Jinamizi ni nini? Naomba msaada wenu

Mtemi Ngeleja II

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
277
250
Asalaam

Nimekuza najiuliza Jinamizi ni nini hasa? He ni Jini? Mizimu? Pepo au mashetani?

Nyakati za usiku hasa usiku wa manane inatokea upo kwenye ndoto ambayo huwezi kupumua wala kuongea lakini unasikia kila kitu.

Mbaya zaidi unakua unatamani hata mtu akuguse ili uzinduke. Kifupi ni kama umekabwa au kubanwa na kitu.

Wengine hali hii huwapata nyakati za mchana wakiwa wamelala.

Hivi Jinamizi ni nini?

Nawasilisha.

=====
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.

Tafadhali Blasto Ngeleja pia soma Kukabwa na jinamizi wakati usiku umelala
 
Jesusfreak08

JF-Expert Member
Jul 20, 2019
760
1,000
Kwa takwimu chache nilizo nazo.

Wanaokukaba hao ni wachawi (nilifanikiwa kuwaona) maana hata Mimi nilikuwa nakabwa Nikita YESU yananiacha

Nikaamua kumpokea YESU kama BWANA na mwokozi kwenye maisha yangu hayo kwa sasa ni storia ni kama navyosoma hapa kwenye Uzi wako.

Kama unakabwa nisikufiche YESU ndio jibu wengine Wote wababaishaji.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,129
2,000
Asalaam

Nimekuza najiuliza Jinamizi ni nini hasa? He ni Jini? Mizimu? Pepo au mashetani?

Nyakati za usiku hasa usiku wa manane inatokea upo kwenye ndoto ambayo huwezi kupumua wala kuongea lakini unasikia kila kitu.

Mbaya zaidi unakua unatamani hata mtu akuguse ili uzinduke. Kifupi ni kama umekabwa au kubanwa na kitu.

Wengine hali hii huwapata nyakati za mchana wakiwa wamelala.

Hivi Jinamizi ni nini?

Nawasilisha.
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,033

Jini, mapepo na mizimu ni kitu kimoja. Mizimu ni majini/mapepo yenye nguvu katika familia, ukoo au jamii fulani. Mashetani ni malaika walioasi na wapo katika daraja la juu na wana nguvu zaidi ya mapepo/majini/mizimu.

Jinamizi kusababishwa na majini yapendayo kumwingia mtu akia usingizini na kuchukua hatamu ya sehemu muhimu katika ubongo wa mwanadamu ili kuweza kufanya watakavyo. Mchawi aliye katika roho anaweza pia akamwingia mtu kama jinamizi. Hawawezi kuchukua hatamu ya roho yako kwani roho yako ina nguvu ya ajabu ya kimungu, hivyo huchukua hatamu ya mwili wako tu.

Wanapenda pia kuchukua hatamu ya uwezo wa mtu wa kutamka ili mtu asiweze kupata msaada kwa wenzake au kwa Mungu (Yesu Kristo).

Cha kufanya unapopata jinamizi ni kujitahidi kuita Jina la Yesu. Kama huwezi basi fikiri au leta picha ya Yesu kichwani na mara moja jinamizi hutoweka.

Ili usipate jinamizi dawa yake ni kuwa mtu wa Yesu Kristo, yaani mtu aliyekombolewa kwa Damu ya Yesu Kristo na kuishi maisha safi. Pia usikubali hata siku moja kulala bila kusali na kujiweka chini ya ulinzi wa Yesu Kristo. Ukifanya hivyo majinamizi utasikia tu hadithi zake kwa wengine.
 
Asante sana ndugu... Nimeelewa sana
 
Mtemi Ngeleja II

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
277
250
Kwa takwimu chache nilizo nazo
Wanaokukaba hao ni wachawi(nilifanikiwa kuwaona) maana hata Mimi nilikuwa nakabwa Nikita YESU yananiacha

Nikaamua kumpokea YESU kama BWANA na mwokozi kwenye maisha yangu hayo kwa sasa ni storia ni kama navyosoma hapa kwenye Uzi wako

Kama unakabwa nisikufiche YESU ndio jibu wengine Wote wababaishaji
Asante ndugu yangu.. Kweli Yesu ni kimbilio
 
Zabron Hamis

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
3,973
2,000
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
Asante kwahili. Hii haki siku ya kwanza mimi nilijua ndio nimekufa kabisa. Ni kitendo cha chini ya dakika 3 lakini unahisi kama mwaka vile. Lakini mimi hua nawaza, hv mtu akikugusa au kukushtua katika hali hiyo, sinndio unasafiri mazima?
 
