Jimboni kinondoni: Shule ya Mtambani wanafunzi wanakaa chini

Jimboni kinondoni: Shule ya Mtambani wanafunzi wanakaa chini

Hii elimu ya wabunge na mawaziri kwa wengi ni wa kuandikiwa essays na thesis. Siku moja waweke heading na wawape wabunge karatasi, kila mmoja aandike essay ya maneno 500 ndiyo atoke nje ya jengo. Ninaamini wengi watalala mjengoni.
Hivi adhani hata mbunge kama Msukuma ahitaji maneno 500?

Mie nampa aandike essay na maneno 300 tu.

Namwambia nataka intro (maneno 50) body (200) na conclusion (maneno 50)

Mtihani asimamiwa na hakuna longolongo weye na karatasi na kalamu.

Bila hivyo ubunge hamna.
 
Nyie mmeitendea nini nchi yenu kabla ya kuwanyooshea vidole wenzenu?
Mbona ndio tupo hapa twaandika maoni mazuri tu yaso na athari kwa mtu yoyote awe raisi au mbunge.

Watu wa intelligence kazi yao ni kusoma na kuchukua yale maoni mazuri na kumpatia bi mkubwa.

Lakini badala yake ni kuundwa kwa red army kusaka watoa maoni na kuwapopoa macho.

Sasa nchi itasonga vipi mbele kama hutaki maoni hata kama maoni hayo ni mazuri au ni makali?
 
Kukosekana kwa madawati ya kutosha Shule ya Msingi Mtambani iliyopo Bunju - Kinondoni jijini Dar es Salaam kumesababisha baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa sakafuni, jambo linalowakosesha utulivu.

Kukosekana kwa madawati ya kutosha Shule ya Msingi Mtambani jijini Dar es Salaam imefanya baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa sakafuni jambo linalowakosesha utulivu.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002, hadi sasa ina wanafunzi 2,606 huku ikiwa na madawati 580 kati ya 865 yanayohitajika.
Idadi hii inaleta upungufu wa asilimia 33 wa madawati endapo wanafunzi watatu watachangia dawati moja na hiyo kufanya wanafunzi 867 kukaa chini.

Hayo yamesemwa leo Juni 5, 2025 na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Venance Mwasamakwela, wakati akikabidhiwa madawati 65 kutoka kampuni ya ulinzi ya Gardaworld.

Amesema kwa muda mrefu wanafunzi wamekuwa wakikaa chini au kushirikiana madawati kutokana na uhaba mkubwa wa samani hizo.
"Tunashukuru sana wahisani wetu kwa kuzawadiwa madawati 65 kutoka Gadaworld ambapo itapelekea kupunguza msongamano darasani kwenye ukaaji kwani wanafunzi 195 watakuwa wamepata pakukaa," amesema Mwasamakwela.

Mwasamakwela amesema msaada huo utakwenda kuongeza ari ya kujifunza kwa wanafunzi, huku akiahidi kuyalinda madawati hayo ili yatumike kwa muda mrefu.
“Sasa tuna upungufu wa madawati 224.”

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, Chitegese Dominic Ngaluku amekiri kupokea madawati hayo na kueleza kuwa manispaa ya Kinondoni bado ina uhitaji wa madawati, huku akiwataka wadau kujitokeza kusaidia Serikali katika kuchangia sekta ya elimu.

“Ni jambo jema lililofanywa na wahisani wetu kwani tunapenda kuona kila mtoto anasoma katika mazingira rafiki na yenye staha. Hili ni jukumu letu sote kama jamii na sio kuiachia Serikali pekee," amesema Chitegese.

Mbali na hayo Chitegese amesema wilaya ya Kinondoni ina upungufu wa madawati lakini Serikali kupitia bajeti zake inajitahidi kupunguza uhaba huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Gardaworld, Goodluck Lukumani amesema samani za darasani zina mchango mkubwa kwa mwanafunzi kumsaidia katika masomo yake.
Jimbon kwa ponjoro mzee wa kuchezesha kamar
 
Back
Top Bottom