Jinsi Card ya harusi ilivyovunja urafiki wetu

Ba Razaack

Member
Jun 15, 2020
31
41
Habara wana JF, hope mpo poa.

Ilikuwa mwaka 2016 rafiki yangu anaefanya kazi Jiji la Dodoma wilaya ya Kongwa alinitumia card ya harusi akiniomba kumpa support kwenye harusi yake kama ilivyo desturi ya Waungwana nilimsaidia huo mchango na kufanikisha hiyo harusi.

Miaka miwili mbele yaani 2018 nami nikawa na Mchakato wa kufanya harusi, kama ilivyo desturi zetu unapokuwa na jambo la kheri unashirikisha watu niliamua kumshirikisha Pia rafiki yangu wa Dodoma_Kongwa kwa kutumia card ya Mchango wa harusi.

Duuuuu! Tenda wema uende zako toka siku nimemtumia card hiyo hajawahi kupokea simu yangu wala kujibu SMS yangu ni miaka miwili sasa toka nimeoa.

Bado natafakari ni card ya mchango tu ilitutenganisha au kuna kitu kingine.

Natua peni chini.
 
Ukitaka kuoa bora tu utaute pesa mjichange wewe na ndugu mfanye harusi halafu watu waje tu kufurahia pamoja nawe. Haya masuala ya harusi kuchanga sana wengine wanakupa kadi kama wanakudai. Mimi suala la michango ya harusi nishaweka pembeni maana michango mingi utakuta inaanzia 50,000 kwa mwezi unaokea kadi hata 6, mweeeh si ntafilisika na hiki kipato cha ba Jesca.

Katika maisha yangu niliwahi kuchangia harusi 3 tu, moja ya rafiki yangu mkubwa harusi yake hakuchangisha walichangia ndugu na yeye poa, mimi niliamua tu kuchangia na nilichangia kiasi kikubwa sana kwa mapenzi yangu tu.

Zilizobaki za watu wangu wa karibu na baada ya hapo sichangii harusi labda msiba na wagonjwa. Nikitaka kuoa sitochangisha nikishindwa, tunafunga ndoa ya kawaida, halafu familia tunakutana dinner kwisha habari yake. Bi harusi kama hataki aende zake
 
Wee mchawi km siyo mchawi utakuwa mchawi huyo rafiki ako aliangalia sura yako ya moyoni haipo.
Ulitoa ili ulipwe baadae lkn siyo kwa moyo wa dhati. Unajuaje km simu iliibiwa? Ilipotea au iko kwa fundi?

Wewe ndo mbaya unastahili zaidi ya hayo. Well rafiki Hajibu nenda physically.

anaweza asiwe na hela by that time mwambie ahudhurie tu.sababu ya urafiki au vipi mripie!!

Hujui anaumwa au mwenza wake anaumwa au ndo kamzuia. Au kapiga ramli asiudhurie.hata wewe huenda ingekusaidia.

Au labda alidhani unataka ulipwe au alituma kakosea number na hapohapo simu ikapotea.
Au nae anakupima upendo wako km ulimpa kwaupendo. Sas unmtangaza humu.bila huruma hukuwa rafiki mzuri tangia zamani

hata alikuomba tu mchango kwa kukujaribu alijua hutatoa. Au unataka kitu kwake. Au. Pia alikosea tu kuomba hela ya harusi kwako huna thamani kiviile muongo muongo tu. Watu hukosea njia ghafla tu ameomba. hayaaa

Hivi unajua urafiki wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom