Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!


mkuu, ngoja tu tuendelee kuibiwa. kuna siku nilisikia TCRA wanatetea wizi huu iliniuma sana.
 
Last edited by a moderator:
Hivi mnajua hii mitandao ya simu nchini inakichangia Chama Tawala shs ngapi kwenye Uchaguzi mkuu? Voda ndio partner mkubwa wa CCM.
Mnafikiri hizi Kampuni za simu zitafidia vipi michango mikubwa zinazodaiwa na CCM.?

Mnafikiri TCRA haifahamu huu wizi unaofanywa na hizi Kampuni?
 
Jinsi Vodacom walivyonisumbua kwa takribani miaka mitano(hapo ni baada ya kuhangaika na mitandao mingine pia)...Dawa sasa hivi ninatembea na vocha kwenye wallet tu..nikitaka kutumia ndio ninaweka(natuma sms afu napiga simu) hadi salio liishe.
 
Mkuu kama Mimi simu yangu nikijiunga na kifurushi halafu nikaweka buku lina zurura tu kwenye simu kesho nakuta 250 kesho kutwa nakuta shillings 0 kabisa.ila siku hiz nimeshtuka nawaachia shillings 5 tu kwenye salio wakakate Mbele ya safari huko.

kweli kabisa mkuu, ni bora kuweka vocha 500 maana ukiacha fedha nyingi kwenye simu ndio mwanzo wa kuibiwa.

mimi huwa nanunua vocha nyingi za 500 nakaa nazo na kuziweka tu pale ninapotaka kununua kifurushi.

wakuu, hili ni suluhisho mojawapo ambalo kila mtu anapaswa kulizingatia maana ukitegemea suluhisho la kiufundi kutoka TCRA huwezi kulipata kamwe.kila mtu achukue tahadhari ya fedha zake mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini usi file up case kwa nini ishu?
 
Daaaah kumbe buku yangu ya juzi ndo voda waliifanyia mgawo kwa jinsi hiii......
 
Mleta uzi hebu uambie kuhusu Zantel? Uliwahi kufanya kazi hapo mimi ni mteja lakini sijawahi kukumbana na matatizo yoyote na sitaki kusikia habar za voda wa Tigo nimewaacha kitambo sana

mkuu, na huko airtel mtindo ni huo huo...ni WEZI wakubwa!
 
Ahsante Mkuu kwa kutupa taarifa. Kumbe nilikuwa sahihi kutojiunga kwenye promosheni zao. Ila Mkuu umelea tatizo muda mrefu. Ungetutonya mapema. Miaka kumi mingi sana watanzania tumeumizwa.

Hata usipojiunga unalazimishwa kuingizwa bila kujua huku wakichukua pesa yako bila maelezo yoyote. We jaribu siku angalia salio asubuhi, siku hiyo usipige simu kabisawala kutuma sms, kesho yake angalia salio asubuhi uone halafu wapigie simu (ukibahatika kupokelewa) usikie majibu yao.
 
Niko njiani ngoja nitafanya screen shot ya kilichotokea jana. tpaul i promise kuweka ushahidi wa picha ngoja nitulie maana imenibidi nizime simu moja yenye hio issue ili wasiendelee kunikata pesa

mkuu Elli hebu tuwekee ushahidi hapa. hv ni lini hawa mafisadi watakoma kutunyonya? nchi hii ni shamba la bibi. tunaishi maisha ya baharini...samaki wadogo ni chakula cha samaki wakubwa!
 
Last edited by a moderator:
sio kwamba tcra na wenyewe ndio walewale tu..
 
Last edited by a moderator:

yap hilo likinitokea
 

mkuu hizi michezo za bahati nasibu....washind wanakuwa n wa kweli au n waku tengenezwa....?
 
Ndiye Mungu aliyeumba mbingu na nchi, huyu ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Jina lake ni Jehova! Barikiwa!

Sa mbona umesema ni Israel? Africa je? Europe? America? Other planets?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…