Jinsi gani naweza kusoma Open University?

Jinsi gani naweza kusoma Open University?

O'level cheti kiko poa, Cheti changu Cha form VI ndo kiko hovyo ndo nayotaka ku_reseat, sitaki diploma wala certificate maana nilisoma diploma zile za NECTA kifupi hata sikukaa chuoni kusoma kusoma bali nilienda tu kufanya mtihani nikahitimu badae nikaajiriwa shida GPA nlopata ni 2.2 Sasa kwa hiyo GPA unajiendelezaje?
Mkuu unasifazote za kupiga foundation...Nenda open kapige foundation course ukitusua unapiga zako bachelor ni 1 yr tu
 
kama elimu yako ni form four haina shida mkuu.
pale kuna course inaitwa foundation. hii itakufanya uwe na sifa za kusoma degree ukimaliza na kufaulu
course hii inasomwa na wale ambao hawajamaliza form 5-6.
sisi mfumo wetu wa kujiunga na vyuo vikuu unataka lazima umalize form 5-6 ndiyo maana ni vigumu hata kwa wanafunzi kutoka nchi nyingine zisizo na hiyo mifumo
asante

Recently kuna some admission changes made by OUT
Nina ndugu yangu aliharibu form 4 akaunga unga akapata certificate then diploma kutoka govt college
Later alipoenda Open alinyimwa admission kutokana matokeo mabovu ya O-Level. Imagine hata option ya kufanya foundation course for a year haikukubalika japo ana Diploma.

Ushauri wangu ni huu…tafadhali nenda center yoyote ya OUT na ongea na wahusika watakueleza namna unaweza soma zaidi.
Ikishindikana ingia online na wapigie simu upate ufafanuzi

Kila la kheri
 
Kabla ya kuanza kozi itakupasa uwe na android ama pc ukiwa na pc ni vzr zaid maana itakusaidia pia kuandika assigment ama kwenye course ya ICT.

Pili unaweza kujiunga kwa online kupitia website yao ame kwenda tawi lolote la open ulilokaribu nalo ili ufanye usajili. Open kunakuwa na intake ya aprili na november....kuna kipind zilikuwa intake nne lkn kwasasa naona hzo mbili ndio zinafanya vzr

Tatu kufanikiwa kujinga na kulipa ada kulingana na maelezekezo utakayopewa kipindi cha orientation utafunguliwa account mbili kwenye website yao..
Moja itatumika kuweka taarifazako za academic malipo nk
Yapili itatumika kwa ajili ya online lecture mtakazo kuwa mkifundishwa...

Kuhusu mitihani
Open kuna vipind 4 vya kufanya mitihani
February,april, june, sept/ november,
Mwanafunzi utachagua ufanye lini mtihani kulingana na ulivyojiandaa

Lkn pia itakupasa kufanya online test au assigment ama pen and paper test ambzo znachukua 30% na annual exam 70%
Jumla ya matokeo yako yatachangiwa na 30% ya test na 70% ya annual. Pia hutaweza kufanya annual exam km hujafanya test.
Kumbuka open pia kuna kusap na kudisco pia

Chuo hiki kinatambulika na NACTE pamoja na TCU na nichuo cha serikali

Hao ni machache kwa ufupi
Mkuu umeeleza vyema sana hapa. Umeweka vitu clear kabisa.
Emb ngoja na mie nkasome bachelor nyingine ya uhasibu, daah, nmechoka kupiga chaki aisee. Hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama elimu yako ni form four haina shida mkuu.
pale kuna course inaitwa foundation. hii itakufanya uwe na sifa za kusoma degree ukimaliza na kufaulu
course hii inasomwa na wale ambao hawajamaliza form 5-6.
sisi mfumo wetu wa kujiunga na vyuo vikuu unataka lazima umalize form 5-6 ndiyo maana ni vigumu hata kwa wanafunzi kutoka nchi nyingine zisizo na hiyo mifumo
asante
Kaka no hv hiyo foundation aneyesoma ni yule aliyemaliza form six mwenye kuanzia matokeo ya III ya 14( Three ya kumi na nne )
Yaaan matokeo yake haya mwezeshi kwenda kusoma degree moja Kwa moja
NA SIO MTU ALIYEMALIZA FORM FOUR
 
kama elimu yako ni form four haina shida mkuu.
pale kuna course inaitwa foundation. hii itakufanya uwe na sifa za kusoma degree ukimaliza na kufaulu
course hii inasomwa na wale ambao hawajamaliza form 5-6.
sisi mfumo wetu wa kujiunga na vyuo vikuu unataka lazima umalize form 5-6 ndiyo maana ni vigumu hata kwa wanafunzi kutoka nchi nyingine zisizo na hiyo mifumo
asante
Si kweli kiongozi,hiyo foundation program haiwahusu wanafunzi wenye elimu ya kidato cha 4,inawahusu wanafunzi wenye elimu ya kidato cha sita,wenye principle pass moja na subsidiary,ambao hawawezi kusoma degree moja kwa moja,na wanafunzi waliosoma diploma wenye GPA below 2.9,ambao hawawezi kupata udahili moja kwa moja kusoma degree! Makundi hayo mawili tu ndo yanayoweza kusoma hiyo foundation program,huyo wa form four aanze na cheti then diploma,kama atapata GPA 3.0-5.0,atapata fursa ya kusoma degree moja kwa moja,kama atapata GPA ya 2.9 kushuka chini itambidi asome sasa hiyo foundation program.
 
Back
Top Bottom