Script kiddie ni watu ambao kiuwezo hawajawa ma-programmer wa kuweza kutengeneza software zao wenyewe kwa ajili ya hacking, ila wao hutegemea sana software kutoka kwa proffesional programmer wanaotengeneza software kwa ajili ya hacking, mfano wanaweza wakatengeneza software fulani kwa ajili ya kupiga simu pasipo malipo, wewe ambaye hujahusika kutengeneza unaweza ukaitumia kukwepa kulipia gharama za simu, kumbuka hapa wewe utakuwa hacker lakini utaitwa script kiddie hacker kwa sababu huelewi hiyo software imetengenezwaje (program codes) zaidi ya kuitumia
Mkuu ukiachana na hawa wanaojiita black hacker na white hacker, wapo wanaojiita kwa majina yao mengi tu na kila mmoja ana lengo lake, hawa wanaojiita back hacker (black hat) wao kazi yao kubwa ni kuharibu security system kwa manufaa yao wanayoyajua wao pindi wanapotaka kufanya hacking i.e wanapofanya hacking kwako mwisho wanataka wafaidike na nini!?. Na mara nyingi hawa ndio crackers
Kuhusu white hacker (white hat) hawa wao huwa wanafanya hacking ya security system kwa ajili ya kupima uwezo wa hiyo security system, mfano unaweza kutengeneza software yako yenye security system ili kuilinda watu fulani wasiweze ku-access vitu fulani pasipo na ruhusa yako, sasa ili kupima uwezo wa hiyo security yako unawaita hao jamaa ili waweze kuifanyia hacking ili uweze kujua mapungufu ya security system yako, hii mara nyingi huwa inaitwa ethical hacking
Niishie hapa ila kama kutakuwa na wadau wengine wataongezea wanachojua wao