Jina la biashara VS Trade/service mark VS jina la kampuni

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari zenu wapendwa

Naomba kupewa ufafanuzi wa mambo yafuatayo

1)Jina la biashara
2)Trade/service mark
3)Jina la kampuni

Naomba nipewe ufafanuzi katika mambo yafuatayo

~Je jina biashara linaweza kutengenezewa trade mark na likawa ndio jina la kampuni ?

~Jina la biashara lina kazi gani hasa ?

~Je jina la biashara linaweza kubeba jina la bidhaa inayozalishwa na hiyo kampuni / mtu ?

Kama kuna maswali ya ziada mnaweza kuuliza pia kama kutakuwa na nyongeza nitauliza pia.

Ahsanteni
 
1. Jina la biashara ni utambulisho wa biashara yako. Ni lazima kusajili jina la biashara ikiwa jina linalotumika haliendani na jina lako halisi wewe mmiliki wa biashara. Mfano; Nyanzobe Matiku akimiliki duka na kuliita jina hilohilo hatalazimika kusajili jina la biashara, ila Nyanzobe Matiku huyohuyo akimiliki duka na kuliita Majizi Makubwa, itamlazimu kusajili jina hilo kama jina la biashara. Kama biashara ni ya mtu mmoja tu (mmiliki) ndio anashauriwa kutumia usajili wa jina la biashara kibiashara. Usajili hufanyika kwa wakala wa usajili wa biashara - BRELA.

2. Trade / Service Mark ni alama za utambulisho wa huduma au bidhaa - zinazotumika kibiashara au kijamii. Alama hizi husajiliwa na wakala wa usajili wa Biashara (BRELA) na zinalindwa na sheria ya Alama hizo. Mfano, alama ya Toyota inatambulisha kuwa gari hilo unalolitazama limezalishwa na Kampuni ya Toyota na ni Toyota, au Alama ya CocaCola inatambulisha kuwa Soda ni Cocacola na sio Pepsi.

3. Jina la Kampuni ni utambulisho wa biashara inayowatenganisha wamiliki wake na liability za biashara hiyo. Ni lazima kampuni iundwe na watu wawili na kuendelea (mpaka 50). Wamiliki huitwa wanahisa, na liability ya kampuni inaishia kwenye umiliki wao wa hisa tu na sio kwenye mambo mengine. Usajili hufanyika BRELA. Mfano Jiwe Mashimba ni mwanahisa wa kampuni ya Sigara iitwayo Jiwe Company Ltd, wafanyakazi wa kampuni hawajalipwa mishahara kwa mwaka 1 ila Jiwe akaonekana ananunua ndege kwa jina la Jiwe Mashimba, wafanyakazi hawataweza kuikamata ndege hiyo kwa kuwa haihusiani chochote na kampuni ya Jiwe Co. Ltd wakati kwa jina la Biashara wangeweza kukamata hata mashamba anayomiliki ili yauzwe wapate mishahara.

4. Jina la biashara linaweza kuwa la Kampuni. Likiwa jina la kampuni, ule usajili wake kama jina la biashara unakufa.

5. Jina la biashara haliwezi kuwa Trade Mark sababu sio logo, trade mark ni nembo na sio maneno.

6. Tofauti ya jina la biashara na jina la kampuni ni kuwa kampuni kisheria inatambulika kama mti wakati jina la biashara halitambuliki kama mtu (lina thamani ndogo) nk
 
Kwa jinsi nilivyokuelewa kwa mfano
~kale ka nembo ka AZAM ile ndio trade mark
~bakhresagroup ndio jina la kampuni
~ Hapo Bakhressa hana jina la biashara
 
Back
Top Bottom