Jinsi akina mama wanavyochangia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Kasi ya mmomonyoko wa maadili ni kubwa sana kwenye jamii lakini asilaumiwe mwingine bali mwanamke kivipi? Twende pamoja

1. Akina mama majumbani ni kitu cha kawaida kumtambulisha binti yake kwa mchepuko wake,na lengo la kumtambulisha kwa mchepuko ili kurahisisha njia ya kupata vitu vinavyonunuliwa na mchepuko na hela ya matumizi, mfano "Anita nenda kwa baba fulani akupe hela yangu uniletee" na binti na yeye hataogopa kuwa na mpenzi wake maana mama hatagomba na mama ana mpenzi

2. Mabinti wa shule hasa sekondari anapoweka msimamo kutokuwa na mahusiano akiwa shule mama yake husababisha binti kuingia kwenye mapenzi. Utasikia binti anamwambia mama yake"mama unaona lile lijimwanaume lenye duka kule kona ety linanitongoza juzi lilinipa elfu 80 niwe mpenzi wake nikakataa"mama hujifanya kumpongeza binti lakini kwa sababu ya ukata na umasikini utasikia mama anamwambia binti yake"Dahh maisha yametupiga mwanangu mpaka nataman zile elfu 80 ungechukua uniletee" Kifuatacho utajua wewe

3. Mabinti wanatunziwa siri sana na mama zao, binti anaweza akawa anajingiza kwenye mambo ya ajabu mtu wa kwanza kujua ni mama, kamwe usitegemee mkeo atakwambia, wachache sana,binti ana simu, mama anajua baba hajui na mbaya zaidi sometimes mama anaazima simu ya binti yake au mama akiona simu ni kali humtaka binti yake wabadilishane

4. Akina mama majumbani vijana wao wanatambulisha wachumba zao kila siku na vijana hata umri wa miaka 18 hajafika ila mama anatambulishwa mchumba na mama anafurahi sana au mama anakuwa anamtania binti wa fulani kuwa ni mkamwana,kinachofuata utajua wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom