jinsi gani ya kumuandaa marehemu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jinsi gani ya kumuandaa marehemu?

Discussion in 'JF Doctor' started by Kimbori, Oct 18, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwanza niombe samahani kwa yeyote atakayekwazika na yalioandikwa au yatakayoandikwa kuhusiana na thread hii.
  Nimekuwa nikisikia lawama zikitolewa kwa msimamizi wa mgonjwa pindi mgonjwa anapofariki na kutofunga macho, kufunga mdomo, n.k, binafsi yangu sijui jinsi ya kukabiliana na changamoto hozi ikiwa kama zitanitokea. Elimu kama hii haipo kwa wengi kutokana labda na ukubwa wa tatizo.
  Elimu ni muhimu hata kama itauma, kukumbusha au kusababisha machungu kwa baadhi ya watu. Naomba kuwakilisha.
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,347
  Likes Received: 2,984
  Trophy Points: 280
  Pamoja mkuu,acha ningoje majibu pembeni.
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  We ni muumini wa dini gani? kwa waislamu nadhani kuna sheria zake na taratibu zake! Wanazuoni tunaomba msaada hapa. kwa madhehebu/dini zingine sijui, ila kwa katoliki kila mmoja anafanya anavyopenda. hakuna sheria. nadhani kufumba mdomo/macho ni kuwa maiti asionekane vibaya wakati wa kutoa heshima za mwisho, nothing else!
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Japokuwa mimi ni Mkristo, ninachoomba ni elimu ya wanazuoni, hususani kuhusiana na ile huduma inayotolewa muda mfupi baada ya mtu kufariki ili kuhakikisha viungo vinakaa sawa.
   
 5. awp

  awp JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  jamani kila kitu siku hizi dini
   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  yakikukuta utajua hapo hapo cha kufanya, mambo mengine huhitaji course wala practice! ni kama kumtoa mtu bikira au hainaga course wala mafunzo, ni kwamba siku ikifika, utajikuta unaweza na bikra itatoka.!!! nawasilisha!!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mie nadhani Kama unakaa karibia na manesi na madr wanaweza kukupa majibu yote
  Kwani wao wamekuwa wanakutana na mambo haya kila mala
  mara mgonjwa anapofariki ni hatua gani za kuchukua mapema .
   
 8. W

  Wakwetu Senior Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si ukae kimya kama huna la kuchangia? bikira na maiti wapi na wapi?
   
 9. W

  Wakwetu Senior Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cacico si ukae kimya kama huna la kuchangia? bikira na maiti wapi na wapi?
   
 10. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  mkuu mleta mada hapa si mahala pake! leta hoja endelevu sio hoja mfu kama hizi halafu unataka madokta tukusaidie, haya ukishamfunga maiti macho na mdomo? so what? acha mambo ya kuwaza waza vifo kama mchawi, i -tune akili yako ifikirie vitu vya maendeleo!!
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kimbori kwa waislam ni hivi

  HUKUMU ZA KUMWOSHA MAITI

  Ni fardhi juu ya kila Mwislamu kumwosha maiti huyo, na kutengeneza mazishi yake yote, lakini wakishajitokeza watu kumshughulikia huyo maiti basi kwa wengine fardhi hiyo huondoka.

