Jimbo la Njombe Kusini waikataa ccm

Jimbo la Njombe Kusini waikataa ccm

Unao waona kwenye picha waliletwa na fuso lililotumwa kusomba watu toka Uwemba ambalo lilifanikiwa kurudi
 
1463281_582839551788696_213913354_n.jpg


Umeona hapa ni Njombe alikuwepo Kinana, Nape na Migiro alijaza nyomi uwanja huu
Kama Kinana na Nape wanao aminika wana weza kuvuta watu wanaweza kupata idadi hii kweli ccm siimeisha?
 
Nasikia hata Jar people mwenye kusema "Nime wapenda ghafla "alikuwepo akijaribu kuongea kibena wapi!
 
Nasikia mmoja wao alipendekeza Aitwe Makinda ili awafunde kwa kibena lakini wanao wajua wabena wakasema akija Makinda hata hawa kiduchu wataondoka wote
 
CCm ina zidi kupata wakati mgumu majimbo mbalimbali nchini likiwemo hili linalo ongozwa na spika Anne Makinda.viongozi wa ccm wanajaribu kuiokoa hali hiyo lakini bado mambo ni magumu muno!Ikumbukwe ni majuzi tu Katibu mkuu wa ccm mwenyewe alijionea hali hiyo alipo jaribu kwenda kubadili upepo lakini wale wa bena walimkatalia katakata kuhutubiwa.Kwa watu wanao fahamu tabia ya wabena nasikia ni wagumu muno kudanganywa.Kumbuka hata jaribio la kusomba watu watu jimbo la jirani la Deo Sanga kule Lupembe napo ilishindikana baada ya mafuso kukwama kutokana na mvua kubwa iliyo nyesha. Ali sikika mtu mmoja akisema tatizo wa bena wakiona unawadanganya hata ukiwasalimia Kamwene hawakuitikii.Mtu aliye karibu na siasa za Njombe anasema huenda ndiyo sababu Anne Makinda hataki kugombea tena.Aliongeza kusema afadhali kidogo Wahehe wanaweza kupokea hela ingawa nao kura hakupi.Lakini mbena akikukataa hata hela hawataki.Mama Makinda anawajua sana ndiyo maana hataki kurudia akihofu kuaibika


Kwa ANNA MAKINDA SHERIA MPYA KUWA SPEAKER sio lazima UWE MBUNGE -- Kwahiyo atagombea USPEAKER bila ya kuwa MBUNGE...

Sasa hii Issue ya UBENA na KAMWENE havitamgusa hata kidogo...
 
Mama Makinda alisema kuwa hatogombea tena Ubunge kwani wananchi wanamwomba sana pesa kila kaienda jimboni, nadhani ni uamuzi mzuri apumzike na alinde hadhi yake au asije akawa anataka agombee uspika 2015, kama alivyofanya Pius Msekwa 2000.

Hadhi anaitoa wapi?
 
Teh teh, subirini maccm wamwage mapesa mwaka 2015 hapo njombe kama wabena hawatachanganyikiwa na kutoa kura kwa wingi kwa maccm kama wamelewa!
 
Makinda anajiandaa kugombea upresido sikilizia timbwili zake endapo akipata... itakuwa zaidi ya comedy za majuto na inye
 
Wale watu ni fuso moja tu lililo tumwa Uwemba lililo fanikiwa kurudi
 
Taarifa zaidi zinasema hata jimbo la Engineer Gerson Lwenge nalo hali ni mbaya.Nasikia wanjuta kumchagua
 
Mama Makinda alisema kuwa hatogombea tena Ubunge kwani wananchi wanamwomba sana pesa kila kaienda jimboni, nadhani ni uamuzi mzuri apumzike na alinde hadhi yake au asije akawa anataka agombee uspika 2015, kama alivyofanya Pius Msekwa 2000.

Ndugu yangu nina wasiwasi na part ya mwili unachotumia kufikiria ,, kwa taarifa yako Njombe ni moja ya mikoa ambayo watu wake wana maisha mazuri kutokana na kwamba kuna uhakika wa chakula, watu wajitahidi kuwa na nyumba bora tofauti na mikoa mingine ,,Ukiwa Njombe huwezi ona vijumba vya nyasi kama vilivyopo Chalinze na sio ombaomba kama ulivyopotosha,, hata ukija kifedha wana Njombe tumebarikiwa kuipata hali ya hewa inayoturuhusu kupanda miti ya mabao na nguzo za umeme ambayo inatuingizia mamilioni ya pesa,, hata mazao ya chakula pia yanatuingizia pesa za kutosha mfano mzuri ni viazi na mahindi,, kwa hyo kwa ww kusema tunamwomba pesa Mikinda umetudhalilisha wana Njombe ,, Anna Makinda anaona aibu kakaa miaka mingi madarakani lakini hajafanya chochote kijijini kwake tu ofisi imeezekwa kwa nyasi ,Pia imefika wakati ameona ataumbuka kwani kakosa sapoti hata kutoka kwa wana CCM wenyewe ndio maana CCM wenyewe wamemuandaa Deo Mwanyika (yule wa African Barrick Gold).
 
Mama Makinda alisema kuwa hatogombea tena Ubunge kwani wananchi wanamwomba sana pesa kila kaienda jimboni, nadhani ni uamuzi mzuri apumzike na alinde hadhi yake au asije akawa anataka agombee uspika 2015, kama alivyofanya Pius Msekwa 2000.

acha ujinga wana Njombe hatujawa ombaomba kihivyo
 
Back
Top Bottom