Jina la Nicole lishakuwa gumzo mtaani, kila mtoto anapewa

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,377
9,297
Habarini!!!!

Hivi sasa kumekuwa na hali ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kwenye tamthilia hasa hili jina la 'Nicole'. Hata humu ndani kina Nicole na mama/baba Nicole wapo wengi sana.

Je mnajua maana/ tabia halisi na chanzo cha kuitwa Nicole? Mmemwona Nicole wa tamthilia ya 'Without You' na nyinginezo matendo yao yapoje? Usije ukashangaa mtoto anakuja kuwa na matendo ya ajabu mpaka unastaajabu kumbe tatizo ni jina tu.

Binti ana mimba mpaka majirani tunakuwa tumeshajua jina la atakayezaliwa kuwa ni Nicole. Nicole imekuwa kama kandambili za Yeboyebo!
 
Labda tu useme jina limekua common.Lakini ukisema tabia za hao Nicole wa kwenye tamthilia watazirithi hii ina tegemeana na mpaji jina alinuia nini.Mfano jina john kwani john wote washakua maraisi.
hahahah asilimia kubwa mtu anampenda muigizaji hadi anakuwa na Mimba anamuwazia aitw jina hilo.
 
Habarini!!!!

Hivi sasa kumekuwa na hali ya watoto wanaozaliwa wanapewa majina ya kwenye tamthilia hasa hili jina la 'Nicole'. Hata humu ndani kina Nicole na mama/baba Nicole wapo wengi sana.

Je mnajua maana/ tabia halisi na chanzo cha kuitwa Nicole? Mmemwona Nicole wa tamthilia ya 'Without You' na nyinginezo matendo yao yapoje? Usije ukashangaa mtoto anakuja kuwa na matendo ya ajabu mpaka unastaajabu kumbe tatizo ni jina tu.

Binti ana mimba mpaka majirani tunakuwa tumeshajua jina la atakayezaliwa kuwa ni Nicole. Nicole imekuwa kama kandambili za Yeboyebo!
Mtaani kwenu wapi dada?
 
Hivi kwann hamthamin majina ya Kiafrika...
Watu hawajielew wanaanza kidogkdog kujidhalau /kujishusha hadhi yao eg, wameanza kujikoboa wae weupe km wazungu, maisha ndani ya tamthilia, majiNa ya tamthilia yaan kila kitu tamthilia huku wanaacha utamadun wao unazorota.
 
praygod/ musa vilevile kuna ya kimila mwakipesile/ ngosha. hahah ila wakikuuliza mi thimooo!!!!!!!!.
 
Back
Top Bottom