  1. Ni haramu mwanamke kuoshwa na mwanamume, au mwanamume kuoshwa na mwanamke, lakini mke ana weza kumwosha mume hata kama wapo wanaume, na mume anaweza kumwosha mke hata ikiwa wapo wanawake wa kumwosha.
  2. Mwanamume anaweza kumwosha mtoto wa kike asiyezidi miaka mitatu, na pia mwanamke anaruhusiwa kumwosha mtoto wa kiume asiyezidi miaka mitatu.
  3. Ikiwa hakuna mwanamume wa kumwosha mwanamume, wanawake walio karibu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha, kama mama, dada, shangazi, mama mdogo (dada wa mama yake). Vivyo hivyo ikiwa maiti mwanamke na hakuna mwanamke wa kumwosha huyo maiti, basi majamaa waliokaribu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha kama baba, ndugu, na mtoto wake na wale ambawo ni haramu kumuoa, kwa kisheria wanaitwa "MAH-RAM".
  4. Mtoto aliyezaliwa kwa kuharibika mimba, ikiwa mimba iko chini ya miezi minne (bado hakukamilishwa umbo lake) huyu hana haja ya kuogeshwa (kumuosha GHUSLI), ni lazima aviringishwe katika kitambaa na akazikwe. Lakini mimba ya miezi minne au zaidi (aliyekamilika umbo lake), lazima aogeshwe na kuvikwa sanda kama desturi.
  5. Mwenye kumwosha maiti lazima awe mwislamu, tena Shia, na awe amebalehe, mwenye akili, na ajue namna ya kumwosha maiti.
  6. Ni fardhi kumwosha Mwislamu hata akiwa wa madhehebu nyingine, lakini utamwosha kwa mujibu ya Madhehebu ya Shia lthnaasharia tu.
  7. Mwosha maiti anapomwosha maiti anuwie kama ninafanya kazi hii Qurbatan llal-Laahi Taala, na vitu vyote avitumiavyo kwa kumwosha maiti viwe vya halali, si vya kunyang'anya au kuiba hata maji na mahala atumiapo wakati wa kumwosha maiti pawe pa halali.

  SUNNA ZA KUMWOSHA MAITI


  1. Awekwe mahala palipo juu, kama kitanda, au baraza n.k. na mahala pa kuwekea kichwa chake painuke zaidi kuliko miguu.
  2. Alazwe chali, miguu na nyayo zielekee Qibla (kama tulivyotaja katika mambo ya hali ya 'IHTIDHARI'.
  3. Maiti avuliwe nguo zote kwa upande wa chini (miguuni) hata ikibidi itatuliwe (ichanwe) lakini kwa idhini ya warithi wa maiti.
  4. Aoshwe chini ya sakafu, au banda au hema asioshwe chini ya mbingu.
  5. Uchimbwe "UFUO" wa kuingia maji ya kuoshea.
  6. Mwili wake wote uwe wazi isipokuwa utupu wake.
  7. Ufunikwe utupu wake hata ikiwa mkoshaji au watu wanaomuosha ni miongoni mwa wale wanaoruhusiwa kumwangalia.
  8. Mkoshaji apitishe mkono wake juu ya tumbo la maiti kwa taratibu lakini ikiwa maiti mwenye mimba ambaye mtoto pia amekufa tumboni hairuhusiwi kufanya hivyo.
  9. Mkoshaji asimame upande wa kulia wa maiti.
  10. Aanze kuosha upande wa kulia wa kichwa cha maiti.
  11. Mkoshaji aoshe mikono yake mara tatu hadi begani kwa kila 'GHUSLI' tatu.
  12. Mwoshaji anapokuwa anaosha kiwiliwili cha maiti anatakiwa aseme hivi: "Ewe Mola! Hiki ni kiwiliwili cha mja wako mwenye imani (Mumin) na umetoa roho yake kutoka kiwiliwili chake, na umetenga kati yao, basi msamehe kwako." Hasa wakati anapomgeuza.
  13. Asitangaze mwoshaji aibu yoyote aliyoiona mwini mwa maiti.


  UTARATIBU WA KUMWOSHA MAlTI

  (a) Baada ya kusafishwa mwili wake wote kwa sabuni (au kitu kingine) na kuondoshwa uchafu wa aina yo yote kama (madawa, marhamu au mafuta) ndipo huyo mwoshaji Mwislamu atamwosha ghusli tatu (mara tatu kuoshwa). Ni sunna kabla ya kuanza kumwogesha maiti ghusli tatu, atamwosha mikono yake mara tatu, kwa kila ghusli.

  (b) Kwa mara ya kwanza, atachanganya katika maji ya kumwoshea maiti kidogo SIDRI (majani ya mkunazi) kwa kutia katika pipa la maji anachochotea maji ya kumwoshea huyo maiti (atayafikicha yale majani yapate kutoa harufu), wala asitie majani mengi hata maji yawe mudhafu. Baada ya kumaliza ghusli ya kwanza atakisuza kile chombo (pipa) kuondoa harufu ya Sidri.

  (c) Na kwa mara ya pili atamwosha kwa maji yaliyochanganishwa na 'Kaafuri' (Karafu maiti) kidogo tu, wala asitie nyingi hata maji yakawa mudhafu. Tena atasuza pipa baada ya kumaliza ghusli ya pili ili kuondoa harufu ya Kaafuri.

  (d) Na kwa mara ya tatu atamwosha (ghusli) kwa maji haya ya kawaida yaliyo safi bila ya kuchanganywa na cho chote, na hii ndio mara ya mwisho. Ni sunna mwoshaji katika muda anapomwosha maiti awe anasoma, "AFWAN AFWAN".

  HADHARI: Taratibu zote za kuosha ni lazima zifuatwe na kama si hivyo GHUSLI ya maiti hubatilika na ni lazima uanze upya kwa utaratibu ule ule tuliyoueleza.

  Kwa hivyo huyo maiti wa Ki-Islamu baada ya kuoshwa ghusli tatu hizo kama tulivyoeleza, sasa atakuwa ametaharika, Mwislamu yo yote akimgusa wakati huu, hakuna haja ya kuoga kwa yule mwenye kumgusa, lakini

  ikiwa baada ya kutoka roho na kupoa mwili, na kabla hajapewa (maiti) hizo ghusli tatu, akimgusa tu kwa mwili (si juu ya nguo) basi kwa kila mwenye kumgusa ni fardhi juu yake aoge "ghusli massul Mayyit", (ghusli ya kumgusa maiti). Na ghusli (kuoga) hiyo ni faradhi kwa mujibu wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) tu.


  NAMNA YA KUMWOSHA MAITI

  Baada ya kusafishwa mwili wote wa yule maiti hapo (yule mwoshaji) atanuia kuwa, namwosha (huyu maiti) ghusli ya kwanza kwa maji yaliyochanganyishwa na majani ya mkunazi kama tulivyoeleza huko nyuma.

  (a) Kwanza ataanzia kwa kummwagia maji kichwani (maji yafike hadi utosini kwenye ngozi) masikio, pua, mdomo, macho na shingo pia aoshe. Ahakikishe kilmara anapomwosha, maji yafike sehemu zote za mwili wake.

  (b) Tena upande wa mbele wa kulia kutoka begani chini ya shingo na pote kulia hadi kwenye nyayo tena baadaye amlaze ubavu amwoshe sehemu ya nyuma kama alivyomwosha sehemu ya mbele ya kulia.

  (c) Baadaye atamwosha upande wa mbele wa kushoto na baadaye upande wa nyuma kama alivyomwosha upande wa kulia.

  (d) Utupu wa maiti lazima uoshwe anapokoshwa kila upande (maana yake kwa kila mwosho (ghusli) ataosha utupu mara mbili). Ni haramu kuangalia utupu wa maiti na mwoshaji akiangalia ametenda dhambi, lakini ile ghusli haibatiliki.

  (e) Mwoshaji wakati anapoosha utupu wa maiti Iazima aviringe kitambaa au avae mfuko wa kitambaa mkononi, ni haramu kupeleka mkono upekee.

  Hii ndio namna ya kumwosha maiti ambayo utaratib huo kwa kisheria unaitwa "ALGHUSL AT-TAR-TIBI" na inambidi kwa kila mwenye Janaba pia akitaka kuondo (kuoga) Janaba au mwanamke mwenye hedhi au nifasi au kuoga ghusli za sunna lazima waoge vivyo hivyo kama tulivyoeleza katika kitabu chetu cha Sala (mlango wa ukurasa wa 33).

  Kwa kuoshwa ghusli tatu hizo, tena haina haja kumwogesha, ghusli ya janaba au hedhi au nifas ikiwa maiti alikuwa katika hali ile.

