Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Kwa hali hii mi nadhani ile buku kwa mwezi inakatwa bila sisi kujua.
 
hebu soma ujumbe huu wa kitapeli kutoka kampuni moja ya simu hapa nchini:

Ongea BURE Tigo-Tigo saa 24. Jiunge kwa kutuma neno BILA KIKOMO kwenda 15509. Sh 2000 tu

UTAPELI ULIOMO KWENYE UJUMBE HUU:
1. Hiyo bure inakuwaje wakati mteja hukatwa Sh 200 kujiunga? Huu ujumbe unalenga kuonyesha kwamba wateja ni MAJUHA, na hii ni dharau mbaya ambayo makampuni ya simu huionyesha kwa wateja wao.

2.Kuna baadhi ya wateja hawasomi ujumbe hadi mwisho. Akishaona neno BURE hujiunga haraka haraka na hatimaye salio lake kukatwa kinyume cha matarajio na bajeti yake. Huu ni utapeli kama ulivyo utapeli wa aina yoyote ile na hauvumiliki hata kidogo. Hivi nyie matutusa wa TCRA mko wapi wakati masikini wanaibiwa na haya makampuni ya kitapeli?
 
Last edited by a moderator:
shikamoo mtalaamu wa masiliano.je tufanyaje ili tuwe salama na huu wizi?
 
shikamoo mtalaamu wa masiliano.je tufanyaje ili tuwe salama na huu wizi?

Cha muhimu ni kila mtu kuchukua hatua ya kujilinda yeye binafsi, wala tusitegemee mamlaka yoyote ya serikali kutusaidia. Hakikisha kwenye simu yako hubakishi salio....hifadhi fedha kwenye mpesa, tigo pesa au airtel money...ukitaka kununua bundle, nunua airtime halafu jiunge immediately. Pia usijiunge kwenye huduma zozote za kipuuzi zinazokata salio lako.
 

Wewe tpaul umeamua kumwaga hadharani mambo yetu siyo? Basi ngoja sasa tuanze kukutafuta na kukushughulikia ipasavyo. Wewe unadhani sie tumekuja kuwasaidia hao watanzania kupata mawasiliano? Sie tumekuja kuvuna na kuchuma. Tutadeal na wewe sambamba.
 
airtel wamezidi kuna kipindi nalipia internet nikiweka sipati kitu mpaka saa sita usiku kuwafata wakasema haiwezekani nikaweka bando kuweka kujaribu hamna kitu wakashindwa kunisaidia, pia niliwahi kwenda kuwalalamikia tcra kuhusu kukatwa muda wa maongezi wakaniambia niandike barua kuanzia mwezi wa kumi na mbili wakanipigia simu april mwaka unaofuata wakitaka niandike tena barua
vyombo vya habari vinaogopa kuwakosoa ili wasikose matangazo pia kuna waandishi wako kwenye payroll habari yoyote mbaya ya makampuni ya simu haiandikwi natamani tungekuwa na rais kama Kagame ambaye aliyapiga faini makampuni ya simu kwa kufanya uzembe
 
HAWA WEZI WAMEANZA TENA! TAZAMA JINSI VODACOM WALIVYOPUNGUZA UKUBWA WA BUNDLE BILA KUWATAARIFU WATEJA WAO:

Send:1

Receive:1. Tsh1500=1GB (MPYA)


2. Tsh1000=500MB
3. Tsh500=150MB
4. Tsh300=50MB
5. Tsh200=10MB

HIVI HAWA TCRA WANAKUWA WAPI WAKATI WANANCHI TUNAVYODHURUMIWA HIVI NA HAWA MAKABURU?
 
Asante mkuu kwa habari za ndani. Tatizo kubwa ni vyombo husika vya dola vinavyotakiwa kuona wananchi au wateja hawatapeliwi na hawa wezi. Inawezekana vyombo hivi haviwajibiki au havina uwezo wa kuangalia haya au wamekwa mfukoni na wanafanya hawaoni
 
Tena nyongeza,ni wasenge sana hawa airtel ,mie wamenichosha nikiweka pesa kesho yake siikuti ,nimeona bora nihame ,nipo halotel mtandao wa kijanja unaotenda haki,
 
Ngoja nikamueleze bosi wako kuwa umekuja kumuanika humu Jf..!!
 
Hili nalo limenikuta hivi karibuni
 
Haya yote mimi nimeyashudia binafsi.Nilidhani ni matatizo genuine kumbe ni wizi,ila nilisha-smell a rat.Hata hivyo kama TCRA sio collaborators kama ninavyohisi ,wanaweza kutusaidia mkuu.
Mengi ya unayo yasema kwangu binafsi nimeyaona kitambo ila hayakwepeki , TCRA wana titazama tu tukinyonywa.mfano wa kutotoa taarifa pindi kifurushi kikuishiapo katikati ya matumizi, na makato yasio na taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…