Zabron Hamis

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
3,973
2,000
Ni kweli Yesu ni kimbilio, lakini kuna vitu ni vya kawaida kabisa tuache kutumia imani yetu vibaya. Cha kwanza kabisa ambacho naamini mtu anayeamini katika Jina la Yesu Kristo, harogeki hata kidogo. Hivyo kama unaamini sleep paralysis ni uchawi au ujini ilihali unaishi ndani ya Yesu, huyo yesu wako na yesu wa kangi ni hali moja, believe it or not. Mara nyingi nikiwa nimelala ikatokea hali ya uchawi ndani hata kama nimesinzia hujikuta katika mapambano na ndipo Yesu hufanya kazi yake kwa uwezo wa Roho mtakatifu. Biblia inasema Roho ni mwombezi wetu, hivyo hata tukiwa hatuna ufahamu, yeye huomba kwaniaba yetu. Na hajawahi kuniangusha hata kidogo. yesu wako anaruhusu mpaka mapepo yakuingie kabisa?
 
Mtemi Ngeleja II

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
277
250
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
Kaka kwaio hao sio wachawi Kumbe ni hali ya kawaida katika ubongo.?
 
ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,157
2,000
Asalaam

Nimekuza najiuliza Jinamizi ni nini hasa? He ni Jini? Mizimu? Pepo au mashetani?

Nyakati za usiku hasa usiku wa manane inatokea upo kwenye ndoto ambayo huwezi kupumua wala kuongea lakini unasikia kila kitu.

Mbaya zaidi unakua unatamani hata mtu akuguse ili uzinduke. Kifupi ni kama umekabwa au kubanwa na kitu.

Wengine hali hii huwapata nyakati za mchana wakiwa wamelala.

Hivi Jinamizi ni nini?

Nawasilisha.
Mkuu mbona hizo ni ishara za Corona
 
machomanne

JF-Expert Member
Feb 22, 2017
799
1,000
Usiwe na hofu brother. Hali ya kujihisi umebanwa na kushindwa kupumua hutokana mambo mawili:-.
1. Watu wengi wanaodai kukabwa usingizini huwa ni wale wanaopenda kulala wakiwa chali. Hili ni jambo la kawaida kabisa hata Mshana Jr, analisimulia mara Kwa mara , (Astra Projection).
Kila Mtu anapokua usingizini , Roho pamoja na Nafsi hutoka kwenye mwili na kuranda randa maeneo yaliyo karibu na mwili wake, au hata zaidi ya hapo, Lakini, hawezi kujua kwa vile hana elimu ya kutoka katika mwili. Hivyo aamkapo hudhani kuwa alikuwa katika ndoto.
Walio na Elimu ya kutoka katika maili yao, huwa wanatoka wakiwa na akili timamu na hata kuwawezesha kuona maili yao umelala vitandani.
Nakutahadharisha kuwa unyemelewa na hali ya kutengeneza "Astra Projection". Ili kuiepuka hali hiyo, epuka kuingia usingizini ukiwa umelala chali, hali haitakutokea, itakoma. Zoea kulala ubavu.
2. Vile vile, yawezekana ikawa unatembelewa na Pepo wachafu wa ngono waitwao Succubi, au Succubus.(Mapepo ya kike) yanayofuata wanaume usiku kufanya nao ngono hasa wale wasiokuwa na Wanawake. Au Incubus (Mapepo ya kiume) yanayofuata Wanawake usiku kufanya nao ngono.
Mojawapo ya dalili za kuwa unavamiwa na pepo hao, ni kubanwa pumzi na kushindwa kujigeuza.
Epuka kulala chali brother, you 'll be Okay.
Kalagha bahho!!.
 
Expert Judgement

JF-Expert Member
May 29, 2019
399
1,000
Daaa mm imewahi kuikumba siku moja nipo macho sijalala Tena hata usingizi Sina ilikua saa 8 usiku nsona tu tukio linaendelea mbele yangu ikabd nijikusanye nguvu nakujitingisha mwili mzima ndo haliikapotea. Ila waliokuwa wanafanya Mambo yao mbele yangu waliaibika sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom