TANZIA: Dr.Hilman Ndembelwa Ngunangwa Mbunge wa Njombe Kusini 1990-1995 Afariki

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
17,287
10,700
RIP Dr.Hilman Ndembelwa Ngunangwa Mbunge wa Njombe Kusini 1990-1995.
Amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Taratibu za kusafirisha msiba kurudi Njombe zinafanyika Nyumbani kwake Changanyikeni Dar.Msomi wa masuala ya Uongozi,hata kuwa na Phd ya ukweli/jasho, Dr Hilman Ndembelwa Ngunangwa. Ambaye alikuwa Mhadhiri ktk Chuo cha MANTEP, Bagamoyo hadi 1990 alipogombea na kushinda nafasi ya ubunge Jimbo la Njombe-Kusini.

Kabla ya kushindwa kwa kuchakachuliwa na CCM+Anne Makinda 1995, itakumbukwa kuwa akiwa Bungeni, yeye alikuwa ni miongoni mwa wale
Wabunge 55 walioitaka serikali ya Tanganyika irudishwe. Wabunge wengine walikuwa ni Njeru Kasaka na Pius Msekwa.
 
  • Thanks
Reactions: Gor
RIP in Dr. Ngunangwa!

Nakumbuka Malecela akiwa PM, Dr. Ngunagwa aliwahi kumwambia bungeni, kwamba falsafa anayoongea ni ya juu sana kwa Malecela kuifahamu/kuielewa. Ni watu tu wenye doctorate kama yeye (huku akionesha kidole chake alichovaa pete ya ud doctorate) wanaweza kufahamu.

Hivyo akamshauri PM Malecele atumie wataalamu katika ofisi yake, wamusaidie kuelewa falsafa aliyoongea bungeni. Aaikuwa msomi aliyeamini usomi wake.
 
Ndio huyu aliyemuuliza Anne Makinda wakati alipokuwa anataka kugombea ubunge kipindi kile kama sikosei ni mwaka 1995 kwa lugha yao ya asili kama sikosei ni kibena Alikwina?
 
Daaaah huwezi amini lakini ndio imeshatokea. Nitakukumbuka kwa swali lako ulilouliza "Siasa za Tanzania ni za kurithishana" ?. Mfano kikwete. , Mwinyi. Makamba , Sokoine, et al
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom