Jini mahaba linavyonitesa

Jini mahaba linavyonitesa

migisha

Member
Joined
May 13, 2013
Posts
99
Reaction score
20
Hi ni history ya kweli ya maisha yangu naomba mnishauri wadau.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 29 ni mkristu na ni mzaliwa wa morogoro mwenye asili ya mkoa wa kilimanjaro.Wakati wa utoto wangu nilikuwa ni mtu mwenye akili sana.Kuanzia la standard 1 mpaka form 4 nilikuwa naongoza nikishuka sana nakuwa mtu wa pili au wa tatu.Kifupi nilizaliwa nikiwa na akili sana pia nilikuwa na nyota ya kupendwa na watu na nililelewa kwenye mazingira mazuri nikiheshimu kila mtu.
Tatizo hili lilinianza nilipokuwa shule ya msingi yaani nilipofika std 7. Nilikuwa napita karibu na mto na kuna mti mkubwa.Nilihisi nywele kusisimka na nikawa kila nikipita hapo naokota pesa. Tabia hiyo iliendelea kila siku mpaka jamaa na wazazi wakawa wananiambia nawaibia na kusingizia naokota.Mpaka namaliza std7 nilikuwa sijawahi kutana na mwanamke.Nilipofika form 2 nikibalehe bt hapo ndipo nilipoanza hisi utofauti.Nilianza kupata wet dream ila nilijua ni kawaida kama mwalimu wa biology alivyotufundisha bt cha kushangaza ndoto hizo zilikuwa ni endelevu.Mwaka huo huo nilipata dada mmoja akawa mpz wangu ila nilipokuwa namdu sikuwa nahisi raha kama ambavyo naota.Pia nikaanza tabia ya uongo, uchonganishi, unafki, hasira pia nikawa nachukiwa na wanafunzi na hata walimu bila sababu.
Nilipomaliza form 4 nilifaulu kwenda A level pindi hko nilikuwa na mwanamke m1 ambae alikuwa na mimba yangu bt cha kushangaza ile mimba ilitoka kwa mazingira ya ajabu.
Nilipofika A level nikawa na tabia ya kujichua na kupenda wanawake kupitiliza.Nilikuwa natoroka shule na kutafuta wanawake kuanzia mabaamedi, mama guest mpaka wanaojiuza nikikosa napiga punyeto huku na zile tabia zingine zikiendelea.
Nilienda chuo kikuu k1 moro na kuendeleza hizo tabia mpaka nilipomaliza chuo na kuanza kazi arusha.Wakati nilipokuwa chuo nilimtia dada m1 mimba ila pia mtoto alifia tumboni bila sababu.
Nikiwa kazini arusha mabosi na wafanyakazi wenzangu wakawa wananichukia bila sababu mwisho nikafukuzwa.
Siku 1 nikiwa arusha wakati nimefukuzwa kazi nikaenda kanisa la safina.Nilijishangaa nilipopandisha mashetani baada ya maombezi na kuanza ku confess na hayo mashetani yakasema yote tangu kuniingia mpaka walivyosababisha kuua watoto wangu pia kunisababishia UKIMWI, kuchukiwa, kutopata maendeleo mi na familia yangu yote.
Nilimshukuru mungu na kuanza maisha mapya ya maombi ila sasa kuna lingine limeibuka.Nikipitiwa na kulala bila kusali huwa naingiliwa sana kinyume na maumbile nikiamka najikuta nimechafuka.Nguo zangu za ndani zinachafuka sana.Nateswa na haya majini natamani kujiua husasani kwa vitendo ninavyofanyiwa pia mi ni muathirika bila kupenda.Nimechoka na maisha haya sijui nitafanyaje?Mnanishaurije wana jf?Natamani nikipata pesa niende nigeria kwa tb joshua kwa ajili ya maombezi.Naombeni ushauri wenu.
 
Rudi safina ukaombewe. Kama ulisaidiwa mara ya kwanza, utasaidiwa mara ya pili. Hii story yote kama ilivyo hadi ya kuokota pesa uwaambie.

Umeshahudhuria clinic ya hiv? Nakushauri usiache kupimwa ili kama unahitaji dawa uhudumiwe.
 
Maombezi unaweza kuyafanyia chumbani kwako...jiulize swali, imani yako iko wapi? Una imani walau udogo wa punje ya haradali? Kama ndivyo piga magoti hapo chumbani kwako na uyakemee katika jina la Yesu.

