Jini hili jini gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jini hili jini gani?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by mapango, Jan 10, 2011.

 1. mapango

  mapango Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kama hili hulioni, macho yako yana kutu
  meliona mie jini, langamiza wetu watu
  zaidi ya subiani, kiziwi kupewa tutu
  jini hili jini gani, chano chake damu zetu?
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Jini hilo nimeliona, linaua bila huruma
  Halijali maamuma, wala imamu
  Jini hilo bwana, linatisha kama b52
  Jini hilo ni ...........
   
 3. mapango

  mapango Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mbona mekaa kimya, au jini mwamogopa?
  hata kama hana haya, vidonge vyake tampa
  mie sioni vibaya, kwa mola wangu naapa
  dawa ya baya ubaya, si museme hapa hapa!
   
 4. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Sor nimekosea mlango.
   
 5. October

  October JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Mtunzi kwanini Habari za Majini hakuwauliza wale wanaoyafuga na kusali nayo.????
   
 6. mapango

  mapango Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hapa ndugu yangu unakuwa kilaza sasa. Pole sana siwezi kukusaidia.
   
 7. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hili ni jukwaa la lugha, wee kama sio mtaalam wa lugha kaa kimya, huna haja ya kuchangia. Hapa imetumika lugha ya picha na hilo jini lililotajwa humo sio jini unalolifikiria wee. Unayotaka kuyaleta ktk jukwaa hili wala hayastahili.
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jini limekuwa gumzo bara na visiwani
  Jini linanyonya damu na kuweka gizani
  Jini hili twalijua na tutaliweka kiganjani
  Jini hili si maimuna wala shubiani
  Jini lenyewe jeupe kama "Muirani"
  Jini limeng'angani halisikii la muadhini
  Jini halikubali linataka kutulisha majani
  Jini lina kibri, kushanda mumiani
  Jini limejikita uraini mpaka bungeni
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Nadhani tatizo ni shule yako ndogo sana.................
   
Loading...