Jimbo la Musoma mjini kurudi kwa CCM?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Chadema Musoma Wanaharakati

Japokuwa Musoma ni jimbo linaloongozwa na majembe ya CHADEMA kila kona, lakini sifurahishwi na utendaji wa baadhi ya madiwani pamoja na mbunge wake waliopewa ridhaa na wananchi kuwaongoza. Huu ndio muda muaafaka wa sisi kujipanga ili kuhakikisha jimbo hili pamoja na kata zake zinabaki mikononi mwetu 2015.

Kata ya mwisenge ambayo iko chini ya Mheshimiwa Bwire Nyamwero Bwire (DIWANI-CHADEMA),ndio kata inayolalamikiwa sana na wananchi wake kutokana na mheshimiwa huyu kutokuwa karibu na watu wake. Mwaka juzi tulichagua viongozi wa matawi na kata,lakini hadi leo imebaki kuwa simulizi tu,kwani viongozi hawafanyi kazi zao ipasavyo kwani ni wanafiki,mafisadi na ni waoga.
Hali hii inawapa wenzetu wa CCM kuendelea kujiimarisha wakati walikuwa wameisha lowa tepetepe..

Pongezi nyingi ziende kwa diwani wa makoko Mh. RENATUS ALLOYCE kwani ameonyesha kuwajali sana wapiga kura wake na wale wote wanaoendeleza harakati za kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa BEBERU CCM.

Pamoja tunaweza.

PEOPLESS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kurudi magamba sahau labda sema huyo diwani kibarua kitaota majani na kata itachukuliwa na jembe jingine toka CDM,watu enye akili nzuri wako CDM kwa sasa
 
Japokuwa Musoma ni jimbo linaloongozwa na majembe ya CHADEMA kila kona, lakini sifurahishwi na utendaji wa baadhi ya madiwani pamoja na mbunge wake waliopewa ridhaa na wananchi kuwaongoza. Huu ndio muda muaafaka wa sisi kujipanga ili kuhakikisha jimbo hili pamoja na kata zake zinabaki mikononi mwetu 2015.

Kata ya mwisenge ambayo iko chini ya Mheshimiwa Bwire Nyamwero Bwire (DIWANI-CHADEMA),ndio kata inayolalamikiwa sana na wananchi wake kutokana na mheshimiwa huyu kutokuwa karibu na watu wake. Mwaka juzi tulichagua viongozi wa matawi na kata,lakini hadi leo imebaki kuwa simulizi tu,kwani viongozi hawafanyi kazi zao ipasavyo kwani ni wanafiki,mafisadi na ni waoga.
Hali hii inawapa wenzetu wa CCM kuendelea kujiimarisha wakati walikuwa wameisha lowa tepetepe..

Ukaribu upi unaotaka wauonyeshe...au kwa lugha nyingine , unataka wafanye kipi ambacho hawakifanyi? Ni bora uwaeleze ukweli wajue nini cha kufanya kuliko kuacha mambo juu juu hivi....utaonekana unawapiga majungu pengine 'ulibwangwa udiwani' or something. Wasaidie kwa kuwaambia do this or do not do this....simple!
 
Mnataka mbunge na madiwani wawe karibu na wananchi kwa kutoa michango ya misiba, kutoa misaada ya 'hela ya kula' kama ilivyozoeleka kwa wananchi wengi;Nk.
Wananchi wengine wamezoea ubunge wa ccm..
 
Chadema Musoma Wanaharakati

Japokuwa Musoma ni jimbo linaloongozwa na majembe ya CHADEMA kila kona, lakini sifurahishwi na utendaji wa baadhi ya madiwani pamoja na mbunge wake waliopewa ridhaa na wananchi kuwaongoza. Huu ndio muda muaafaka wa sisi kujipanga ili kuhakikisha jimbo hili pamoja na kata zake zinabaki mikononi mwetu 2015.

Kata ya mwisenge ambayo iko chini ya Mheshimiwa Bwire Nyamwero Bwire (DIWANI-CHADEMA),ndio kata inayolalamikiwa sana na wananchi wake kutokana na mheshimiwa huyu kutokuwa karibu na watu wake. Mwaka juzi tulichagua viongozi wa matawi na kata,lakini hadi leo imebaki kuwa simulizi tu,kwani viongozi hawafanyi kazi zao ipasavyo kwani ni wanafiki,mafisadi na ni waoga.
Hali hii inawapa wenzetu wa CCM kuendelea kujiimarisha wakati walikuwa wameisha lowa tepetepe..

