Jinamizi ni nini? Naomba msaada wenu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,421
2,000
Kaka kwaio hao sio wachawi Kumbe ni hali ya kawaida katika ubongo.?
Kichawi liko hivi
19399370_1346869158681885_8247704969629167972_n.jpg
 

Kapyepye Mfyambuzi

JF-Expert Member
Jun 18, 2020
421
500
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.

Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
Hatua hiyo sasa tunaiweka kwenye Astral projection? au Lucid dreaming? maana hata Mimi huwa inanitokea sana nakuwa sijuw nini nifanye.
 

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,546
2,000
Majinamizi ni roho za watu na mapepo ambao hayana mwili.
Kwahiyo yanakuvagaa wew kidogo yaonje raha ya kua na mwili.
Na yanavyokukaba haliwi moja yanakua mengi mengi ili yakuzidi nguvu vizur, yani hufurukuti hata kidogo.
 

bugaruu

Senior Member
Jun 7, 2020
183
500
Nakumbuka nyumba ya mwisho niliyohama usiku mmoja mwenye nyumba alisikia kuku wake wanapiga kelele usiku binafsi pia niliwasikia ila kW mbali na sikutilia mkazo, ila wao walitoka nje kuangalia ni nini. Katika kutafuta wakapita dirishani kwngu huku wanazungumza jamaa anamuambia mkewe... Ila ni muda huu na nna uhakika hajatoka nje" ikabidi niwaulize kupitia dirishani sababu nilikuwa nawasikia VP! Mmefanikiwa kuona chochote? Hapana... Na wakarudi ndani yani kile kitendo wanamaliza kufunga mlango nikaanza kusikia vishindo vinaelekea kutoka nje kupitia geti dgo si ndio nikataka niinuke nichungulie dirishani kwani niliweza kuinuka sasa! Nilikandamizwa mpka vishindo vilipotokomea ndo nikaweza kuinuka yaani ule mkandamizo ni dizaini hii ya jinamizi kiasi hta kuongea nilishindwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom