Jina lako lina chapa mbili

Jina lako lina chapa mbili

Sijui kwa nini umeniunganisha na hili; lakini tafsiri ya mchambuzi ipo sawa kulingana na 'imani' aliyokuwa nayo mwandishi na chanzo cha 'maarifa yake'

Hmmm

Chanzo chake hakitoshi, kwa hiyo sina ulazima wowote wa 'kubadilishana naye mashauri' mpaka awe tayari kunipa 'ruhusa' niweze kuyabatilisha yote hayo; ama anioneshe yuko tayari kusikiliza na kufuatilia yaliyo ni mbadala...

Je, ndugu Ndaga uko tayari kuniruhusu nibatilishe msingi wa 'maarifa' yako? kuanza na mapungufu ya 'vina vya tafsiri'?

Kama hauko tayari ni sawa tu. Komaa katika mashauri ya imani yako mpaka pale utakapodhani unaweza kuyapitiliza...

Yote kheri
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa hisani yako naomba kumkaribisha @Mzee Mwanakijiji asome huo ujumbe.Maana tuko wengi ametukwaza na programu yake ya Zinduka!

Mdogo wangu, umenifanya nitabasamu. Usikwazike sana... mwenzio nimekwaza na hawa wenye programu ya mabadiliko feki... kwa kweli wamenikwaza lakini nawaelewa.
 
Hivi pengo mbona simsikii kimya sana .mahana wanao tamba gwajima na kakobe tu.wapi pengo?
 
mose reply ni ya Ndaga ila mimi ndio nimekutag, naamini Ndaga hatajisikia vibaya kwenye hili
Nia ilikuwa ni kukualika kwenye kile alichokisema
 
Last edited by a moderator:
Hivi pengo mbona simsikii kimya sana .mahana wanao tamba gwajima na kakobe tu.wapi pengo?

Mwadhama kadinali Pengo ana utaratibu maalum chini ya kanisa katoliki kufanya au kusema chochote au kuamua
Hawa wengine wawili wao ndio wenye maamuzi ya mwisho kwenye kila jambo kwakuwa hawafungwi na taratibu za Taasisi wanazoziongoza
 
Ni kitu ambacho hujawahi kukiwaza au kukisikia popote, lakini pia Inawezekana kabisa umeshakisikia tena mara nyingi tu lakini pengine kwa lugha tofauti.

Jina lako lina chapa mbili, chapa ya kuzimu na chapa ya mbinguni au kwa maana nyingine chapa ya nuru na chapa ya giza
Kawaida ya mwanadamu hupenda kubalance mambo kwa shetani kidogo kwa Mungu kidogo...kiasili jina lako huandikwa mbinguni tangu uumbaji na unapoingia duniani hufanya new registration ya kuzimu ambayo ndio huwa na nguvu zaidi ya kutawala maisha yako.

Pale unapoangaziwa , kwa imani yoyote ile na kuacha mabaya yote na kuamua kumrudia Mungu wako ni kipindi ambacho hutaka kufuta ule usajili wa kuzimu na kubaki na usajili wako wa asili, usajili wa mbinguni.

Hapa ndipo penye shida na ukisikia vita ya kiroho basi ujue ni hii . shetani hayuko tayari umkimbie kwakuwa usajili wake huweza kufutika tofauti na ule wa mbinguni au haufutiki milele, ni kipindi hiki ambapo shetani hukodi majeshi yake yoote kwa ajili ya kukurudisha kwenye himaya yake...hii ni vita ngumu mno vita ya kiroho vita ya mbingu.

Chunguza kwa makini huwezi kukosa mfano wa walao mtu mmoja unayemfahamu ambaye alikuwa ni mshika dini na mlokole hasa halafu akaanguka dhambini, huwa mbaya maradufu ya vile alivyokuwa mwanzoni na mtu wa namna hii ni ngumu kusimama na kumrudia tena Mungu.

Mtu wa namna hii anapoamua kusimama dede na kupambana kiroho, mbingu hutakisika, familia na jamii huingia katika mkanganyiko mkubwa mambo huharibika na hata vita yaweza kutokea katikati ya jamii hasa kama mlengwa alikuwa ni mtu mwenye nafasi ya kimamlaka na ushawishi katika jamii.

Tunaelekea kwenye uchaguzi ambao kwa namna moja au nyingine na kwa uroho wa madaraka na kutawala kuna baadhi ya washika dau wakaambiwa kuhusisha nguvu za giza lakini vilevile baadhi kwa mapenzi mema kabisa wakaamua kumhusisha Mungu moja kwa moja...hapa tutaingia kwenye uchaguzi wenye chapa mbili mbili uchaguzi wenye utusi tusi wenye vita ya kiroho kati ya ufalme wa nuru na ufalme wa giza.

Mungu pekeyake ndiye atakayeweza kutupitisha salama kwenye uchaguzi huu....tuuombee sana huku tukiikataa ile chapa ya pili chapa ya kuzimu
Mkuu hapa nadhani unazungumzia sadaka
Kitu pekee kinachopatikana kwa Mungu na kwa Shetani ni sadaka.
Sasa upande mmoja humtolea shetani sadaka za makafara,mauaji ya albino n.k.
Upande wapili hutoa sadaka zilizo njema machoni kwa Mungu.
USHAURI.
Inabidi sadaka iliyo njema machoni kwa Mungu iwe kubwa kuliko sadaka itolewayo kwa shetani,hii itafanya mambo yawe shwari/murua.
n.b.
unachukua,unaweka.............

nzalendo shetani hapaswi kupata chochote hata sifuri
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa hisani yako naomba kumkaribisha @Mzee Mwanakijiji asome huo ujumbe.Maana tuko wengi ametukwaza na programu yake ya Zinduka!
Khaa!! Kwa kuzinduliwa kutoka kwenye giza? kwanza ungekuwa na akili ungemshukuru
A%20S%20shade.gif
 
Mdogo wangu, umenifanya nitabasamu. Usikwazike sana... mwenzio nimekwaza na hawa wenye programu ya mabadiliko feki... kwa kweli wamenikwaza lakini nawaelewa.

Mkubwa tuko kwenye Boti mmoja likizama wote twafa-mbaya zaidi wewe umeamua kulitoboa kabisa pamoja na kuwa wimbi liloipiga Boti kwa kiasi Boti linaweza kuhimili Safari yetu.

Hadithi mmoja kama hutajali/au kwa nani mmoja ni swali!

Usiku mmoja Mama au Baba mmoja kamfumania mwenzi wake kitandani kwao kwa hasira akatoka nje ya nyumba na kuitia kibiriti nyumba yao na kuteketea kwa moto huku ndani yeke kukiwa na Watoto!
Je hapo Burasa au akili ya kawaida imetumika?

Neno la hekima,
 
Sina hakika kama ntakuwa nimechelewa sana lakini kwa sababu muda hauishi na natumai wazi kuwa muda haujaisha hivyo bado nipo au tupo ndani ya muda pamoja tukitakikana kufanya yale tunayotakiwa kufanya na si kufanya tu alimuradi wa kufanya ila kila lifanyikalo juu ya nchi hufanyika kwa sababu na MUNGU anakusudio lake kwa viumbe wake kufanya hayo tuyafanyayo, natumai sijatupwa mkono na muda nikitumai wazi kabisa kuwa muda/mada haijaisha, shukran.

Situmai kuwa ntakuwa muongeaji sana laa hasha ila kwa lile ntakalokuwa nimeongea limepaswa kuongelewa hivyo ambavyo limeongelewa, kama tu nilivyokwisha sema mwanzo ya kuwa kila litendekalo juu ya nchi ni kusudio la MUNGU mpaka likatendeka hivyo. Binadamu amepewa utashi wa kujua jema na baya lakini haiyumkiniki kusema kuwa MUNGU angeshindwa kuweka akili za binadam zikafanya mambo mazuri na mema tu siku zote, kwa hilo ni dogo sana mbele za MUNGU ila pia kuna jambo ambalo amelificha kutaka kujua kiumbe wake yupi atakayeweza kuling'amua jambo hilo japo sitaweza kusema ni jambo gani lakini binadamu kama binadamu si tumepewa utashi na akili basi natumai tutaweza kufaham ni jambo gani hilo nnalolizungumzi.

Kwani wakati tunaumbwa na MUNGU wadhani MUNGU hakujua kuwa viumbe wangu ni dhaifu ?, wadhani MUNGU hakujua kuwa viumbe wake hatujakamilika isipokuwa ni yeye tu ndiye aliyekamilika ?, kwani angeshindwa kutufanya tukawa IMARA JUU YA KILA KITU ?, kwani angeshindwa kutuleta peke yetu tu pasina kumleta huyo mnayemwita shetani ?, shetani ni nani kwani ?, usione nauliza maswali haya ukadhani kuwa nahitaji majibu hapa ila ni moja kati ya maswali-maelezo ambayo hayahitaji majibu ndani walau tu kama yatakuwa na majibu nayo vyema si mbaya. Ni nani ambaye hataweza kuwa na kosa ndani ya ulimwengu sidhani kama atakosekana hata mmoja ilhali tu wameweza kuwa na makosa viumbe wa karibu kanisa na MUNGU ; MANABII ambao walikuwa na uwezo wa kipekee na wa hali ya juu seuze sisi binadam wa kawaida tusio na chochote ?.

Kusudio la MUNGU ni nini hasa kumleta huyo mnayemwiya shetani aje kuishi nasi binadam au MUNGU anapenda kututupa watoto kuzimu!jehanam na kufurahi akituona tukiungua wadhani hili ndio kusudio pekee la MUNGU na kama ndio kusudio lake wadhani MUNGU akiamua kufanya jambo lolote atashindwa kufanya ?, nikimaanisha kuwa akiamua kiumbe wake awe kati ya wenye kuokoka wadhani ashindwa ?, au labda kusudio la MUNGU ni kutuchoma JEHANAM nani atakayeweza kumkataza hilo lisitendeke ilhali viumbe aliowaumba ni wake...?.

Ila yote ya yote ni kuwa, kama tufahamuvyo ya kuwa IMANI ni kitu tofauti sana na IMANI YA MTU inabaki kuwa ni IMANI YA MTU tu husika hakuna awezae kuibadilisha vile mtu anavyoamini, hivyo basi kama mtu anaamini hivi itabaki kuwa akiamini hivi na kama anaamini vile, itabaki kuwa akiamini vile kwa sababu ni IMANI YAKE BINAFSI ila kwa IMANI YANGU naamini wazi kuwa kila litendekalo juu ya nchi ni kusudio la MUNGU na mbele za MUNGU hakuna jambo ambalo linashindikana kama akiamua chochote juu ya kiumbe chake.

NAWASILISHA.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kitu kinachoitwa nguvu za giza.
Mnajazana uongo mtupu.
 
Na usamehewe bure tu maana unenacho kinafanana na hilo jina lako hapo hivyo, si kosa lako.
NDUKI tusonge mbele tuu...kumbuka kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom