Willy unapochokoza mada kama hizi usikimbie kaa hapa tukufunde ili uwe na uwelewa wa kile unachotamani au kutaka kukifanya uwe na uhakika nacho.
Jimbo la Segerea ukiwa kama mgombea wa CCM kuna kata za Vingunguti, Buguruni, kipawa na kiwalani, kihistoria hili jimbo ni la Waswahili wa pwani hasa hizi kata nilizokupa orodha yake hizo kata kwa wanaCCM uzaramo na Uislamu ni moja ya advantage ya mgombea.
Kwa ninavyowafahamu mimi wanaCCM wenzako kwa jimbo hili unatwanga maji kwenye kinu, kuna mtu mmoja anaitwa Joseph Kessy yeye ndiyo alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Maendeleo ya Tabata na Tabata unayoina leo ni mchango mkubwa wa Joseph Kessy lakini amegombea mara 2 mfululizo na huyu Makongoro hakufuwa dafu.
Sifa kuu na umahiri wa Makongoro anawafahamu fika wanaCCM wa jimbo hili kwahiyo yeye huwa anawaandalia bahasha zao basi mchezo unakuwa umekwisha
CCM jimbo la Segerea sasa hivi iko vipande vipande wana siasa za makundi kuliko CCM ngazi ya Taifa tofauti tu ni kwamba wao hawapati coverage ya media.
Usitake kuvuna ambacho haujakipanda nakushauri ufanye research kule kwenu Mtera tatizo lao kubwa ni nini na uanze kuwatatulia hayo matatizo kabla hata ya kugombea, hii ndiyo njia aliyoitumia George Simachawene kule kwao Kibakwe licha ya kwamba yeye tunaishi jimbo moja la Segerea na anakaa kata ya Vingunguti.