Jina la Jakaya Kikwete linatumika na matapeli mtandaoni

Jina la Jakaya Kikwete linatumika na matapeli mtandaoni

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Kwa Bahati mbaya sana kuna kikundi kimoja mtandaoni ambao wanawatapeli watu wakijifanya wao ni kikundi cha vikoba, kwa kutumia jina la Rais wetu mstaafu wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete

Wanawahimiza wananchi wajiunge na hivyo vicoba vyao ambapo wanadai wameweka masharti mepesi mno ya kupata pesa hizo kuwa ukiweka 200,000 unapata 2,000,000 within 35 minutes!

Master mind wa mpango huo ni jamaa mmoja anayetambulika kwa jina la Maliki Chambela, mwenye namba 0710803516 ambaye anadai makazi yake ni Dodoma

Mbaya zaidi wana mtandao wao ambao wanadai wamefaidika na huo mtandao wao wa kitapeli, wakati ni syndicate ya huo mtandao

Yupo mwanadada mmoja anayeitwa Asha Hassan, ambaye anadai anaishi Kigoma ambaye anadai amenufaika na vikoba hivyo na kuinua msingi wake wa kununua vitenge, wakati ni mwongo, naye ni miongoni wa hao matapeli!

Tunaliomba Jeshi la Polisi liwamulike matapeli hao ambao wanaendelea kuzitafuna pesa ambazo hawajazitolea jasho, tena mbaya zaidi kwa kulitumia jina la Rais wetu mstaafu wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete!
 
Kuna moja alijifanya Mzee Samatta, alijuta sana yule kijana!
Ni kitu kibaya sana kulitumia jina la mtu maarufu huku ukitapeli mtandaoni

Ni vyema Jeshi la Polisi likawatafuta hao wezi wa mtandaoni na kuwatia mbaroni
 
Kila siku utapeli mitandao unazidi kuenea sijui jeshi la polisi na TCRA huwa wanaona ni utani.
 
Pumbafu sana.kuna siku nilitaka kutoa laki tano ili nipate million tano!!!
 
Back
Top Bottom