Jinamizi / Nightmare

Mara ya kwanza mkuu kupatwa na hio hali nilihisi nataka kuaga dunia, niligopa sana nilivorudi kwenye hali ya kawaida, yalipigwa maombi ya kufa mtu

Aliko Dangote
Pumzi zinakata, halafu unajiona nguvu zinakuishia.

Yaani unaona kabisa wewe na kwa Mungu jirani.

Hiyo ukipata haueni lazima ukae Kitandani kwanza ili Mawenge yashuke, na Mimacho lazima ikutoke kama Mjusi aliebanwa na Mlango.

Na lazima uwashe Taa hiyo.

Hapana kabisa chezea Jinamizi
 
Kulala Chali nadhani ni watu wengi inawatokea.Rafiki yangu aliniambia eti ukilala Chali damu inatoka kwenye ubongo na kurudi nyuma ndipo unahisi kukabwa.Umenichekesha na kutingishwa una tatizo kama langu na mm huwa naomba mtu aje anitingishe!Kama ni mchana unasikia watu wanaongea unawaita waje kukutingisha hawasikii!

Sent from my SM-A710F using JamiiForums mobile app
Bora kulala Chali.

Mambo ya kulala kifudi fudi Popobawa anaweza kukutimbia.

Kifudi fudi sio ulalaji hata kidogo, afadhali kiubavu ubavu
 
Inaitwa sleep paralysis unaparalyze sekunde kadhaa baada ya kuamka... inasemekana hutokea kwa sababu mtu anakuwa ameamka akili na macho tu misuli inakuwa bado katika hali ya kulala hapo mtu huhisi kama amekufa huku anajiona
Hii yako ina Mantiki fulani.

Na hata Akilini inaingia
 
Bujibuji asante sana kwa elimu mm ni muhanga wa majinamizi kwa kweli yanatesa kinomanoma yaani.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Pole sana Kiongozi.

Jaribu kubadilisha Mlalo.

Na kama wewe ni Mkandamizaji (Mpenda Kula) jitahidi Chakula cha Usiku husijishindilie, kula kiasi/kidogo.

Na upate Chakula mapema, ikiwezekana hata Masaa Matatu au japo Mawili kabla ya kwenda Kulala.

Kuvimbiwa nako kunachangia
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom