Jimboni kinondoni: Shule ya Mtambani wanafunzi wanakaa chini

Jimboni kinondoni: Shule ya Mtambani wanafunzi wanakaa chini

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,433
Reaction score
139,501
Kukosekana kwa madawati ya kutosha Shule ya Msingi Mtambani iliyopo Bunju - Kinondoni jijini Dar es Salaam kumesababisha baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa sakafuni, jambo linalowakosesha utulivu.

Kukosekana kwa madawati ya kutosha Shule ya Msingi Mtambani jijini Dar es Salaam imefanya baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa sakafuni jambo linalowakosesha utulivu.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002, hadi sasa ina wanafunzi 2,606 huku ikiwa na madawati 580 kati ya 865 yanayohitajika.
Idadi hii inaleta upungufu wa asilimia 33 wa madawati endapo wanafunzi watatu watachangia dawati moja na hiyo kufanya wanafunzi 867 kukaa chini.

Hayo yamesemwa leo Juni 5, 2025 na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Venance Mwasamakwela, wakati akikabidhiwa madawati 65 kutoka kampuni ya ulinzi ya Gardaworld.

Amesema kwa muda mrefu wanafunzi wamekuwa wakikaa chini au kushirikiana madawati kutokana na uhaba mkubwa wa samani hizo.
"Tunashukuru sana wahisani wetu kwa kuzawadiwa madawati 65 kutoka Gadaworld ambapo itapelekea kupunguza msongamano darasani kwenye ukaaji kwani wanafunzi 195 watakuwa wamepata pakukaa," amesema Mwasamakwela.

Mwasamakwela amesema msaada huo utakwenda kuongeza ari ya kujifunza kwa wanafunzi, huku akiahidi kuyalinda madawati hayo ili yatumike kwa muda mrefu.
“Sasa tuna upungufu wa madawati 224.”

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, Chitegese Dominic Ngaluku amekiri kupokea madawati hayo na kueleza kuwa manispaa ya Kinondoni bado ina uhitaji wa madawati, huku akiwataka wadau kujitokeza kusaidia Serikali katika kuchangia sekta ya elimu.

“Ni jambo jema lililofanywa na wahisani wetu kwani tunapenda kuona kila mtoto anasoma katika mazingira rafiki na yenye staha. Hili ni jukumu letu sote kama jamii na sio kuiachia Serikali pekee," amesema Chitegese.

Mbali na hayo Chitegese amesema wilaya ya Kinondoni ina upungufu wa madawati lakini Serikali kupitia bajeti zake inajitahidi kupunguza uhaba huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Gardaworld, Goodluck Lukumani amesema samani za darasani zina mchango mkubwa kwa mwanafunzi kumsaidia katika masomo yake.
 
Sio jimboni kwake tu, ni nchi nzima kiufupi haya majinga yameshindwa kila kitu yanabaki yanajihami kwa kuteka na kuua, NRNE
Wakiwa bungeni kumtetea mama utazani wao ndio abduli na mchengerwa
Wanasema hawadai.Yaani kila kitu majimboni mwao ni safi,mwororo,maridadi,dukinaa,dangachee,shega sanaaaa!
 
Mleta uzi,ni watoto wa Rais, waziri na makatibu/wauirugenzi tu ndiyo hukaa kwenye viti/madawati.Ninyi wengine mtajicheki.
Kuna mtu nilimpa kazi ya kunitafutia mtoto japo mmoja wa DED, DC, DAS,DSO,Mbunge,Katibu wa CCM wa Wilaya,DPO, DIO, DEO, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya anayesoma kwenye shule ya St. Kayumba (shule za msingi za kawaida za serikali) kwenye wilaya yake anaishi, na akimpata nitampatia milioni moja.

Mpaka kesho anasema hajaona.
Yaani hao wanaosifia shule za serikali kuwa elimu imeboreshwa na "mama yao" ndio hao hao ambao watoto wao huwakuti kwenye hizo shule.

Huyo jamaa alichoniambia baada ya kukosa mtoto wa kiongozi anayesoma shule za msingi za serikali, alikiri kuwa wanadanganywa sana na hawa viongozi.
Kama shule ni bora na kimiundombinu na kimasomo, kwa nini watoto wao hawasomi huko!!?
 
LIKUD njoo upige milioni huku
 
Kwa msiomjua Ponjoro wa pwani
FB_IMG_1749280660059.jpg
 
Ponjoro according to his CV, he studied his first degree within a year at UDSM.
Katika mambo ambayo JPM alikosea sana katika utawala wake ni kuachia Bunge lae lijae watu wenye elimu ya kuungaunga na wale wa darasa la saba.
 
Katika mambo ambayo JPM alikosea sana katika utawala wake ni kuachia Bunge lae lijae watu wenye elimu ya kuungaunga na wale wa darasa la saba.
Hii elimu ya wabunge na mawaziri kwa wengi ni wa kuandikiwa essays na thesis. Siku moja waweke heading na wawape wabunge karatasi, kila mmoja aandike essay ya maneno 500 ndiyo atoke nje ya jengo. Ninaamini wengi watalala mjengoni.
 
Back
Top Bottom