Jinsi hacking ilivyonipa 250,000 tshs leo!!!!!!!!!

Jinsi hacking ilivyonipa 250,000 tshs leo!!!!!!!!!

mkuu,login kwenye hii site: HackThisSite.org, ukiweza kwel we mkabe
 
Huyu Jamaa sijaona alipojisifia,Zaidi ya Ku'inspire Ma'hackers wengine wa kibongo na kustua wanajiita Ma'security Officer wa IT hapa Bongo. Ni Sawa na Diamond kupost picha Instagram ndani ya Private Jet Trip
 
Sijapata kuona unamhack mtu alafu unamfuata. Ila asante kwa kuongeza siku zangu za kuishi. Ila kumbuka hacker ni muharifu kama waharifu wengine. Unafanya uharifu alafu unakuja jukwaani kujisifu jela inakwita.
 
sijapata kuona unamhack mtu alafu unamfuata. Ila asante kwa kuongeza siku zangu za kuishi. Ila kumbuka hacker ni muharifu kama waharifu wengine. Unafanya uharifu alafu unakuja jukwaani kujisifu jela inakwita.
.
Sio wote....
.
.
 
So how do I start / get training on becoming a hacker?
 
Ni majuzi juzi tu nlianzisha thread kwamba inabidi tanzania tujiupgade kwenye techs kwa njia ya kuhack, well nkapost topic inayohusu site ndogo tu nliyohack hata sekunde kumi hazijapita thread ikafutwa , nkakaa mezani nkafikiria hivi nikipata loopholes kwenye site za tz na nkienda kuziripoti itakua dili , mzee mzima nkaingia mzigoni na brand new kali linux nkaanza kusearch loopholes na kujaribu kuziexploit nikazinotedown fasta fast nkang'oka mbio kwenda ofisi husika ya shirika nliloweza kupata matundu, mwanzoni nmefika pale secretary ndo kwanza hata hajui maana ya kuhack bahat nzuri mkubwa flan akasikia then akanifata nlienda na laptop yangu na nkamwonyesha jinsi itavyokuwa wasipoziba sio siri alikua surprised akapiga simu kwa kijana wake wa i.t akaja mbio kuhakiki maana alikua ni mbishi mno kafika pale nae anatoa macho tu ndo kwanza hata kali haijui well tukafix mambo palepale nkapelekwa ofisi zao za uhasibu chap chap nkapewa kitita cha laki 2 nae jamaa wa i.t akaniita palepale akanipa 50 jumla ikawa 250 k na kiukweli nilifurahi sana maana nimefumbuliwa macho kuwa kipaji changu cha kuhack kinaweza kuwa bonge la dili
Hongera kwa hizo pesa ulizopata,kuhusu "thread yako ya hacking" kuondolewa walichofanya ni sahihi kwani forum nyingi huwa hawaruhusu topic zinazofundisha hacking.Unaweza ukafundisha kwa nia njema ila watu wakatumia vibaya.
Kuna software ulizitaja last time za kuingia bila password,nilishawahi kuzitumia si vizuri akiweza kuzitumia mtu mwenye nia mabaya kumbuka kuna wengine hawazijui unapozifundisha ,una uhakika gani hawatatumia vibaya?
Kwa hiyo usijisikie vibaya thread yako kutolewa,pia nataka nikutahadharishe hicho ulichofanya kwa kali linux,si unajua ni kosa kisheria?Doing penetration/vulnerability test without the permission of the system owner?
Kama unafuatilia security issue unatakiwa ujue otherwise kuna wengine utaenda badala ya pesa wataita security.
I am just giving you my suggestions,software hizi ukiweza kuzitumia tafuta njia nzuri ya kumake money with them,unabahati hapo ulipoenda inaonekana they know nothing about security issues.
Nakushauri uwe unaenda kama mtu wa kufanya say "Security audit" au "penetration test" waki kupa kazi then,unaonyesha uwezo wako.Remember it is important you get permission to do so.
 
Back
Top Bottom