Jingles za Clouds FM na Bongo FM ni kiboko

Jingles za Clouds FM na Bongo FM ni kiboko

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
5,717
Reaction score
7,397
Hizi redio zenye maudhui ya vijana zinashindana sana.Zimetengeneza nyimbo za utambulisho wa redio zao kiboko kwelikweli.

Clouds wimbo wao ni nyoosha njia na Bongo FM wimbo wao ni hakuna mipaka. Nyimbo hizo huwavutia sana wasikilizaji kiasi cha kuwaongezea wasilikilizaji, kitu ambacho ndio mtaji wa vipato vyao.

Ni ubunifu wa hali ya juu sana.Redio zingine zinasuasua sana kwenye eneo hili.
 
Kumbe Kuna watu bado wanasikilizia redio ?
Oh sana tu,tena mfano mimi nasikiliza redio kutoka kwenye redio yenyewe na sio kwenye simu.Na nina redio nyingi tu za brands mbalimbali.Na kuna moja nimeletewa wiki 2 zilizopita ambayo inatumia umeme,sola na ina mkono wa kuzungusha ili ipate chaji.Ni fm/am redio na ina tochi pia.Ipo redio nayosikilizia nikiwa chumbani,kuna nyingine sebuleni,nyingine nikiwa nje ya nyumba na kuna nyingine ni kwa ajili ya safari tu.Japo mie ni mwislamu lakini nasikiliza stesheni za kila dini
 
Clouds fm ishakuwa ya magen-z kuanzia jingles zake na kila kitu.

Sisi millennial tusikilize radio free Africa asubuhi na mchana saa 7 na jioni saa 12
 
Hizi redio zenye maudhui ya vijana zinashindana sana.Zimetengeneza nyimbo za utambulisho wa redio zao kiboko kwelikweli.Clouds wimbo wao ni nyoosha njia na Bongo FM wimbo wao ni hakuna mipaka.Nyimbo hizo huwavutia sana wasikilizaji kiasi cha kuwaongezea wasilikilizaji,kitu ambacho ndio mtaji wa vipato vyao.Ni ubunifu wa hali ya juu sana.Redio zingine zinasuasua sana kwenye eneo hili.
Sawa mkuu. Hizo ndizo nyimbo zenu vijana.
 
Back
Top Bottom