Kipindi Vodacom wameleta haka ka system ka kuona jina la unaemtumia pesa/muda wa maongezi kabla ya kutuma kwa kutumia MPesa nilifurahi manake nilijua ingepunguza matatizo ya kutuma pesa kwa watu ambao hawahusiki. Kinyume na matarajio yangu nashangaa nikiwa najitumia muda wa maongezi kupitia Mpesa linakuja jina la mtu mwingine kabisa nikadhani nimekosea namba yangu lakini nikihakikisha hiyo ndo namba yangu..... nikajua labda hizo database zao bado zinachakata lakini kila siku nikijaribu namba yangu inaandikiwa jina la mtu mwingine tena jina hilohilo. Bado sijajua kama hili tatizo ni langu tu au kuna wadau wengine wanashida kama hii..Manake hii ni hatari sasa.