  Ikiwa SIDRI (majani ya mkunazi) au KAA-FUR (Kafuri maiti) zote mbili au mojawapo haipatikani, basi maiti ataoshwa kwa maji haya ya kawaida kwa nia ya badala ya Sidri au Kafuri mradi lazima maiti aoshwe Ghusli tatu tu (mara tatu).

  (a) Ikiwa maji hayapatikani au maiti ameungua au alikuwa na maradhi fulani na akitiwa maji nyama au ngozi itatoka, basi badala ya maji atafanyiwa Tayamamu mara tatu kwa Ghusli tatu.

  (b) Tayamamu ni lazima ifanywe na yule hai, na kumpaka maiti, na kama inamkinika kutayamamu kwa mikono ya maiti pia ifanywe - (Namna ya Tayamamu angalia kitabu chetu cha 'Sala' ukurasa wa 44 Mlango wa 8).  MAMBO YA FARADHI BAADA YA KUOGESHWA MAITI HADI KUZIKWA KWAKE

  Haifai wakati anapooshwa maiti kuweko moto au kiteso cha kufukiza wala wakati wa mazishi hadi mwisho.

  AL-HUNUUT
  : Kupakwa maiti kafuri mahali maalum ni faradhi kwa Waislamu baada ya kumwosha na

  kupanguswa (afutwe vizuri kwa nguo kavu) maiti kabla ya kusaliwa na kuzikwa apakwe 'Kafuri' laini sehemu

  saba (viongo vya kusujudia) navyo ni kipaji, viganja viwili, magoti mawili, ncha za vidole gumba viwili. Na sunna

  kupakwa kwenye pua, vile vile sunna kuwekwa pamba kwenye utupu wa maiti na kila penye tundu. Wakati wa

  kupaka HUNUUT ni baada ya kuogeshwa na kupanguswa na kabla ya kuvikwa sanda au wakati wa kuvikwa sanda.

  Ikiwa Kafuuri haikupatikana hatakumwoshea maiti, basi hapo faradhi ya HUNUUT inaondoka, na kama amekogeshwa na Kafuuri lakini haikuzidi kwa ajili ya HUNUUT basi si kitu.

  AL-HUNUUT
  : Kupakwa maiti Kafuri ni faradhi kwa kila maiti mdogo, mkubwa mwanamke, mwanamume, huru

  au mtumwa isipokuwa maiti yule aliyekufa hali yuko katika Ihramuni haramu kumpaka Kafuri. Kafuri lazima iwe

  mpya si kukuu yenye kupotea harufu yake, na pia lazima iwe laini iliosagwa.

  SANDA YA MAITI ILIYO WAJIBU

  Ni faradhi kuvishwa maiti mwanamume au mwanamke mkubwa au mdogo vipande vitabu vya nguo:

  (1) Kanzu (2) Shuka (3) Shuka

  (1) Kanzu: Bila kuishona, itobolewe sehemu ya shingo tu halafu kitumbukizwe kichwa. Kuanzia begani hadi nusu ya miguu kupita goti.

  (2) Shuka:Kama anavyovaa mwanamume kutoka kitovuni
  hadi magotini, na ni bora si wajibu kuanzia kifuani hadi chini ya magoti.

  (3) Shuka:Kitambaa kikubwa cha kumfunika mwiIi wake wote mzima mbele na nyuma kwa urefu hata uweze kufunga pande zote mbili (upande wa kichwa na upande wa miguu) na kwa upana, ncha moja iweze kuja juu ya ncha va pili

  SUNNA: Si wajibu bali ni sunna (a) Kuvishwa mwanamume kiIemba, mwanamke sidiria na ushungi (b) Nguo nyeupe isiyokuwa na rangi yoyote (c) Nguo iwe ya pamba (d) Ni bora kama aliwahi kuhiji basi 'IHRAMU' itumiwe au nguo za kusalia ambazo akisali nazo.

  SANDA: Kwa kiasi kilichofaradhi lazima gharama yake na gharama ya vitu vya kumwoshea maiti, maji, Sidri, Kafuri, ardhi pa kuzikiwa na gharama zake zote haya hutoka katika asili ya mali ya maiti kabIa ya kulipwa deni

  au kufuatwa wasia wake. Na yako mambo ya sunna katika sanda ikiwa ameusia sanda itolewe katika theluthi (1/3) ya mali yake, au ameusia theluthi ya mali atumiliwe yeye basi sanda itatolewa humo, na kama hakuusia

  theluthi (1/3) basi kiasi kilichowajibu kitatolewa katika asili mali.

  Sanda ya mke juu ya mumewe hata ikiwa mke anayo mali ya kutosha, na vivyo hivyo yule mke aliyeachwa kwa

  mara ya kwanza au ya pili na bado yupo katika eda, mume lazima atoe sanda. Ikiwa mtu mwingine yoyote

  ametoa sanda ya yule maiti (mwanamke) basi faradhi humuondokea mume.

  Ni sunna kwa kila mwislamu kutayarisha SANDA yake na kuiweka nyumbani, pia ni sunna kuiangalia hiyo sanda

  kila mara. Mtukufu ,Mtume (s.a.w.) amesema, "Mwenye kutayarisha sanda yake, huwa kila siku zipitazo kila

  huandikwa thawabu kila apoiangalia, na kwa kufanya hivyo hatahesabiwa miongoni mwa waliomsahau Mwenyezi Mungu.


  NAMNA YA KUMKAFINI (KUMVISHA SANDA MAITI)

  Baada ya kukatwa mapande hayo, kwanza utatandika ile shuka kubwa ya Namba 3: Na ndio ya kwanza, baadaye utatandika Kanzu Kanzu kwa kuikunjua upande mmoja, (na hii ni ya pili), baadaye utaliweka shuka

  kwa upana kwa kukunjua. Ukisha tandika yote hayo vipande vitatu vya vitambaa vilivyo wajibu, basi sasa atalazwa maiti juu ya mapande yote ya sanda.

  1. Kwanza utamfunga shuka na kuondoa kile kitambaa ulichotumia wakati wa kumwoshea kuficha utupu wake.
  2. Utaurejesha ule upande wa kanzu ulioukunjua kwa kupitisha kichwa cha maiti kwenye shingo.
  3. Ikiwa umeshafanya mambo ya 'AL-HUNUUT' basi utaikunja hiyo shuka kubwa kwa kuiweka ncha moja juu ya pili, na kama bado hujampaka AL-HUNUUT na mambo yake basi fanya, ndipo umalize kumfunika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,744
  Likes Received: 8,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu MziziMkavu ushukuriwe kwa hilo lkn nafikiri muanzisha mada ameuliza swali tofauti kidogo na maelezo yako.

  Kama nimemuelewa vyema anataka kujua nini afanye ikiwa binaadamu amekata roho mbele yake. Yawezekana amekufa kwa maumivu kwa hiyo ametoa macho, au amejitupa mikono huko na kule na kwa kawaida ya maiti atakakamaa akiwa katika hali hiyo. Nafikiri anataka ajue namna ya kumfummba macho, kumweka kwenye orientation nzuri mwili wake n.k
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwana Mtoka Pabaya anakufa mtu inatakikana marehemu afunikwe shuka nyeupe au shuka yoyote ile afunikwe macho yake anyoshwe mwili wake uwe umenyooka sio kujikunja na awe na watu wake wa karibu pamoja nae kwenye chumba cha maiti .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. S

  Smarty JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  asante sana mzizi mkavu kwa hii darasa..
   
 15. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2017
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
   
 16. Ngozi Joram

  Ngozi Joram JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2017
  Joined: Sep 9, 2016
  Messages: 587
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 80
  Bro mbona sioni tatizo lolote kwenye post hii?? Ww sema kweli tu mwoga!! Ukisikia habari za kifo hulali
   
 17. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2017
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  Kila nafsi itaonja Mauti. Haya matamko huku duniani ni mbwembwe tu
   
Loading...