Jimbo la Songea lapata askofu mpya

Jimbo la Songea lapata askofu mpya

Lini jimbo kuu la Songea litatoa askofu?

Limetoa askofu wa Lindi Bruno Ngonyani, Askofu Mstaafu wa Mbinga Emmanuel Mapunda na hata zaman Mbinga ikiwa sehemu ya Songea alitoka Askofu Mkuu Komba na Askofu Maurus komba wa zamani Tanga wote sasa ni marehemu!
 
Kwa nini jimbo la lringa linatoa maaskofu wengi nchini? Huyo Dallu wa lringa, Mtega nae wa lringa, kuna Chengula-Mbeya wa lringa.

Tosamaganga iliyopo mkoa wa Iringa ni kitovu cha elimu na ukatoliki kwa muda mrefu sana; hivyo wanyalukolo wengi walipata nafasi ya kusoma hapo na baadae kupata upadri ukilinganisha na sehemu nyingine!!!
 
Hongera yake, sasa jimbo la Geita linaongozwa na nani?
 
Limetoa askofu wa Lindi Bruno Ngonyani, Askofu Mstaafu wa Mbinga Emmanuel Mapunda na hata zaman Mbinga ikiwa sehemu ya Songea alitoka Askofu Mkuu Komba na Askofu Maurus komba wa zamani Tanga wote sasa ni marehemu!

Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu
 
Kwa nini jimbo la lringa linatoa maaskofu wengi nchini? Huyo Dallu wa lringa, Mtega nae wa lringa, kuna Chengula-Mbeya wa lringa.

Umeanza wivu,umewasahahu wengine.... Tarcisius Ngalalekumtwa Askofu wa Iringa -mzaliwa wa Iringa,Paskal Kikoti Askofu wa Mpanda -mzaliwa wa Iringa
 
Huyu Askofu Norbert Mtea kuna jambo amelifanya na ndio maana amejiuzulu na kwa taharifa ni kuwa hayupo Tanzania yupo Ujeeumani na afya yake ni nzuri tu...

No research no right to speak! Si vyema kupika majungu yasiyo na kichwa wala miguu. Huu ni uzushi. Vinginevyo leta concrete evidence to prove your unfounded allegations.
 
Naomba totauti ya jimbo kuu na jimbo la kawaida, madaraka na mipaka ya maaskofu husika. Mimi sio Mkatoliki, naomba kujuzwa.

Majimbo makuu au kwa jina lingine Metropolitan ni majimbo au jimbo linalosimamia majimbo mengine. Huwa linaongozwa na Askofu Mkuu au Kadinali (kwa uchache sana). Kwa Tanzania yamegawanywa kikanda, kwa upande wa Kusini ni Metropolitan ya Songea yenye Askofu Mkuu (mteule) Damian Dallu ikiwa inasimamia majimbo ya Mbeya, Iringa, Njombe, Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara na Lindi; kanda ya kati na magharibi ni Metropolitan ya Tabora chini ya Askofu Mkuu Paul Ruzoka inasimamia majimbo ya Singida, Rukwa, Mpanda na Kigoma; upande wa kaskazini ni Metropolitan ya Arusha ikiongozwa na Askofu Mkuu Josephat Lebulu ikisimamia majimbo ya Mbulu, Moshi, Same na Tanga; upande wa Mashariki ni Metropolitan ya Dar es Salaam ikiongozwa na Polycarp Kadinali Pengo akisaidiwa na maaskofu Wasaidizi (Auxiliary Bishops) Eusebius Nzigilwa na Titus Mdoe ikisimamia majimbo ya Morogoro, Dodoma, Mahenge, Zanzibar na Ifakara na kwa kanda ya ziwa metropolitan ya Mwanza ikiongozwa na Askofu Mkuu Yuda Tadei Ruwaichi (OFMCap) ikisimamia majimbo ya Mara, Bunda, Geita, Shinyanga, Ngara, Rulenge na Bukoba.
 
Fr Norbert Mtega, Fr Kikoti marehemu kwa sasa Mungu amrehemu, Fr Damian Dallu, Fr NgalaleKumtwa, Fr Chengura huyu anatokea jimbo la Njombe, Fr Mario Mgulunde

Kwa nini jimbo la lringa linatoa maaskofu wengi nchini? Huyo Dallu wa lringa, Mtega nae wa lringa, kuna Chengula-Mbeya wa lringa.
 
Seminari kuu ya Peramiho.

Kwa nini jimbo la lringa linatoa maaskofu wengi nchini? Huyo Dallu wa lringa, Mtega nae wa lringa, kuna Chengula-Mbeya wa lringa.

Si Iringa tu kuna majimbo mengine yana historia ya kutoa maaskofu kwa wingi. Mfano jimbo la Bukoba Ukianzia kwa askofu Nkaranga, Timanywa, Kyaruzi nafikiri yupo Sumbawanga, Rweyongeza yupo jimboni Karagwe, Rwoma alikuwa Singida, Kiraini Method yupo Bukoba ,Marehemu Cardinal Rugambwa na Askofu Mwoleka aliyekuwa Karagwe. Vile vile kuna askofu Rugambwa mwingine ambaye ni balozi wa papa sikumbuki nchi gani.
 
Majimbo makuu au kwa jina lingine Metropolitan ni majimbo au jimbo linalosimamia majimbo mengine. Huwa linaongozwa na Askofu Mkuu au Kadinali (kwa uchache sana). Kwa Tanzania yamegawanywa kikanda, kwa upande wa Kusini ni Metropolitan ya Songea yenye Askofu Mkuu (mteule) Damian Dallu ikiwa inasimamia majimbo ya Mbeya, Iringa, Njombe, Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara na Lindi; kanda ya kati na magharibi ni Metropolitan ya Tabora chini ya Askofu Mkuu Paul Ruzoka inasimamia majimbo ya Singida, Rukwa, Mpanda na Kigoma; upande wa kaskazini ni Metropolitan ya Arusha ikiongozwa na Askofu Mkuu Josephat Lebulu ikisimamia majimbo ya Mbulu, Moshi, Same na Tanga; upande wa Mashariki ni Metropolitan ya Dar es Salaam ikiongozwa na Polycarp Kadinali Pengo akisaidiwa na maaskofu Wasaidizi (Auxiliary Bishops) Eusebius Nzigilwa na Titus Mdoe ikisimamia majimbo ya Morogoro, Dodoma, Mahenge, Zanzibar na Ifakara na kwa kanda ya ziwa metropolitan ya Mwanza ikiongozwa na Askofu Mkuu Yuda Tadei Ruwaichi (OFMCap) ikisimamia majimbo ya Mara, Bunda, Geita, Shinyanga, Ngara, Rulenge na Bukoba.

Najiuliza ni vigezo gani huwa wanatumia kuchagua Mkoa fulani kuwa Metropolitan......Tafadhali hebu nisaidie hapo..
 
Kwa tafsiri nyepesi ni kama kanda; kwamba nchi hugawanywa katika kanda mbalimbali halafu kunakuwa ma makao makuu ya kanda
Vivyo hivyo kanisa Katoliki imegawa nchi ya Tanzania katika katika majimbo makuu kadhaa ambayo ni pamoja na jimbo kuu la Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Songea, Tabora Dodoma na mengine ambayo sina uhakika wa kuyataja. Kila jimbo kuu linakuwa na majimbo mengine yaliyo chini yake. Mgawanyo wa mipaka ya jimbo kuu haiangalii mikoa na inaweza kuunganisha mikoa kadhaa katika jimbo moja kuu

Dodoma sio Jimbo kuu mkuu...
 
Fr Norbert Mtega, Fr Kikoti marehemu kwa sasa Mungu amrehemu, Fr Damian Dallu, Fr NgalaleKumtwa, Fr Chengura huyu anatokea jimbo la Njombe, Fr Mario Mgulunde

Fr Chengula si wajimbo la njombe amezaliwa njombe lakini yuko registered jimbo la iringa.
Maaskofu kutoka Jimbo la Iringa ni
1. Mario Mgulunde marehemu sasa
2. Evaristo Chengula Mbeya sasa
3. Ngalalekumtwa Iringa
4. Kikoti marehemu sasa
5. Lunyungu jimbo la tunduru masasi sasa amestaafu
6. Msemwa tunduru masasi
7. Damian Dallu huyu sinauhakika kama yuko registered Iringa ingawa amekulia na kusoma iringa kama sikosei
8. Norbert Mtega Songea ila amestaafu.
Hawa ndo maaskofu kutoka jimbo la iringa.
 
Back
Top Bottom