Jimbo la Songea lapata askofu mpya

Jimbo la Songea lapata askofu mpya

Hongera baba Damian Dallu.. ni mpenda umoja naamin ataiunganisha Songea vyema.
 
Papa Francis amemteua askofu Damian Dallu wa jimbo la Geita kuwa askofu Mkuu wa Jimbo la Songea. Anachukua nafasi ya Mhashamu askofu mkuu Dkt Norbert Mtega aliyestaafu.
 
Baba Mtakatifu Fransic amemteua Askofu Damian Dennis Dallu wa Jimbo la Geita kuwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Songea,hivyo kwa sasa Jimbo kuu la Songea litaongozwa na Askofu Mkuu Damian Dennis Dallu.
Nafasi hiyo imezibwa baada ya Askofu Nobert Wendelin Mtega kuachia nafasi kutokana na matatizo ya kiafya.
Askofu Damian Dennis Dallu alizaliwa mwaka1956 Kijiji cha Kiponzero,Parokia ya Ifunda,Jimbo katoliki la Iringa,baada ya masomo,malezi na majiundo yake ya kitume alipadirishwa 15/11/1984,Baba Mtakatifu Yohane Paul II alimteua Askofu wa pili wa Jimbo la Geita 06/05/2000 na 30/07/2000 aliwekwa wakfu kuwa askofu wa Geita.
Akizungumza leo na Radio Vatican,Askofu Mkuu D.D.Dallu amesema kwa miongozo ya katekisimu ya Kanisa katoliki na Mtaguso wa pili wa Vatican vinatoa muongozo wa uinjilishaji katika ulimwengu wa sasa wenye changamoto ya utandawazi,nafasi ya kuimarisha haki za binadamu na utu wa mwanadamu,Ametoa mwaliko wa kanisa katoliki kukuza mashauriano na ushirikiano wa kidini katika ulimwengu wa leo.
Kila la kheri waumini wa jimbo Kuu la Songea,ambapo metopolitan yake ni majimbo ya Mbeya,Njombe,Mbinga,Iringa,Mtwara,Lindi na Tunduru-Masasi,hivyo Askofu mkuu Dallu atasimamia majimbo hayo.
BRAVO S.E MONS DAMIAN DENIS DALU
 
Naomba totauti ya jimbo kuu na jimbo la kawaida, madaraka na mipaka ya maaskofu husika. Mimi sio Mkatoliki, naomba kujuzwa.
 
Hongera Askofu mkuu D Dallu. Mwalimu wangu nikiwa seminari miaka hiyo.
 
Hongera sana Askofu Dallu na Kila la kheri katika kazi yako ngumu ya kuliongoza jimbo kuu la Songea. Sikujua kama Askofu Mkuu Mtega ni mgonjwa au amezeeka anahitaji mapumziko. Times change! Ni mzee sana sasa.
 
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Damian Denis Dallu wa Jimbo Katoliki Geita, Tanzania kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Dallu alizaliwa kunako Mwaka 1956 huko Kiponzelo, Jimbo Katoliki la Iringa.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 15 Novemba 1984. Tarehe 6 Mei 2000 akateuliwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Tanzania. Askofu Dallu aliwekwa wakfu na hatimaye kusimikwa kuwa ni Askofu wa pili wa Jimbo la Geita hapo tarehe 30 Julai 2000.

Katika mahojiano maalum na Radio Vatican, Askofu mkuu mteule Dallu anazungumzia umuhimu wa Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki kama muhtasari wa imani inayoungamwa na kuadhimishwa na Mama Kanisa. Hii ni imani inayomwilishwa katika maisha adili kwa kufuata Amri za Mungu na kumwilishwa katika sala. Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki imetoa kipaumbele cha pekee katika Mafundisho Jamii ya Kanisa kwa kutoa kipaumbel cha kwanza kwa binadamu na haki zake msingi.

Askofu mkuu mteule Damin Denis Dallu anasema, Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican ni nyenzo msingi katika maisha na utume wa Kanisa katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za kichungaji katika ulimwengu mamboleo. Ni mwaliko kwa Kanisa kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kiekumene ili kujenga misingi ya haki na amani kwa Familia nzima ya binadamu. Kumbe, Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki na Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican ni mafundisho mfungamano kwa binadamu wote.


Nyongeza yangu
Itakumbukwa kuwa Jimbo Kuu la Songea lilikuwa wazi tangu Mei 13, 2013 pale Askofu Mkuu Norbert Wendelin Mtega alipojiuzulu rasmi kutokana na hali ya kiafya kuwa si nzuri.
Askofu Mtega alikuwa ni mwenyeji wa Jimbo la Njombe na kabla ya hapo alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Iringa. Huyu naye pia ni mwenyeji wa Jimbo la Iringa. Kutoka usukumani hadi Ungonini. Kutoka Mwadela hadi jalelu va kunyumba.

Chanzo: Askofu Dallu ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea, Tanzania
 
Huyu Askofu Norbert Mtea kuna jambo amelifanya na ndio maana amejiuzulu na kwa taharifa ni kuwa hayupo Tanzania yupo Ujeeumani na afya yake ni nzuri tu...
 
Huyu Askofu Norbert Mtea kuna jambo amelifanya na ndio maana amejiuzulu na kwa taharifa ni kuwa hayupo Tanzania yupo Ujeeumani na afya yake ni nzuri tu...

Serious? Kafanya nini?

Hongereni wana Songea kwa kupata Askofu Mkuu mpya

Cc Fixed Point snowhite
 
Last edited by a moderator:
Naomba totauti ya jimbo kuu na jimbo la kawaida, madaraka na mipaka ya maaskofu husika. Mimi sio Mkatoliki, naomba kujuzwa.

Kwa tafsiri nyepesi ni kama kanda; kwamba nchi hugawanywa katika kanda mbalimbali halafu kunakuwa ma makao makuu ya kanda
Vivyo hivyo kanisa Katoliki imegawa nchi ya Tanzania katika katika majimbo makuu kadhaa ambayo ni pamoja na jimbo kuu la Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Songea, Tabora Dodoma na mengine ambayo sina uhakika wa kuyataja. Kila jimbo kuu linakuwa na majimbo mengine yaliyo chini yake. Mgawanyo wa mipaka ya jimbo kuu haiangalii mikoa na inaweza kuunganisha mikoa kadhaa katika jimbo moja kuu
 
Kwa nini jimbo la lringa linatoa maaskofu wengi nchini? Huyo Dallu wa lringa, Mtega nae wa lringa, kuna Chengula-Mbeya wa lringa.
 
Back
Top Bottom