Pole kwa yaliyokukuta...Mungu na akusaidie.
 
Dah pole sana bro endelea kumtumikia mungu na atakufariji. Usikate tamaa ndugu yangu. Mungu yupo.
 
pole sana.Maombezi ndo mkombozi jitahidi sanai sana kujipigania.Hiyo ya kuingiliwa nyuma inaweza kukuathiri zaidi. Omba sana,sali sana kuwa na imani thabiti pia jitahidi uhudhurie clinic kama hujaanza.
 
Pole sana ndg, usijiue, Mungu aliyekusaidia mwanza atakusaidia na sasa, kikubwa jenga imani yako ktk neno, jifunze kuomba na kusimama peke yako ukimtegemea Mungu.
Tafuta kikundi cha maombi hapo karibu unapokaa, kama huwa wanakutana kila siku na kuomba basi itakusaidia na kukujenga pia.
 
Is it true story?? It sounds fictional.
Anyway, congrats na wewe kwa kuanzisha thread.
 
watu wengine!bwana sasa ndio nini?

hey usilazimishe fikra zangu zimatch na za kwako. Usilazimishe nielewe & kuamini kila nisomacho kama wewe. Mimi sio bendera eti nifuate upepo!

Watu tunatofautiana in thinking & analyzing things. That's why 'akili ni nywele kila mtu ana zake'.
Hapa JF... some topics/threads are just for fun and killing time.
So heshimu maoni ya mtu.
 
hey usilazimishe fikra zangu zimatch na za kwako. Usilazimishe nielewe & kuamini kila nisomacho kama wewe. Mimi sio bendera eti nifuate upepo!

Watu tunatofautiana in thinking & analyzing things. That's why 'akili ni nywele kila mtu ana zake'.
Hapa JF... some topics/threads are just for fun and killing time.
So heshimu maoni ya mtu.

Huna maoni yoyote wewe. Jamaa kasema history ya kweli na anaomba asaidiwe kimawazo then wewe unaleta maskhara? Hebu acha hizo tabia za ajabu ni si lazima ucomment kila kitu. Ser*****kamba you. Mnaboa sana.
 
Is it true story?? It sounds fictional.
Anyway, congrats na wewe kwa kuanzisha thread.

Toa umizengo pinda wako hapa. Kwani lazima utoe comment kwenye kila thread?
Jf siku hizi imejaa mulugo product bado hawajaja wenye jf wenyewe na kuanza kutaniana na kusalimiana ilihali jamaa anaomba ushauri.
 
Pole sn!tafuta anointing water ya tb joshua au rudi safina as kingasti say,comfess yote watakuombea na weka imani kwa maombi,usikate tamaa nenda clinic pia ,ila naimani hata ilo jini ndio sababu ya kukupa yote hayo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Bro nakushauri uende tena safina watakufanyia maombezi na hayo mambo yataisha tu. Usikate tamaa mungu atakupigania.
 
Pole xana kaka,,....rudi kwa Allah faraja inapatikana kwake tu
 
Huna maoni yoyote wewe. Jamaa kasema history ya kweli na anaomba asaidiwe kimawazo then wewe unaleta maskhara? Hebu acha hizo tabia za ajabu ni si lazima ucomment kila kitu. Ser*****kamba you. Mnaboa sana.

hahahaa, so wewe umempa maoni gani? au ndo umeamua tu kunitusi ili na wewe uonekane umekomment? and ebu prove it kama iyo story ni ya kweli.

acha kutoka povu mkuu
 
Nawashukuru wote kwa ushauri wenu. Nitajitahidi nirudi safina kwa ajili ya maombezi na pia naamini hata huu ukimwi ambao ninao utapona kwa yeye awezaye. Kweli nilikuwa nahangaika sana ila baadae nikikaa na kufikiria kwanini mimi nimekuwa hivi. Sijutii kuwa na ukimwi ila naumia sababu siwezi kupata mtoto tena. Naamini mungu atajibu maombi yangu siku 1. Sikuzaliwa hivi najua mungu alinileta duniani kwa malengo maalum.
 
Toa umizengo pinda wako hapa. Kwani lazima utoe comment kwenye kila thread?
Jf siku hizi imejaa mulugo product bado hawajaja wenye jf wenyewe na kuanza kutaniana na kusalimiana ilihali jamaa anaomba ushauri.

mkuu acha kuendeleza umizengo pinda apa. teh teh teh
 
Back
Top Bottom