikabaki na tsh 250, nikaongeza jero nyingine ikawa 750.. jumapili nikaenda ibada (nilizima simu) ile natoka nikasema ninunue kifurushi naambiwa salio halitoshi! kucheki nina tsh 376.00
 

hata mimi nilishashiriki kuiba 'my apology',,,but nilitumwa....mkono kwa kinywa......
 
hata mimi nilishashiriki kuiba 'my apology',,,but nilitumwa....mkono kwa kinywa......

umeona eeh? mkuu nzalendo hebu funguka zaidi ili wananchi wapate elimu kuhusu huu UWIZI.
 
Last edited by a moderator:

mkuu fake ID, UNAIBIWA! chukua tahadhari...sim banking ni huduma ya kulipia...kila mwezi unakatwa service charges.
 
Last edited by a moderator:
Aisee mleta uzi huu umetusaidia sana kujua yani kungekua na zawadi tungekupa asee maana hii mitandao wamezidi wizi sana
 
Jamani tige na Veda ni wezi sana sometimes wanakuunganisha na Huduma ambayo ukiingiza vocha wanalima hela ukiwapigia wanazingua ndio maana nimehamia SMART
 

Mkuu nimewahi kukwaruzana na washauri wa tigo kutokana na wizi uliofanywa wa kunichukulia salio langu bila hata kujua. Nilikuwa na uhakika kabisa tena100% nimeweka salio shs1000/= cha ajabu nataka kutuma sms naambiwa salio halitoshelezi!!

Napiga huduma kwa wateja najibiwa upuuzi mtupu, eti ooh salio lako linaonekana limeshatumika, aisee jamaa walinikwaza mno.

Ubarikiwe kwa uzi huu, naona moderators wameufanya sticky!!
 
Pia kuna hizi huduma za bila kikomo pia ni wizi mtupu utakuta mtu unajiunga na kifuushi cha MB mfano wajanja night unaambiwa peruzi mtandaoni bila kikomo kwa saa 24 kumbe wanakupa GB 1 tu ikiisha basi
 
Mleta mada unaweza kufanya kazi kwenye kampuni ya simu zaidi ya miaka 30 ila usijue chchte kuhusu simu na makato...Inawezekana alikuwa anafanyia H.R or finance !!

Mleta mada kafanya miaka10 makampuni tofauti tofauti. Nini miaka30.
 
Ukweli mtupu....

Tigo nafikiri ndo wahuni wakubwa..
mkuu wewe voda huwajui. kwa wizi Voda ni mwisho wa reli sijawahi ona... unajiunga na kifurushi mda huu halafu wanachelewa kukuunganisha... wewe unaanza kutwanga mara simu inakatika unaambiwa hakuna salio. baadae wanakuletea sms wakisema huwezi kuunganishwa na kifurushi kwa kuwa huna salio la kutosha. Voda wangese kuliko... japo na tigo nao wamo
 
Kiukweli kabisa huu ni wizi uliotukuka inamaana TCRA hawajui kiasi kwamba ufisadi huu unatendeka mchana kweupe.Ulichoeleza hapa kinaukweli 100% hii imenikuta mara nyngi.Pengine kupitia haya uliyoyaeleza hapa watajirekebisha.Kweli Tanzania shamba la bibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…