Pongezi nyingi ziende kwa diwani wa makoko Mh. RENATUS ALLOYCE kwani ameonyesha kuwajali sana wapiga kura wake na wale wote wanaoendeleza harakati za kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa BEBERU CCM.

Pamoja tunaweza.

PEOPLESS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Huyu ndio yule BWIRE aliyekuwa AZANIA ya Kwayu?
 
Mbona hii haitishi mkuu, labda huyo jamaa wa kata ya Mwisenge ndo tatizo lakini jimbo hili kututoka ni ngumu sana.
 
download
 
Kama kuwa karibu na wananchi anakotaka huyu mleta mada hatosheki nako basi ahamie jimbo la Ilala kwa Zungu, yeye misiba yote anatoa turubai viti ubwabwa na shiling 50,000/ ubani, maendeleo mtajijuwa wenyewe.

Kama huu ndio ukaribu kwa Wananchi basi wewe mleta mada ni zuzu na huna tofauti na yule mbunge aliyenunuwa majola ya sanda na kuyagawa kwenye misikiti ya jimbo lake.
 
Mtoa mada ameshindwa kutetea alichokiandika,jimbo litarudi ccm kwasababu zipi?

Nina imani kubwa kwa mbunge wa musoma mjini!kwa mambo anayofanya jimboni kwake hakika mfano bora wakuigwa.
 
musoma wana tabia mbaya inawezekana mbunge kafanya mazuri lakini safari ijayo waamua wambadilishe bila sababu ya msingi angalia rekodi za wabunge wengi wa musoma mjini wananchi huwa na tabia ya kuwachoka wabunge wao hawakai nao muda mrefu
 
Najua CDM wamefanya mambo mengi mazuri kwa wananchi wa Musoma nitawashangaa sana jambo hilo likitokea.
 
Mleta mada kwa taarifa nilizo nazo manispaa hiyo watoto hawalipi ada mashuleni tangu chaema ilipo pata nafasi ya kuongoza..
Kuna madara mengi sana ambayo serikali ya CCM ilikuwa imeshindwa kuyajenga tangu uhuru lakini manispaa hiyo ikiwa chini ya chadema imefanikiwa kujenga tena kwa muda mfupi tu..
je hayo mawili ni uongo au ni kweli?....Nitarudi
 
Kuna wanaodai mbunge ana elimu ndogo kiasi kwamba akiwa kwenye vikao mfano baraza la madiwani mambo mengi yanamshinda.wanataka chadema itafute kamanda mwingine mwenye elimu nzuri zaidi ya nyerere
 
Umeranzisha topic sensitive halafu umeilambalamba tu. Kichwa kikubwa kuliko kiwiliwili cha topic.
Kwa hiyo tatizo la Nyerere ni elimu, je wakati wanamchagua alikuwa na elimu gani? Why it didnt matter then?
 
hata mimi naomba iwe hivyo ila wananchi wa musoma wanasema wanataka mbunge mwenye elimu ya juu zaidi ya mh.vicent nyerere
kama ni suala la elimu mbona MATHAYO VEDA ni kilaza hata FORM FOUR hajafika?? unafikiri kwa siasa za ccm kuna mtu wa ccm mwenye uwezo wa kuchukua kadi ya kushindana na VEDA MANYINYI??

Pili aliyewahi kuwa nan elimu nzuri ni yule MAGOTI aliyekuwa docta bingwa pale HOSPITALI YA MKOA...ila na yeye kwa ubabe wake na kutowajali wananchi hakuna anayetaka kumkumbuka ndio maana hata aliyemfuata(IBRAHIMU MARWA) ilibidi awe ni mtu wa kawaida sana japo na yeye alikua kilaza wa hatari tena cha pombe mwenye kulewa mpaka anaokotwa majalalani kajisaidia hovyo
Kifupi toka siasa za vyama vingi zianze hakuna mbunge MAKINI na MSIKIVU kama NYERERE na hilo sie tuliokaa musoma kitambo tunalitambua
Labda kama magamba waje na mtu ambaye ni wa elimu ya juu na watu wamkubali sana yeye binafsi kuliko sera za chama chake
 
Back
Top Bottom